Search This Blog

Thursday, December 27, 2012

Tanzania yajitayarisha kuingilia kati mzozo wa DRC

Tanzania inajitayarisha kupeleka majeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kupambana na Kikundi cha Machi 23 (M23) kinachopigana kuiangusha serikali ya Kongo, maafisa wa Tanzania waliiambia Sabahi.
    Mtoto akiwaangalia askari wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakirejea makambini kwao huko Goma siku ya Jumatatu (tarehe 3 Disemba), sku mbili baada ya wapiganaji wa M23 kuondok., Tanzania na nchi nyingine za kanda hiyo zinafanyia kazi juu ya kusuluhisha mzozo huo. [Na Phil Moore/AFP]
  • Mtoto akiwaangalia askari wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakirejea makambini kwao huko Goma siku ya Jumatatu (tarehe 3 Disemba), sku mbili baada ya wapiganaji wa M23 kuondok., Tanzania na nchi nyingine za kanda hiyo zinafanyia kazi juu ya kusuluhisha mzozo huo. [Na Phil Moore/AFP]
Majeshi ya Tanzania yatapelekwa kama sehemu ya misheni ya kulinda amani chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, njia hiyo hiyo ambayo wamekuwa wakipelekwa katika nchi nyingine katika eneo hilo. Msemaji wa jeshi la Ulinzi la Tanzania Kanali Kapambala Mgawe alisema siku ya Ijumaa (tarehe 30 Novemba).
"Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi," aliiambia Sabahi, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika misheni hizo huko Lebanoni, Darfur, Sudani ya Kusini, Visiwa vya Komoro na Liberia.
"Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa," alisema.
Mgawe alisema kuwa kwa vile mzozo wa DRC hauna tishio lolote maalumu kwa Tanzania, viongozi wa kikanda wanazidi kuwa na wasiwasi kuwa hali ya kutokuwepo kwa utulivu unaoweza kusababishwa.
Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wanafanyakzi pamoja ili kuhakikisha kuwa serikali za kidemokrasia katika eneo hilo hazitishiwi au kuangushwa na waasi, na kwamba utawala wa sheria ndio utakaotawala, alisema.
M23 kiliundwa tarehe 4 Aprili mwaka huu na takriban askari 300 walioigeuka serikali ya DRC, wakitaja hali duni jeshini na kutokuwa tayari kwa serikali kuwatekeleza makubaliano ya amani ya tarehe 23 Machi 2009, makaubaliano ambayo yamekipatia jina kikundi hicho.
M23 pia kimemshutumu Raisi wa DRC Joseph Kabila kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi wa Novemba 2011, ambao uchaguzi uligubikwa na upinzani wa vurugu, kuenea kwa matatizo ya vifaa na ukosolewaji wa kimataifa.

Mazungumzo ya amani yenye nguvu

Kutekwa kwa mji wa Goma na M23 hapo tarehe 20 Novemba, mji mkuu wenye utajiri wa rasilimali katika Mkoa wa kaskazini wa Kivu, miezi minane baada ya kuanzisha uasi wao dhidi ya serikali, kulizua hofu ya vita vipana zaidi na matatizo makubwa ya kibinadamu, shirika la habari la AFP liliripoti.
Kukindi hicho kilijitoa kutoka Goma siku ya Jumatatu (tarehe 3 Disemba), ingawaje wapiganaji wake wamebaki karibu na mji na bado hawajarejea nyuma kilomita 20 zilizokubaliwa katika mazungumzo ya kikanda.
Kiongozi wa kisiasa wa M23 Jean-Marie Runiga alisema siku ya Jumanne kuwa kikundi chake kilikuwa tayari kuzungumza na serikali.
Mazungumzo yataanza "siku chache zijazo mjini Kampala", Waziri wa mambo ya Ndani wa DRC Richard Muyej Mangez alithibitisha. Alisema kuwa serikali itapeleka kikosi kamili wakiwemo viongozi muhimu wa kijamii na wajumbe wa bunge la taifa na seneti.
Hata hivyo, Kabila -- ambaye kikundi cha M23 kimemtaka awachie ngazi toka madarakani -- hakitarajiwi kuhudhuria katika mazungumzo ya awali.
Wakati huo huo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa walitoa kile walichosema kuwa ni ushahidi moya ambao "unashikilia imara" shutuma za mwanzo kuwa Rwanda na Uganda viliwasaidia M23.
Ripoti hiyo ambayo AFP iliipata siku ya Jumatatu, inasema kuwa Rwanda na Uganda zilikisaidia M23 katika mashambulizi yake, huku Uganda ikitoa msaada wa vifaa na mama ya majeshi ya Rwanda kujiunga na kikosi ambacho kiliuteka Goma.
Rwanda na Uganda zilikataa katakata kuhusika katika mzozo huo.

