ASKARI Polisi wawili wa kituo Kidogo cha Polisi Benacco
wilayani Ngara mkoani Kagera wameuawa na wananchi baada ya kushambuliwa kwa silaha
za jadi huku gari walilokuwa nalo likichomwa moto katika kijiji cha Rugu Chanyamisa
wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Said Mwema |
Alisema baada ya askari hao kuanza kuondoka kurudi benacco wakiwa na Meno ya tembo kufika eneo hilo walikuta njia ikiwa imefungwa kwa mawe na huku kukiwa na kundi kubwa la wananchi wenye siraha za asili na ndipo askari hao waliouawa walipojitokeza na kujitambulisha kwa wananchi lakini walishambuliwa na kuuawa hapo hapo.
Hili ni tukio la pili askari kuuawa na wananchi ambapo
katika tukio la kwanza lililotokea Desemba 15 mwaka jana askari wengine wawili Koplo Pascal na Konstebo Alex wa Kikosi cha Usalama
Barabarani wilayani Ngara waliauawa kwa kushambuliwa na wananchi wakati ambapo
walikuwa wamekwenda katika kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki
mbovu na zisizokuwa na usajili.
Baada ya kupata habari hizo askari hao waliondoka watatu
wakiwa na wafanyabishara hao wawili ambao walipokaribia wilayani Karagwe
walitangulizwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ili kuzungumza naye wakijifanya
wakitaka kununua meno hayo na baada ya kuonyeshwa waliwapigia simu polisi na
kuja kukamatwa.
No comments:
Post a Comment