Pichani juu askari
wakikagua mwili wa Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa
Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL
mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi na kufa papo hapo.
Kwa mujibu wa baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki
dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na
mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa nguvu na kupigwa risasi na
kufariki dunia.
Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa
Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na
watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kujua chanzo cha mauaji yake.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.
No comments:
Post a Comment