Search This Blog

Monday, December 10, 2012

JK atunuku nishani 40 akiwemo na msanii Bi Kidude

Rais Kikwete akimtunuku Nishani Bi. Kidude
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete jana Ikulu ametunuku  nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali ya jamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.

Miongoni wa waliotunukiwa nishani hizo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi.Kidude).
 

Msanii Bi. kidude enzi za Ujana wake.
Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari Jeshi na Polisi. 

Kutunukiwa nishani kwa Bi. Kidude kulikuwa burudani ya iana yake hasa ikizingatiwa umri wake ambao mpaka sasa unakadiriwa kuwa kati 80 hadi 99 pamoja na manjonjo yake.

No comments:

Post a Comment