Waziri wa Ujenzi John Magufuli wakiagana na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga |
Raila Odinga akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na mwenyeji wake Magufuli. |
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Kenya Raila Odinga amerejea Jijini Nairobi Nchini Kenya baada
ya kuwepo nchini Tanzania kwa mapumziko ya siku saba.
Odinga alitumia muda wa mapumziko yake hapa nchini kutembelea
maeneo mbali mbali ya kihistoria, mbuga za wanayama na visiwa vya
Zanzibar ambako alisherehekea mwaka mpya.
Katika ziara hiyo binafsi, Raila Odinga aliambatana na Mkewe
Mama Ida Odinga pamoja na wanafamilia wa karibu. Wakati akiondoka katika
uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, na alielezea kufurahishwa kwake na namna alivyoweza kupokewa na
kupata muda mzuri wa mapumziko na kwamba sasa yuko imara kabisa
kuendelea na majukumu yake ya kisiasa.
Chanzo: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/378302-raila-odinga-arejea-kenya-baada-ya-mapumziko-mafupi-nchini-tanzania-pichani-akiwa-na-magufuli.html
‘Nimepumzika vizuri na kusherehekea vyema mwaka mpya wa 2013 katika
visiwa vya Zanzibar, ninawashukuru wote walioshirikiana na familia yangu
na ninawatakia Heri ya Mwaka Mpya’ alimalizia Waziri Mkuu huyo wakati
akiagana na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
aliyekuwepo uwanja wa ndege kumsindikiza.
No comments:
Post a Comment