Search This Blog

Friday, November 30, 2012

Breaking News: Mengi ashindwa kesi yake na Sarah Hermitage na kuamuliwa kumlipa Bilion 2.4

 Press Release

Date:  30 November 2012

Sarah Hermitage Libel Defence Upheld

Silverdale Farm Blog Justified

At the High Court in London today, Mr Justice Bean delivered Judgment in favour of Sarah Hermitage, who had been sued for libel by the wealthy Tanzanian businessman, Reginald Mengi, the Executive Chairman of IPP Ltd, a company which holds major newspaper and broadcasting interests in Tanzania.
Reginald Mengi sued in respect of five postings on Sarah Hermitage’s Silverdale Farm blog and two emails she had sent, which Mr Mengi claimed to be false and defamatory of him. 
During the trial, the Court heard unchallenged evidence from Sarah Hermitage and her husband, Stewart Middleton, as to how they were by threats, intimidation and corruption driven from Tanzania and forced to abandon the investment they had made in their farm, Silverdale, of which Reginald Mengi’s younger brother, Benjamin, then took possession.  The Court was told that a major factor in the ordeal they suffered was the hostile and defamatory coverage their case received from the IPP-owned English language Guardian and the Swahili Nipashe newspapers.  Reginald Mengi, in the course of his evidence, repeatedly stated that he “was not responsible, not accountable and not answerable” for the editorial content of IPP publications.
In giving Judgment, Mr Justice Bean ruled:
I find that the campaign in the Guardian and Nipashe facilitated Benjamin’s corruption of local officials and intimidation of the Middletons and thus helped Benjamin to destroy their investments and grab their properties; and that Mr [Reginald] Mengi, since he either encouraged or knowingly permitted the campaign, was in that sense complicit in Benjamin’s corruption and intimidation.  The allegation is thus substantially true, and justified at common law.
Following the handing down of the Judgment, Sarah Hermitage said today:
I set up my Silverdale Farm blog in 2009 to document our horrific experience in Tanzania, and to expose as a warning for others the corruption we encountered and our helplessness with no protection from the local Courts and officials.  As the Judge has found, my response to the campaign waged against us in IPP publications was reasonable, proportionate, relevant and without malice. To find myself then sued for libel in my own country, facing a claim of  legal costs of £300,000 from Mr Mengi before the proceedings had even started, was itself frightening and oppressive.  I am relieved that, with the support of my legal team who were prepared to risk getting paid nothing at all under a “no win, no fee” agreement, justice has in the end prevailed in this case. I also must thank the brave and honest Tanzanian journalists who either openly or privately assisted in the preparation of our defence. I will continue to use my blog, my voice, to do all I can to fight against the corruption I have seen first hand in Tanzania, not least in the hope that it may in the end help the very good people, not least our loyal staff, who have stood by us throughout.
After handing down judgment Mr Justice Bean ordered that Reginald Mengi should pay the defence costs at the higher “indemnity” rate. In reaching this decision, the factors cited by the Judge included that Counsel for Sarah Hermitage had “rightly described the litigation as “oppressive”, that “enormous costs had been thrown at the case from the beginning, indeed before the issue of proceedings” and that the evidence of the Claimant and his witnesses had in a number of respects been “misleading and untrue.”
Mr Justice Bean ordered that Reginald Mengi should pay £1.2million on account of Sarah Hermitage’s legal costs, which will be subject to detailed assessment by the court in due course.
Enquiries to Andrew Stephenson, Carter-Ruck, Tel: 020 7353 5005  
 

Thursday, November 29, 2012

MTOTO ALIYEZALIWA KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE AOMBA WASAMALIA WEMA KUMCHANGIA AKAPATIWE MATIBABU NCHINI INDIA.


 DICKSON VEDASTUS WASIWASI ALIZALIWA 7/07/1996 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA, KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE (KIKIONEKANA WAZIWAZI), MADAKTARI WAMEMFANYIA MATIBABU KUPITIA OPARESHENI MARA TATU BILA MAFANIKIO.

