Search This Blog

Monday, January 28, 2013

Msanii Lulu (Elizabeth Michael) aachiwa kwa dhamana


Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maaarufu kwa jina la Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba.

Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.

Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.


Lulu ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani kila siku ya kesi yake ikiwa ni pamoja na wadhamini wake kuweka bondi ya Shilingi mil 20.

No comments:

Post a Comment