Nilisikitika baada ya kuona taarifa kuhusu kuondolewa kwa picha ya
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mmoja wa waasisi wa Umoja wa Afrika (OAU).
Kwenye Bango hili lenye Picha za viongozi waasisi ya Nyerere hakuna. |
Mwalimu Nyerere,
mmoja wa watetezi na wakubwa Afrika aliyetoa nchi yake Tanzania
kusaidia ukombozi wa Afrika, hivi tunaweza kumuweka kanda katika
orodha ya waasisi wa OAU?.
Hivi tumefikia wapi au Serikali
imeamua kukubaliana na kupuuzwa kwa historia muhimu ya Umoja huo? Kwangu
mimi, kutokuwepo kwa picha ya Mwalimu ni ishara ya kupuuzwa kwa kiwango
cha juu mchango wake binafsi, tena wa moyo kabisa, kwa bara letu na pia
ni kupuuzwa kwa mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara
hili.
Tumepoteza watu na rasilimali nyingi za taifa kupigania haki ya
utu na heshima ya mwafrika na kujenga umoja. Nadhani umoja wa Afrika
utatukosea haki isiporejesha picha ya Mwalimu.
No comments:
Post a Comment