OPARESHENI YA KWANZA ILIFANYIWA AKIWA NA MIEZI MIWILI, OPERESHENI YA PILI IKAFUATIA NA YA TATU IKAFANYIKA MWAKA 2000 HAPO HAPO HOSPITALI YA BUGANDO, LAKINI KWA BAHATI MBAYA ZOTE HAZIKUZAA MATUNDA.


KWA MUJIBU WA MZAZI WA KIJANA DICKSON, BW. VEDASTUS WASIWASI AMBAYE NI MKAZI WA MTAA WA SONGAMBELE, MAGOMENI KIRUMBA KATIKA  JIJINI MWANZA AMESEMA KUWA ALIPEWA USHAURI NA MADAKTARI WA HOSPITALI HIYO KUMPELEKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU ZAIDI.

GHARAMA ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 20, NAYE HANA UWEZO HIVYO AMEOMBA WASAMALIA WEMA KUMSAIDIA KUNUSURU ADHA NA MATESO AYAPATAYO MTOTO WAKE.

 CHANGIA KUPITIA AKAUNTI ZIFUATAZO:-
CRDB     0152457709500
AZANIA 003003005102370001

SIMU 0762324527 OR 0683580004

 LEO tulipata fursa ya kuzungumza na mzazi wa mtoto anayehitaji upasuaji (Dickson) Bw. Vedastus Wasiwasi kujua usumbufu na adha aipatayo mtoto naye kwa ufupi alikuwa na haya ya kuongea.. Bofya play.
Source: http://gsengo.blogspot.com/2012/11/mtoto-aliyezaliwa-kibofu-cha-mkojo.html

Serikali yapiga marufuku Posho kwenye Halmashauri!

Imeandikwa tarehe 30 Novemba 2012 na Christopher Maregesi, Bunda | HabariLeo

SAKATA la posho kwa watendaji wanaolipwa mshahara baada ya kupoa kwa wabunge, limehamia katika halmashauri nchini kote baada ya Serikali kupiga marufuku posho za watumishi wa halmashauri hizo zinazotolewa wakati wakitimiza majukumu yao ndani ya vituo vya kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mathayo Kadata alitoa kauli ya kuzuia posho hizo jana mjini hapa, akiwa katika ziara yake ambapo pia alikutana na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Alifafanua, kuwa malipo ya posho yanapaswa kutolewa kwa mtumishi aliyetumwa kikazi nje ya kituo chake cha kazi na si vinginevyo na kumtaka kila mtumishi wa halmashauri nchini kuzingatia hilo ili kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali.

Kadata alionya watumishi wa halmashauri nchini wenye tabia ya kuomba wakurugenzi wao posho kila mara hata wawapo ofisini mwao na kuongeza kuwa kudai posho ni sawa na kuiibia Serikali.

Mbali na kuonya watumishi hao, Kadata pia alionya wakurugenzi wa halmashauri kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na ikibidi kuwaondoa kazini mara moja, wakibainika kulipa posho watumishi wao kwa mambo yaliyo ndani ya majukumu yao ya kila siku.

Alisema watendaji hao wanapaswa kutambua, kuwa wameajiriwa kwa lengo la kutumikia Watanzania wanaowalipa mishahara kupitia kodi wanazotoa.

Alitaka watumishi watumikie wananchi maana wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi kutokana na walichokifanya kwa mwezi na kusisitiza, kwamba kudai posho ni wizi.

“Wananchi hawa wanaelewa sana. Hatuwezi kuwafanya wajinga siku zote. Tunawazidi utaalamu tu lakini si kingine; hivyo tunapaswa tuwatumikie kwa ubunifu na uadilifu wenye uzalendo mwingi ndani yake,” alisema Kadata.

Aliongeza kuwa Watanzania wanatarajia kuona mabadiliko ya maisha yao yatokanayo na ubunifu, uadilifu, uwajibikaji na uzalendo wa watumishi wao.