Walinda amani wanajiandaa

Wakati taharuki iko juu, Tanzania inaendelea na mipango yake ya kupeleka kikosi kimoja chenye askari kati ya 700 na 800 chini ya uangalizi wa SADC, ikisubiri amri ya Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe alisema.
Mwezi Agosti, nchi wanachama 11 za Mkutano wa Kimataifa juu ya Eneo la Maziwa Makuu (ICGRL) uliomba SADC kupeleka askari 4,000 huko DRC baada ya kuthibitishwa na Kifungu cha 7 cha mamlaka ya Umoja wa Mataifa, inayowapa walinda amani mamlaka ya kuchukua hatua iwapo raia watakuwa katika tishio la mara moja.
Mpaka sasa, Umoja wa Mataifa umeruhusu tu walinda amani kujilinda wenyewe iwapo watashambuliwa chini ya Kifungu cha 6 cha mamlaka yake, ambacho hakiruhusu kuwa na wajibu zaidi ya huo.
"Tunalaani kile waasi wanachofanya huko mashariki mwa Kongo," Membe alisema. "Haikubaliki kwa Tanzania." Ili kuimarisha amani katika DRC, majeshi yanaweza kutumia nguvu ili kutekeleza majukumu yao, alisema.
"Tanzania inawataka waasi waondoke Goma na maeneo mengine muhimu wanayoshikilia ili kuruhusu mazungumzo, au Umoja wa Mataifa utatoa kibali kwa majeshi ya SADC kuwa sehemu ya misheni ya kuyasaidia majeshi ya serikali ya DRC mara moja," alisema.

Vitisho kwa Tanzania

Mzozo wa DRC ni muhimu kwa Tanzania kwa sababu ikiwa utaachwa bila ya kuangaliwa, utakuwa na athari za kijamii na kisiasa kwa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Membe alisema. Tanzania inaweza kukabiliwa na kumiminika kwa wingi kwa wakimbizi ikiwa mzozo utaenea, na kulifanya taifa kuwa katika hatari sana kwa vitisho vya usalama, alisema.
Tanzania imekuwa ikiwapokea wakimbizi kutoka Burundi na DRC tangu miaka ya mwanzo ya 1990. Hadi kufikia mwezi Januari huu, kulikuwa na zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini, nusu yao wakitokea DRC, kwa mujibu wa Kamishna wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi.
Membe alisema kuwa wadau wa kanda lazima waonyeshe uongozi na kufuata mkabala wa kuwa wenye harakati ili kutuliza hali.
Mnamo tarehe 24 Novemba, Raisi Jakaya Kikwete alikutana na Kabila, Raisi wa Uganda Yoweri Museveni, Raisi wa Kenya Mwai Kibaki na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma katika mkutano wa tano wa ICGRL.
ICGRL ilitoa wito kwa M23 kusitisha shughuli zote za vita, na kuzitaka pande zote mbili za M23 na serikali kufungamana na makubaliana yaliyotangulia. Washiriki kwa mkutano huo pia walitoa wito kwa nchi za eneo hilo kuchukua wajibu mkubwa zaidi wa kuhakikisha amani ya DRC.

Hatua za wananchi

Wananchi jijini Dar es Salaam walieleza maoni tofauti kuhusu ama Tanzania ingejishughulisha katika operesheni ya kijeshi huko DRC.
Omary Mkonge, mwenye umri wa miaka 75, alisema anapingana na serikali kupeleka askari huko DRC. "Hakuna haja kwetu kuingilia kati katika vita hivi na vitaigharimu sana nchi yetu," alisema. "Unaona, miaka 33 baada ya vita na Uganda, nchi yetu bado haijatengamaa kiuchumi. Bado tuna makovu ya vita."
Mkonge alisema kuwa serikali inapaswa kutumia nyenzo zake ili kuwasaidia Watanzania, baadhi yao wanaoshi katika umasikini wa kutisha.
Kambarage Manuga, mwenye umri wa miaka 80, yeye alisifia uamuzi wa Tanzania kupeleka wanajeshi kuwalinda wale ambao wako katika hatari ya kuathirika haraka.
"Katika vita vyovyote, kutokana na uzoefu wangu mrefu, wanawake, watoto na wazee ndio wanaoteseka zaidi," aliiambia Sabahi. "Ninaunga mkono hatua hiyo ya serikali yangu kuingilia kati mzozo wa DRC. Huwezi kubakia katika amani ambapo nyumba ya jirani yako inaungua moto.
Source:  http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/features/2012/12/04/feature-02

No comments:

Post a Comment