January Makamba afanya majaribio mfumo wa kuripoti Rushwa
Muda mfupi baada ya kukaririwa na gazeti la the Guardian la nchini
Uingereza akiahidi kuanzisha mfumo utakaosaidia wananchi wa Tanzania
kuripoti rushwa kwa njia ya simu na mtandao wa internet, jana Makamba
amefanya majaribio ya mfumo huo mbele ya wataalam mbalimbali wa social
media.
Akitambulisha mfumo huo kwa wadau, January Makamba alisema
"Ni asilimia 6.9% ya vitendo vyote vya rushwa nchini ndio vinavyo
ripotiwa kwa vyombo husika. Kwahiyo zaidi ya 93% ya matukio ya rushwa
hayafikishwi polisi au TAKUKURU. Kutokuwa na ufahamu ya wapi rushwa
inatendeka na saa ngapi, ni kizingiti kikubwa katika vita dhidi ya
rushwa. Ni matumaini yangu kwamba mRushwa itatoa taarifa kuhusu rushwa
ilivyo nchini ili tuweze kuitokomeza".
No comments:
Post a Comment