Wadau wa habari waliokutana jijini Dar es Salaam leo, tarehe
9 Oktoba 2013, wamesikitishwa na hatua ya serikali ya kutosikiliza kilio cha wamiliki
wa vyombo vya habari, wahariri, waandishi, taasisi za vyombo vya habari,
wasambazaji wa magazeti na watu wengine wa kawaida, juu ya kuyaondolea adhabu magazeti
matatu yaliyofungiwa na serikali ya MwanaHALISI, MTANZANIA na MWANANCHI.
Aidha, wadau wamesikitishwa na hatua ya serikali ya kupuuza
kilio chao cha kuomba kusitishwa kwa sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976;
na kudhoofisha mchakato wa kuibadilisha sheria hiyo iliyotajwa na Tume ya Jaji
Francis Nyalali mwaka 1992 kuwa ipo kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Vilevile, tumesikitishwa na hatua ya Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dk. Fenella Mukangara na Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene ya kudharau na kufanya uamuzi wa
kuyafungia magazeti hayo bila kuyasikiliza na kupotosha umma juu ya jambo hilo.
No comments:
Post a Comment