Hafla ya kukabidhiwa magari hayo ilifanyika jana ambapo ilielezwa kwamba magari yote yatagharimu dola 36.56 za Marekani .
Akipokea magari hayo jana Dar es Salaam, Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema magari
hayo yametolewa kwa mkopo uliosainiwa Januari 26, 2012 kati ya Tanzania
na India kupitia Benki ya Exim.
Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani kikicheza ngoma na Msewe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari hayo |
“Mpaka sasa tumeshapokea magari 592 na makontena
16 yenye vifaa vya akiba. Magari 88 yaliyobaki tunatarajia kuyapokea
Septemba 2013,” alisema Nahodha.
Alisema Serikali ya India imetoa magari manne kama
zawadi kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya jeshini na kwa wananchi
wa kawaida.”
Nahodha alisema magari hayo yamefika katika wakati
mwafaka kwa kuwa yatasaidia kupunguza tatizo la usafiri na kwamba
hayatatumika katika shughuli za ndani za kijeshi pekee bali yanatarajiwa
kutumika kusomba mahindi katika mikoa mbalimbali nchini.
Alisema mkataba kati ya Tanzania na India
ulifikiwa kutokana na uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili
ambao ulianza tangu miaka ya 1950 chini ya Mwalimu Julius Nyerere na
Rais Jawaharlal Nehru.
Nay Balozi wa India nchini, Debnath Shaw alisema
magari hayo ambayo yametengenezwa na Kampuni ya Ashok Leyland ya India,
baadhi yao yatatumika kulinda amani katika nchi ya Democratic Republic
of Congo (DRC).
“Magari haya yametengenezwa kustahimili hali ya nchi zinazoendelea…tunatarajia yatatumika kulinda amani DRC,” alisema Shaw.
Akizungumzia ulijo wa magari hayo, Mkuu wa majeshi
ya ulinzi nchini, Meja Jenerali Davis Mwamunyange alisema kati ya
magari yaliyopokelewa yapo maalumu kwa ajili ya shughuli za kijeshi.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/India-yakopesha-Tanzania-magari-675-ya-Jeshi/-/1597568/1940880/-/9htc9z/-/index.html
Source: http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/India-yakopesha-Tanzania-magari-675-ya-Jeshi/-/1597568/1940880/-/9htc9z/-/index.html
No comments:
Post a Comment