Sakata la posho limekuwa likiibuka mara kwa mara katika ngazi ya wanasiasa na hasa wabunge ambapo wananchi na wadau wamekuwa wakihoji mantiki ya posho kwa mtu anayelipwa mshahara.

Serikali: Rada ya Chenge imechoka; Usalama wa anga sasa upo shakani!

*Waziri ashangaa, ashauri inunuliwe nyingine 

*TCAA yasema moja haitoshi, zinahitajika tano


HATIMAYE Serikali imekiri kuwa rada inayotumika kwa ajili ya kulinda usalama wa anga nchini, imechoka. Kutokana na hali hiyo, usalama wa anga la Tanzania upo shakani, kutokana na ubovu wa rada hiyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya usalama wa anga.


Taarifa hizo za majonzi kwa Serikali, zilielezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba alipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Tizeba, alisisitiza umuhimu wa Serikali kununua rada nyingine haraka iwezekanavyo, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na ubovu huo.

Dk. Tizeba alikiri kuwa amepata maelezo juu ya utendaji kazi wa rada hiyo, yanayotia wasiwasi kuhusu usalama wa anga hasa kwa usafiri wa ndege.

Kutokana na hali hiyo, ameitaka mamlaka husika kuwasilisha maombi mapema ofisini kwake, ili jambo hilo liweze kuingizwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014.

“Ni kweli rada yetu imechoka….kwa hili tusiweke mzaha kuna umuhimu wa kununua rada nyingine haraka iwezekanavyo, tukiendelea na mtindo wa kulilea tatizo hili siku moja litatuaibisha jamani,” alisema Tizeba.

Mapema Agosti, mwaka huu rada hiyo ilishindwa kufanya kazi baada ya kuharibika kifaa (Power Supply Unit) ambacho kiliigharimu Serikali Sh milioni 40.

Rada hiyo, ilinunuliwa kutoka Kampuni ya BAE System ya Uingereza kwa Sh bilioni 40 na hivyo kuibua mjadala mkubwa, baada ya kubainika bei hiyo, ni kubwa kinyume na bei halisi.

Rada hiyo, ilinunuliwa kwa ushauri wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, Andrew Chenge ambaye sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM).

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TCAA, Fadhili Manongi alisema mamlaka yake inafanyakazi katika wakati mgumu, kutokana na rada hiyo kusuasua.

Hata hivyo, Manongi alisema kulingana na ukubwa wa anga la Tanzania rada moja haitoshi na kusema Tanzania inapaswa kuwa na rada zisizopungua tano, ili kuongeza ufanisi wa usalama wa anga.

“Anga la Tanzania ni kubwa ikilinganishwa na maanga ya nchi nyingine za Afrika Mashariki, wenzetu Kenya wanatumia rada tano.

“Wanatumia rada tano kwa hivi sasa, licha ya anga yao kuwa ndogo kuliko ya kwetu, iweje sisi tuendelee kutumia rada moja tena iliyochoka na ukiangalia bei ya rada kwa sasa imeshuka kwa kiasi kikubwa,” alisema Manongi.

Alisema mamlaka yake inalazimika pia kufanya kazi katika anga ya Rwanda na Burundi na inatarajia kutumia Sh milioni 102, kwa ajili ya kutengeneza kituo kipya eneo la Kasulu, ili kuongeza ufanisi.

Taarifa hiyo ilimshitua naibu waziri, ambaye alihoji kama huduma za TCAA nchini Rwanda na Burundi zinalipiwa.

“Inakuwaje mnahudumia mataifa hayo, mnafaidika nini…kama hawawalipi inabidi wachangie gharama za kituo cha Kasulu…sababu mambo ya kubeba majukumu ya taifa lingine ni ya kizamani na tukiendelea hivi wanatudharau,” alisema Dk. Tizeba.

Mkurugenzi wa TCAA alikiri mamlaka yake hailipwi chochote na nchi hizo na wanafanya hivyo kwa kufuata agizo la Mamlaka ya Kimataifa ya Usalama wa Anga, (ICAO).

