Search This Blog

Saturday, December 29, 2012

KITENDAWILI CHA KUJERUHIWA KWA PADRI ZANZIBAR

Written by ZanzibarTweets // 29/12/2012 // Makala/Tahariri // No comments
Padri Mkenda akizungumza na Rais Kikwete
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefika njia panda kutokana na matukio mabaya na ya ghafla yanayotokea hapa Zanzibar, hasa yanayobeba sura ya ‘hit and run attacks’ ambayo pia yanaingia katika sura ya visasi (revenge) — kuanzia lile la Soraga hadi la huyu Padri.

Kuna nadharia nyingi hapa zinazohusu uhalifu (theories on criminology) — au hata conspiracy theory.

Nadharia 1: hujuma inafanyika lakini hakuna clue/au hata alama ya namna uhalifu ulivyofanyika — hapa inakluwa taabu kwa wapelelezi kugundua namna ya ualifu huo ulivyofanyika, au vipi umefanyika, na hata kuanzia pa kufanya upelelezi.

Nadharia ya 2: Uhalifu umefanyika, aliyefanyiwa uhalifu yuko hai, na kauli thabit anaweza kusema. Hapa inakuwa rahisi sana sana kwa makachero kujua na kuanza upelekezi wa kina. Kesi zote mbili zilizotokea Zanzibar (Soraga na Padri zinaingia hapa).

Wote wazima na wote wana kauli thabit. Padri ameweza kuzungumza na kuweza kuidhalilisha POLISI kama taasisi pale alipotoa kauli yake kumpinga RPC Aziz.

Kauli ya Padri dhidi ya jeshi la polisi inaonyesha dhahir kuwa kanisa linataka watendewe vile wanavyotaka wao; na sio hali halisi ilivyo. Ingawa hakusema wazi wazi, lakini indirectly, ana maana ya kusema kuwa ‘polisi ni muongo, au waongo’. Hii ni idhalali kubwa kwa jeshi la polisi.

Kw auhakika ni kuwa padri huyu alikuwa anashika pesa, whether awe mhasibu by professional or not. Kwa uhakika 100% padri huyu ndiye signatory wao.

Bila yeye haitoki pesa. Je, na hili atalipinga. Naomba hao makachero wa kutajika kutoka Dar, waanzie hapa kama ndio ‘lead’ yao. Tumelewwana? Muanzie hapa. Je, haiwi kuwa ‘internal job’.

Angalia sequence za kihalifu zilizofanyika TZ karibuni:
i. Afisa wa kuzuia rushwa apigwa na kuuliwa na mwenzake Dar
ii. RPC Mwanza apigwa risasi na kuuliwa Mwanza.
iii. Pesa nyingi zimeibiwa duka la Dar (150m) — kitendawili mpaka leo???? Au kwa sababu hili limetokea Zanzibar. Achane kuwa bias!
iv. Kuna mauwaji mengi yametokea Dar during chrismas time, mzungu mmoja amenyongwa hotelini, na wengine kuuwawa kikatili …kimya! kimya!

Nadharia 3: Nadhani kanisa, CCM TZ na serikali zote zitafurahi sana kama report ya makachero hayo zitasema kuwa UAMSHO ndio waliofanya kosa hilo. Mimi naomba kuwasaidia kitu.

Mpaka sasa, ukweli ni kuwa, waislamu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hawajafikia level hiyo ya kutumia silaha au kuhujumu. Hili linajulikana na liko wazi. Kisocholojia, bora hata siasa Zanzibar zinaweza kuwa ni ‘problem’ kuliko hata dini.

Mimi naomba serikali ya JK, Shein na IGP Said Mwema muwe waangalifu sana na trend hii inayojitokeza. Mjaribu sana kuwa fair na wakweli – otherwise, mnaimaliza nchi hivi mnajiona. Your careless minds — JK, Shein, Mwema and others — inaweza kuleta bad feelings kwa waislamu ambayo wanaamini kuwa Zanzibar ni nchi yao na nchi ya kiislamu. Hivi JK kuoni fakhari kuwa hivyo, yaani Zanzibar ndio kama kigezo kwa dunia v.s Tanzania.

Kumbuka kuwa mnapewa pesa za bure na nchi za kiislamu kupeleka hajj waislamu (ni kupitia mgongo wa Uislamu wa Zanzibar, na sio Tabora au Singida n.k); then mnachagua wakereketwa kwenda huko Hajj na kuacha waumin wa kweli.

Chokochoko hizi za dini, na hasa ukiristo — hautoijenga TZ, ila itaivunja vunja viapande vipande – angalia secratian war — Northern Ireland, former Yugoslavia [Kosovo, Serbia n.] Iraq n.k.

Shein na JK mnakaa na kubabaishwa na washauri wenu; na hamtaki kutumia akili zenu mlizojaaliwa hata 0.01%. Hebu tafuteni ukweli wa mambo. Huu ndi ushauri w abure kutoka kwangu.

* Na balozi Seif Ali Iddi acha kuwa bias. Mbona hujaenda kumuona Fadhil Soraga mpaka leo? umeamua kwenda wewe na Mohammed Aboud kumuona Padri na aila yake na wafuasi wake.

* Naomba tena hao makachero waliokuja Zanzibar waanzie pale benki anapokwenda kuchukua ‘hela’ padri huyu ambaye pia ndiye signatory mkuu, benki xxxx! nendeni hapo mkaone transaction alizokuwa anazifanya padri huyo, na kama kuna bank reconciliation zinazokubalika — au shaghla baghala tu.

* Na kama je, hali ya makusanyo na matumizi ya kanisa hili yanaridhia financial regulations za Tanzania, Zanzibar na bank of Tanzania. Check …kama kuna a kind of money laundry hapo?

Kwa ufupi matukio haya bado yamebaki kuwa kitendawili (unresolved mystery).

Like · ·Follow postUnfollow post · 19 minutes ago via Mobile.Write a comment....

No comments:

Post a Comment