Search This Blog

Tuesday, November 6, 2012

Breaking News: Mhashamu Askofu Alosius Balina afariki dunia



MHASHAMU Askofu mkuu wa Jimbo la Shinyanga Kanisa katoliki amefariki dunia akiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa akitibiwa.
  
Historia yake:
Mhashamu Askofu Aloysius Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika kijiji cha Isoso Ntuzu wilayani Bariadi  mkoani Shinyanga na aliwekwa wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka 1984 kuwa Askofu wa Geita na kusimikwa Machi 10, 1985.
Septemba 23, 1997 alihamishiwa Jimbo la Shinyanga na kuwa Akofu wa tatu wa Jimbo la Shinyanga hadi mauti yalipomkuta, huku watangulizi wake wakiwa Askofu Edward A. McGurkin, aliyetumikia cheo hicho toka mwaka 1956 hadi 1975, alifariki Agost 281983 huko Marekani, wa pili ni Askofu Castor Sekwa, aliyetumikiwa kuaznia mwaka 1975  hadi  Juzi 6, 1996 alippofariki na askofu Balina kushika nafasi yake.

Taarifa kamili zitatolewa baadaye

No comments:

Post a Comment