“Kwa kuwa nchi hizi zina eneo dogo la anga, kwa kuanzia umbali wa mita 24,500, inabidi tuwahudumie na hii inatokana na agizo la Mamlaka ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO),” alisema Manongi.

Chanzo: Mtanzania | Nov 30, 2012

Hatutoi sasa majina ya walioficha fedha Uswiss

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha ya vigogo walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina hayo kama Serikali inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi ambayo ilitajwa Mwembe Yanga bado haijashughulikiwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara jijini Mwanza, Mnyika alisema kwamba kama Serikali ya CCM inasisitiza kutaka majina ya walioficha fedha huko Uswiss yatajwe, wanapaswa kusimama na kueleza ile orodha ya mafisadi ambayo Chadema waliitaja pale Mwembe Yanga imefanyiwa kazi gani.

“Watu wanapotutaka tutaje majina, na sisi tunawambia kwanza wasimame na kutueleza ile ‘list’ (orodha) ya mafisadi ambayo tuliitaja kwa majina wameishughulikia vipi?” alihoji Mnyika na kuongeza kwamba wanajua jinsi ambavyo CCM wanalivyonufaika na ufisadi kupitia Kampuni ya Kagoda jambo ambalo linadhihirisha kuwa haiwezi kuwa rahisi kwao kushughulika na vita ya ufisadi.

Alisisitiza kuwa wanaotaka majina yatajwe wanayo ajenda yao na wao wameshaifahamu hivyo hawatashughulika nayo na kusema ukifika wakati ambao wao wanautambua wataweka kila kitu nje, lakini siyo kwa kushinikizwa na Serikali ya CCM.

“Tunajua serikali hii inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi haina dhamira ya kushughulika na ufisadi, na hili ndilo litakalowaondoa madarakani,” alifafanua.

Hata hivyo mkutano huo uliingia dosari wakati Mnyika akiendelea kuhutubia ambapo mawe yalianza kurushwa na vijana wanaodaiwa kuwa ni vijana wa Diwani wa Kata ya Kitangiri kwa tiketi ya Chadema, Henry Matata aliyevuliwa uanachama.

Kutokana hali hiyo vijana wa Chadema walizungumza katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa vijana wawili ambao walishambuliwa na kueleza na kunusuriwa na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje aliyeita polisi na kuwaomba waache kuwashambulia.

Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Wenje alieleza wananchi kuwa katika mkakati wake wa kuboresha elimu ya msingi na sekondari amefanikiwa kutengeneza madawati mengine 400 baada ya madawati ya awali 500 kugawiwa katika shule.

Alisema madawati hayo yatagawanywa kwa shule 30 za wilaya ya Nyamagana na kubainisha kwamba kutokana na madaati ya awali 500 kutolewa bila utaratibu na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,Wilson Kabwe hivyo madawati haya alieleza kuwa yatasambazwa na madiwani wa Chadema katika shule pamoja na katibu wa ofisi yake ili kuhakikisha yanafika katika shule husika iliyopangwa.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1632500/-/vib3dv/-/index.html

