Mkurugenzi Usalama wa Taifa |
AFISA
Usalama wa Taifa mstaafu wa mkoani Mbeya Joseph Mwasokwa (76) amekufa
baada ya kuchinjwa nje ya nyumba yake eneo la Block T , Mbeya mjini.
Tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia siku ya Uhuru wa Tanganyika, Disemba 9, 2012, baada ya mwili
wake kugundulika saa 12.45 Asubuhi.
Akisimulia mkasa huo, mtoto wa kiume wa marehemu Mwasokwa, Mpoki Mwasokwa (37), amesema kuwa Baba yake aliondoka nyumbani siku ya Jumamosi Desemba 8, mwaka huu kwenda kuangalia mpira ligi ya Uingereza.
Akisimulia mkasa huo, mtoto wa kiume wa marehemu Mwasokwa, Mpoki Mwasokwa (37), amesema kuwa Baba yake aliondoka nyumbani siku ya Jumamosi Desemba 8, mwaka huu kwenda kuangalia mpira ligi ya Uingereza.
Alisema alipokuwa akiondoka
alimuaga na kumsihi kuwa asiondoke na gari bali aliingize ndani
kwasababu hakukuwa na mafuta ya kutosha.
“Baada ya hapo hatukumuona mpaka nilipokuja kuambiwa na mama kuwa kulikuwa na mtu ameuawa nje ya geti letu,’’ alisema Mpoki.
Aliendelea kusimulia kuwa Mama
yake alimpa taarifa kuwa kuna binti alienda nyumbani hapo kwa ajili ya
kununua mahitaji ya nyumbani katika kiosk kilichopo nyumbani hapo na
kuukuta mwili wa marehemu nje na kutoa taarifa kwa mama yake.
“Mama alienda katika chumba
anacholala Baba hakumkuta ndipo akaja na kuniambia kuwa kuna mtu ameuawa
nje ya nyumba yetu na tulipotoka nilipojaribu kuugeuza mwili ule kwa
mguu nikagundua kuwa ni Baba ambapo mwili wake ulikuwa na majeraha ya
kukatwa katwa,’’ alisema mtoto huyo wa marehemu.
Ametanabaisha kuwa alimkuta baba
yake yupo kifudifudi huku mwili wake na ardhini kukiwa kumetapakaa damu
na wakachukua hatua ya kuwapigia Polisi na Polisi walipofika na kumpekua
waliukuta mwili huo ukiwa na pesa Dola za kimarekani 200 na Shilingi za
Kitanzania 110,000/= na simu ya kiganjani.
Alisema mwili wa marehemu
utasafirishwa siku ya Jumanne Disemba 11, mwaka huu kwenda wilayani
Kyela mkoani hapa kwa ajili ya mazishi. Marehemu ameacha mjane na watoto
saba.
Habari hii imeandikwa na mwandishi wa FikraPevu, Mbeya
No comments:
Post a Comment