Maji ya Tindikali (Acid) |
Polisi katika kisiwa cha
Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid
katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume
wawili waliwatendea wanawake hao kitendo hicho walipokuwa wakitembea
katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi yao wanaume hao.
Wanawake hao, wanasemkana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi halo haijulikani.
No comments:
Post a Comment