Jaji chande aikwepa kesi ya Lema

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amejitoa kusikiliza rufaa ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, badala yake nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.
Kujitoa kwa jaji mkuu kumekuja ikiwa zimebaki siku tano kusikilizwa upya kwa rufaa hiyo Desemba 4, mwaka huu, baada ya awali Mahakama ya Rufani, kuona rufaa hiyo ilikuwa na dosari.
Jaji Mkuu Chande Othman
Mahakama hiyo ilikubali hoja ya wajiburufaa kuwa rufaa hiyo ilikuwa na dosari kutokana na tofauti ya vifungu vya sheria vilivyotumika katika hukumu iliyomvua ubunge Lema na vilivyotumika katika hati ya kukaza hukumu, iliyowasilishwa mahakamani sambamba na rufaa hiyo.
Hata hivyo, kilichomwokoa Lema ni kifungu cha 111 cha Kanuni za Mahakama, ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa chini ya kanuni hiyo, dosari hizo zinaweza kurekebishwa.
Jaji Chande ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo la majaji watatu katika kesi hiyo akiwamo Salum Massati na Natalia Kimaro.
Jaji Mkuu aliingia kwenye kesi hiyo akichukua nafasi ya Jaji Mbarouk Salim Mbarouk aliyekuwa amepangwa awali, ambaye sababu za kuondolewa hazikuwekwa wazi.
Wakili wa  Lema, Method Kimomogoro alithibitisha kuwa amepata taarifa kuwa jaji mkuu hatasikiliza rufaa hiyo na badala yake Jaji Luanda ndiye atachukua nafasi yake.
“Ni kweli jaji mkuu hatakuwapo kusikiliza rufaa ya Lema nimewasiliana na Msajili Dar es Salaam ameniambia hatokuwepo kwenye hilo jopo,” alisema Kimomogoro na kuongeza:
Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alisema “Huu ni utaratibu wa kawaida wa mahakama kwa kuwa huenda jaji mkuu akawa amesafiri au ana shughuli nyingine.”
Wakili wa wajiburufaa, Alute Mughwai alisema hajapata taarifa kama Jaji Mkuu ameondolewa kwenye jopo hilo kwa kuwa huo si utaratibu wa mahakama kutoa taarifa hizo.
“Mahakama huwa haitoi taarifa, zinawekwa (taarifa) kwenye ubao wa mahakama siku ambayo rufaa inasikilizwa,” alisema.
Aliendelea, “Jaji yeyote atakayepangwa sisi hatuna tatizo kwa kuwa wote ni majaji, wewe uko huko Dar na mimi niko huku bara (Arusha), hivyo unaweza ukazipata taarifa zaidi huko kwa kuwa ndiyo uko jikoni Dar.”

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma alipoulizwa kuhusu suala hilo hakukataa wala kuthibitisha.
Awali alikana kuwa na taarifa kuwa rufaa hiyo imeshapangiwa tarehe ya kusikilizwa na jopo la majaji, huku akihoji ni ratiba gani hiyo inayoonesha hivyo.
Baadaye alisema kuwa hawezi kueleza jambo lolote kuhusu rufaa hiyo kwa mtu ambaye si mhusika.
“Unafuatilia rufaa ya Lema kwani wewe ni mhusika? Wewe si mhusika katika kesi hiyo wala si wakili wa Lema. Mimi siwezi kukueleza lolote, maana mimi siwajibiki kwako, nawajibika kwa Lema, kwanza wewe nilishakwambia lakini bado tu.” alisema Maruma.
Lema mwenyewe alisema hajui kwa nini Jaji Mkuu amejitoa, lakini akaeleza kuwa anajua wanyonge wataendelea kumwomba Mungu ili afanikiwe kwa kuwa hana mashaka na hatua hiyo iliyofikiwa.
“Mimi sikuzaliwa kuwa mbunge na ubunge kwangu siyo ajira, hivyo sina mashaka na kutokuwepo kwa Jaji Mkuu kwenye kesi yangu,”alisema Lema.
Lema alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, 2012 kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu  wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Baadaye alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupitia kwa wakili wake, Method Kimomogoro kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, huku akitoa hoja 18 za kupinga hukumu hiyo.
Tarehe ambayo rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa na jopo la  majaji watatu Mahakama ya Rufani; Salum Massati, Natalia Kimaro  na  Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande (kiongozi wa jopo), wakili wa wajiburufaa, Alute Mughwai, aliweka pingamizi la awali.
Katika pingamizi hilo, wakili Mghwai aliiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali rufaa hiyo, akidai kuwa ina kasoro za kisheria na za kikanuni huku akibainisha hoja tatu za kuunga mkono pingamizi hilo.
Hoja hizo za pingamizi la awali zilikuwa ni pamoja na kuchanganywa au kutofautiana kwa vifungu vya Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, kati ya hukumu iliyomvua ubunge na hati ya kukaza hukumu hiyo.
Pia hoja nyingine ni kwamba hati ya kukaza hukumu hiyo haikuwa na mhuri wa Jaji aliyeitoa wala tarehe ambayo  hati hiyo ilitolewa.
Hoja ya tatu ilikuwa ni mtindo wa kuandika hati ya kukaza hukumu, kwa kutokuandika maneno, “imetolewa kwa mkono wangu na mhuri wa mahakama.”
Hata hivyo, katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufani ilikubaliana na hoja moja ya pingamizi hilo, kuwa tofauti au kuchanganywa kwa vifungu hivyo vya sheria ni dosari ambayo inaifanya hati hiyo isiwe halali na ikatupilia mbali hoja nyingine mbili kuwa hazina msingi.
Source:  http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1632562/-/vib3j9/-/index.html

