MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Radio
Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na
kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na Bastora
iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake porini.
Habari ambazo zimepatikana na kutoka
wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa
Kigoma Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma
(KPC) Deo Sonkolo imedai mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo
na watu ambao hawajajulikana.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa
njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa waliwasiliana
na waandishi wa wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia
uchunguzi wa Daktari Primus Ijumaa aliyeeleza kuwa mwili wa marehemu umenyonga
ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi mkono wa kushoto.
Mwili wake umepatikana jana katika
pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi
baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea Jumapili siku moja baada ya
kutoonekana kwake.
“Sisi tunaelekea wilaya ya Kakonko
toka Kigoma mjini, lakini walioshuhudia mwili huo huko eneo la tukio waneleza
kwamba kando ya mwili wake kumekutwa Bastora moja, haijafahamika iwapo ilikuwa
inamilikiwa na marehemu ama nani, simu zake mbili na kwa mujibu wa Dkatari
maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi,” alieleza Sonkolo.
Imeelezwa kwamba bastora iliyokutwa
eneo la tukio imekutwa na ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali ya marehemu
ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi
mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo lakini
alisema kwa sasa jeshi lake linangoja taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi
wa mwili wake ikiwa ni pamoja na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo
toka eneo la tukio.
Aidha akizungumza na gazeti hili
Naibu Mharari wa kituo cha Radio Kwizera kinachorusha matangazo kutoka wilayani
Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu, alisema kwamba tokea Januari 5 mwaka huu
walikuwa majira ya saa 11 walikuwa wakijaribu kuwasiliana naye na simu zake
zilikuwa zikiita bila ya kupokelewa mpaka jana ambapo zilikuwa hazipatikani.
“Maelezo kutoka kwa mke wake Rukia
Yunus ni kwamba Marehemu aliondoka nyumbani kwake jioni na kumuaga mkewe kuwa
alikuwa akienda madukani (center) lakini tokea hapo hakurudi wala kuonekana
ambapo ilipofika Jumapili serikali ya kijiji ilianzisha msako mkali kumsaka
mpaka jana asubuhi walipokutana na mwili wake porini,” alieleza Mhariri huyo.
Kwa mujibu wa Naibu Mhariri wa Radio Kwizera ya Ngara Seifu Upupu, Story ya mwisho kuhusu mfugaji aliyekula nyama ya uso ya
kijana aliyekuwa akichunga mifugo yake aliiandika Novemba 24, tukio lililotokea
nove 23, kijiji cha Muhange, wilayani Kakonko mkoani Kigoma.Kijana aliyetajwa kwa jina moja la Susuruka akiwa na majeraha sehemu za uso |
-----------------------------------
STORY HII HAPA
-----------------------------------
Kijana aliyetajwa kwa jina moja la Susuruka amejeruhiwa kwa
kuliwa nyama za sehemu ya uso wake na mwajiri wake aliyekuwa akimfanyia kazi ya
kuchunga ng’ombe katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Saimon Anthony amesema kuwa
tukio hilo limetokea jana usiku (Ijumaa Nov 23, 2012) ambapo aliyefanya unyama
huo ni Bw Imani Paulo.
Amesema kabla ya kumla nyama za usoni mfanyakazi wake, Bw
Paulo alimuua mbwa wake na kisha kula ulimi wa mbwa huyo Jeshi la polisi wilayani
Kakonko limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo
amekamatwa ambapo baada ya kuhojiwa amesema hajui chochote kuhusu matukio hayo.
Taarifa zinasema kuwa majeruhi huyo amepelekwa katika
hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya matibabu
No comments:
Post a Comment