Msanii nyota wa vichekesho na uimbaji Sharomillionea (Ramadhan Hussein) amekufa kwenye
ajali iliyotokea huko Tanga. Kijana nyota yake ilikua inaanza kung'ara
na kupata dili za matangazo akiwa na Mzee Majuto.
Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo
majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja
alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa
anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam
kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari
lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake,
mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya
Muheza”
Kamanda amesema
hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata
ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari
imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
No comments:
Post a Comment