Monday, November 26, 2012

Viongozi wa chadema mbaroni kwa wizi wa milioni 16 za umma





Baada ya Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita, wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.
Mwanri alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa, viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42) kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).
Kamanda huyo alisema “Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma.”
Alieleza kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.
Alisema, fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka yaliyopo kijijini hapo.
Alifafanua kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani zilipokwenda.

Kamanda Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili.
Source:  http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/359705-viongozi-wa-chadema-mbaroni-kwa-wizi-wa-milioni-16-za-umma.html

Breaking news: Sharo milionea afariki dunia kwa ajali ya gari

Msanii nyota wa vichekesho na uimbaji Sharomillionea (Ramadhan Hussein) amekufa kwenye ajali iliyotokea huko Tanga. Kijana nyota yake ilikua inaanza kung'ara na kupata dili za matangazo akiwa na Mzee Majuto.
Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

Ridhiwan, Lowassa waelezea utajiri wao

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan wamezungumzia tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwao kwamba wanamiliki rasilimali zenye thamani ya mabilioni ya shilingi.
Lowassa kwa upande wake amekuwa akidaiwa kuwa tajiri anayemiliki kampuni kubwa za kibiashara na kumekuwa na taarifa kwamba ana ukwasi ambao vyanzo vyake vinatia shaka na siyo rahisi kuvitolea maelezo.
Ridhiwani Kikwete akiwa na Baba yake Jakaya Kikwete
Kwa upande wake Ridhiwan naye amekuwa akidaiwa kuwa na utajiri mkubwa na amekuwa akihusishwa na biashara za kampuni za kusafirisha mafuta ambayo hupelekwa kwenye migodi, umiliki wa hoteli na majengo kadhaa ya kifahari.
Wote wawili wamekuwa wakidaiwa kwamba baadhi ya mali zao wamekuwa wakiziendesha chini ya kivuli cha wafanyabiashara wengine wakubwa nchini ili kukwepa kuhojiwa walikotoa utajiri huo, taarifa ambazo hata hivyo imekuwa vigumu kuzithibitisha.
Hata hivyo jana kwa nyakati na mazingira tofauti, Lowassa na Ridhiwan walijitokeza hadharani na kukanusha madai kwamba wao ni matajiri wa kupindukia.
Lowassa kwa upande wake akiwa mjini Mbeya alisema yeye siyo tajiri kama ambavyo imekuwa ikidaiwa lakini wakati huohuo akasema “sijafilisika”.
“Wengi wanasema kuwa mimi ni tajiri siyo kweli, lakini sijafilisika kutokana na kuchangia makanisa kwani nina marafiki wengi ambao wananisaidia katika kuchangia makanisa nao pia hawajafilisika,”alisema Lowassa.
Lowasa alitoa kauli hiyo alipokuwa akiendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanachuo wanawake ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji cha mkoani Mbeya, kinachomilikiwa na Kanisa la Moraviani Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi.
Kiongozi huyo ambaye alichangia kaisi cha Sh25 milioni, alisema kila mtu ana wajibu wa kuchangia elimu na kwamba mwanamke anapaswa kutazamwa kwa karibu zaidi kwani ndiye anayebeba jukumu kubwa la kutunza familia.
