JESHI la polisi, limetoa taarifa ya awali ya mauaji ya
aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow (53) na kubainisha
idadi ya watuhumiwa 10 wanashikiliwa kwa mauaji hayo huku likitaja sababu mbili
za kisasi cha mapenzi na ujambazi ndiyo zinaweza kuwa chanzo.
Taarifa hiyo ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa mauaji imetolewa na
Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba mbele ya Mkuu
wa Jeshi la Polisi, Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Said Mwema na makamanda
mbalimbali wa jeshi hili kutoka wilaya na vituo mbalimbali mkoani Mwanza.
Taarifa hiyo imetolewa jana jioni muda mfupi baada ya IGP
Mwema kumaliza vikao viwili kimoja kikiwa ni Kamati ya Ulinzi na Usalama cha
Mkoa kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, na
baadaye kikao cha maofisa wa polisi ambavyo vyote waandishi wa habari
hawakuudhuria.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza,
Evarist Ndikilo akizungumza na Mwananchi alieleza kwamba jeshi hilo lilitoa
taarifa hiyo katika kikao hicho awali na kwamba baada ya kuridhika nayo ndipo
alikwenda kuzungumza na maofisa wake na kutoa kwa vyombo vya habari.
Uchunguzi ulivyoendeshwa:
Akizungumzia namna ambavyo jeshi hilo liliendesha uchunguzi
huo, DCI Manumba alisema kuwa walipofika Mwanza yeye na kikosi chake
kilichojulikana kama Kikosi kazi cha Upelelezi walilazimika kujigawa katika
vikosi vitatu ambavyo ni Kikosi cha Ukamataji, Kikosi cha Mahojiano na kingine
cha ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za Interejensia huku wakitumia njia za
kisanyansi katika ufuatiliaji mitandao ya simu.
Alisema kuwa kikosi kazi cha ufuatiliaji kilijikita katika
ufuatiliaji katika mikoa yote ya kanda ya ziwa ikiwemo Dar es Saalam kutoka na
taarifa walizokuwa zikichambuliwa kinterejensia na kutoa majukumu kwa kikosi
cha ukamataji na waliokamatwa walikabidhiwa kikosi cha mahojiano.
“Wakati tunafanya hivyo tayari wenzetu walikuwa
wanamshikiria Mwalimu Doroth aliyekuwa na marehemu wakatia akiuwawa na
majambazi hao huku wakimuhoji kutokana na tarifa mbalimbali zilizokuwa
zinafaikia zikiwemo zile wivu wa mapenzi”alisema Manumba na kuongeza kuwa.
Sababu za Ujambazi:
Alisema katika ufuatiliaji wa pili baada ya kupatikana simu
ya Mwalimu Dorothy Moses aliyekuwa na marehemu kamanda huyo usiku wa tukio,
ambayo ilipatikana na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa watano jijini Dar es
salaam ambao wameonekana kuwa na rekodi ya kuhusika na mtukio kadhaa ya
Ujambazi Mwanza na Dar es salaam.
DCI Manumba akisoma ripoti ya uchunguzi kwa Waandishi wa Habari |
“Watu hawa ni majambazi, na kabla ya kumuua kamanda Mwanza
inaonekana walihusika na matuko kadhaa ya ujambazi, na hata baada ya kukimbilia
dar nako walihusika na matukio kadhaa na kufanikiwa kukamatwa ambapo wamekiri
kuhusika na kutuwezesha kukamata siraha aina ya Shotgun pamoja na silaha
nyingine aina ya Pumpaction,” alieleza DCI Manumba.
Aliwataja waliokamatwa katika tukio la Dar es salaam kuwa ni
Muganyizi Marko Petro (36), Chacha Mwita (50), Magige Mwarwa(35), Edward Masota
(33) pamoja na Bhoke Mwita (54) ambao wote wamekamatiwa jijini Dar es Saalm.
Kutokana na rekodi ya ujambazi na mmoja wao kubainika kuwa
alitoka jela miezi minne kabla ya tukio hilo jeshi la polisi kwa watuhumiwa
hawa limedai sababu inaweza kuwa ni tukio la ujambazi.
Sababu za kisasi cha Mapenzi:
Hata hivyo akielezea wakati wa maswali kwa waandishi wa
habari, IGP Mwema alisema Waliokamatwa Dar ni watuhumiwa watano, lakini wapo
watuhumiwa wengine wa Mwanza ambao ni pamoja na Dorothy Moses na mpenzi wake
Feliex Felician na nduguye Fumo Felician pamoja na wengine wawili bado wanashikiliwa
na jeshi hilo kutokana na dhana ya awali ya kisasi cha mapenzi ambao
hawaajaachiwa.
Kwa sasa hatuwezi kueleza iwapo sababu ya mauaji ni nini
hasa bado tunaendelea na kuunganisha sababu za makundi haya mawili na kile
walichosema ili kupata sababu moja ya mauaji yao na pindi tutakapokamilisha
tutaitangaza.
Wengine watatufwa:
Aidha IGP Mwema na DCI Manumba walieleza kuwa katika itadi
hiyo ya watuhumiwa 10 bado jeshi lake linaendelea kuwasaka watu wengine wawili
ambao wametajwa kuhusika na tukio hilo na kundi la watuhumiwa waliokamatwa Dar
es salaam.
IGP Mwema alisema kuwa tukio la mauwaji ya kamanda Barlow
halijawavuja moyo na badala yake wamejifunza na kuongeza ulinzi zaidi ili
kuzuia matukio kama hayo yasitokee tena.
Alisema kuwa Jeshi la Polis linajipanga kuwapatia mafunzo
askali wake ili kuhakikisha analinda hali ya usalama wa Taifa hili.
“Hata hivyo tumeweza kufanya kazi nzuri katika kipindi hiki
kwa kuhakikisha mkoa wa Mwanza unakuwa na amani na utulivu baada ya kifo cha
kamanda Barlow”alisema IGP Mwema.
Aliendelea kwa kusema kuwa Jeshi la Polisi halitasita
kumchukulia hatua mtu yeyote ambayo atakuwa
nataka kuvuja amania ya nchi hii iwe uchambazi au uchochozi.
Aliwaasa wananchi kuwa na siri binafsi,ya umma na yakijamii
ili kujikinga na kuharibu amani ya Taifa hilo ambayo imekuwepo kwa muda
mrefu.
Kamanda Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu majira ya saa 8
usiku wakati akitoka kwenye kikao cha maandalizi ya arusi ya mtoto wa dada yake
Sembuli Moleto kilichofanyika Hotel Florida wakati akimsindikiza mwalimu wa
shule ya Msingi Nyamagana B, Dorothy Moses eneo la Minazi mitatu Kitangiri.
No comments:
Post a Comment