Bendera ya Tanganyika Huru |
Leo tunaadhimisha miaka 51 tangu Tanganyika ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni. Huu ni umri wa kutosha kama Taifa na haina shaka sisi siyo taifa changa tena. Lakini tunaposheherekea umri huu wa Taifa hebu tutafakari mambo kadhaa kuona kama umri wa taifa letu unaendana na hali halisi ya maendeleo yake.
1. Hali ya uchumi: Inaonekana kuwa uchumi wetu unakua kwa kasi ya kuridhisha lakini pia umaskini uliokithiri umeongezeka kwa zaidi ya 50%. ( Haya nimeyasikia leo kwenye uchambuzi wa profesa G. Mpangala TBC taifa asubuhi ya leo).Hii nadhani inatokana na ubinafsi wa watawala wetu pamoja na ufisadi na ubadhirifu wa mali ya uma. Wewe unaelezeaje hali ya uchumi ya nchi yetu katika umri huu wa miaka 51?
2 . ELIMU. Kwa maoni yangu elimu yetu imeporomoka kwa kiasi kikubwa kulinganisha na miaka ya sitini/sabini. Wewe unasemaje?
3. Michezo Sijaona nia ya dhati kuendeleza sekta ya michezo, Wewe una maoni gani??!Una weza kutoa tathmini gani ya miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika!!?? Karibu tusheherekee pamoja huku tukijadili Tanganyika at 51.
No comments:
Post a Comment