HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza chini ya
Mkurugenzi wake Willson Kabwe, imeingia katika kashfa baada ya kulipwa
Sh1.6 bilioni na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa lengo wa
kununua viwanja 692 katika eneo la Bugarika na Kiseke, lakini
haikufanya hivyo.
Kashfa hiyo iliibuliwa juzi wakati Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Kashfa hiyo iliibuliwa juzi wakati Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo iliwakutanisha maofisa wa NSSF na
uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo
hilo lililodumu kwa miaka mitano.
Akitoa maelezo kwa wabunge hao, Kaimu Mkurungenzi
wa NSSF, Ludovick Mroso, alisema mfuko wake uliingia mkataba na
halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Kabwe na kwamba hiyo ilikuwa
mwaka 2008.
Alisema mkataba huo ulikuwa ni kwa ajili ya
kununua jumla ya viwanja 692 ili kujenga nyumba za kuuza, lakini licha
ya kuwalipa, bado hawajatoa viwanja kwa NSSF.
Kwa mujibu wa nyaraka za makubaliano baina ya NSSF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza wa Agosti 18, 2008, NSSF iliingia mkataba wa jumla ya Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kupewa viwanja.
Kwa mujibu wa nyaraka za makubaliano baina ya NSSF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza wa Agosti 18, 2008, NSSF iliingia mkataba wa jumla ya Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kupewa viwanja.
Katika mkataba huo uliosainiwa na Kabwe na
mwanasheria wa Jiji John Wanga (wakati huo), utaratibu wa malipo ulikuwa
ni katika awamu tatu.
Awamu ya kwanza ilihusisha fedha Sh943 milioni sawa na asilimia 50 mara baada ya mkataba kusainiwa zikiwa ni kwa ajili ya kulipa fidia.
Awamu ya kwanza ilihusisha fedha Sh943 milioni sawa na asilimia 50 mara baada ya mkataba kusainiwa zikiwa ni kwa ajili ya kulipa fidia.
Awamu ya pili ya malipo ilikuwa ni Sh755 milioni
sawa na asilimia 30 zikiwa ni fedha zilizopaswa kulipwa baada ya ujenzi
wa barabara katika viwanja na malipo ya awamu ya tatu na ya mwisho
ilikuwa ni asilimia 20.
Kwa upande wa NSSF waliweza kukamilisha asilimia
80 ya malipo kwa awamu ya kwanza na ya pili kwa kulipia jumla ya Sh1.6
bilioni hadi kufikia Juni 2011, lakini Halamshauri ya Jiji hakuweza
kuwakabidhi viwanja hadi jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji alidai kuwa mpango huo wa
viwanja 300 vya NSSF huko Bugarika ulikwama kutokana na eneo hilo
kuibuka vurugu baada ya wananchi wamiliki wa mashamba kuhamasishwa na
Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema) kuanza vurugu. Nkamia
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho alisema
maelezo ya Jiji yamekataliwa na wabunge na kwamba sababu za kudai
walikwamishwa na mbunge wa Chadema ni za uzushi na kuwaomba kuandaa
maelezo zaidi ili wawasilishe katika kikao maalumu mjini Dodoma mbele ya
waziri wao.
“Hapa tumebaini kuna uhuni mwingi sana. Tumekataa upuuzi huu, Jiji walilipwa fedha ili kutoa viwanja kwa NSSF lakini viwanja hivi wameviuza kwa watu wengine huku wakidai kisa ni Mbunge.
Sasa tumewaita mjini Dodoma mwezi ujao wakati wa
vikao vyetu vya Bunge ili waje waeleze mbele ya waziri wao,” alieleza
Nkamia na kubainisha hata hivyo alisikitishwa na kukosekana kwa
mkurugenzi mwenyewe.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1670262/-/xl8quy/-/index.html
No comments:
Post a Comment