Kwa upande wake Ridhiwan alisema: “Ikiwa mimi ni tajiri wa kiasi kinachosemwa, basi mimi ninamzidi Bakhressa (Said Salim, mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki), maana nimepewa kila hoteli hapa mjini, kampuni za mafuta na kila biashara kubwa inayoanzishwa hapa mjini ni ya Ridhiwan”.
Said Salim Bakhressa ni mfanyabiashara ambaye anatajwa kuwa tajiri kuliko wote nchini na anashika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, huku akiwa miongoni mwa wafanyabiashara 10 wanaonyemelea kuingia katika nafasi za juu za utajiri Afrika.
Hata hivyo Ridhiwan ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), aliongeza: “Ninaweza kuwa nafanya biashara moja au mbili, lakini siwezi kuwa mmiliki kiasi chote hicho cha mali.
Mtoto huyo wa Rais Kikwete alikuwa akijibu tuhuma kwamba magari yake kumi ya kusafirisha mafuta yamekamatwa na kuzuiwa katika mpaka wa Kenya na Tanzania, Namanga mkoani Arusha kutokana na kukwepa kodi, taarifa ambayo aliikanusha.
Maelezo ya Ridhiwan
Maelezo ya Ridhiwan yamekua wakati kukiwa na taarifa kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inayashikilia malori mapya 10 ya kubebea mafuta yanayodaiwa kuwa ni yake, yanayodaiwa kuingizwa nchini.
Hata hivyo Ridhiwan alikanusha kuhusika na biashara ya mafuta akisema: “Ili kuwa na utajiri unaotajwa kwangu lazima niwe nimekopa benki au nimeiba, sasa wale wanaonituhumu wasema nimekopa benki gani na kama nimeiba basi wajitokeze watu kulalamika kuhusu wizi nilioufanya”.
Mtoto huyo wa Rais Kikwete, alisema kumekuwa na kile alichokiita uzushi wa ajabu na kwamba hajui wanaozusha mambo hayo wana malengo gani. “Wameanza kusema kwamba nauza dawa za kulevya jambo ambalo siyo kweli, mie sifanyi biashara za aina hiyo, kama kuna jambo jingine tuunguze lakini hilo ni uzushi tu,”alisisitiza.
Habari zilizopatikana jana, zilidai malori hayo mapya yanashikiliwa na TRA kituo cha mpakani cha Namanga kwa madai ya kuwapo “utata” wa malipo ya ushuru wa forodha.
Taarifa za kuzuiwa kwa malori hayo zilianza kuzagaa nchini wiki mbili zilizopita kupitia mitandao ya kijamii ukiwamo mtandao maarufu wa Jamii Forums (JF).
Kulingana na taarifa hizo, watu walioshuhudia magari hayo walidai yalikuwa zaidi ya 70 yakitokea Kenya kutengenezwa bodi huku wengine wakidai yalikuwa ni mapya.
Baadaye taarifa hiyo ilibadilika na kusema kwamba magari hayo yalikuwa 20 na kwamba ni malori 10 tu ndiyo yaliyolipiwa ushuru na kuingia nchini, lakini malori mengine 10 yalikuwa yakiendelea kushikiliwa kutokana na ukwepaji wa kodi.
“Ni kweli hayo magari ni ya huyo bwana mkubwa na yalikuwa 20, lakini 10 yalilipwa ushuru halali”alidai ofisa mmoja wa TRA kituo cha Namanga.
Ridhiwan alisema kuthibitisha kwamba tuhuma hizo ni za uwongo haiwezekani mtu anayetajwa kuwa tajiri kama yeye ashindwe kulipia ushuru wa malori kumi. “Uwongo mwingine huo, kama kweli ningekuwa nina utajiri wote huo, nishindwe kulipia ushuru wa malori kumi tu! Ndo maana nasema ni uwongo tena wa kutunga,”alisema.
Kaimu Meneja wa TRA Arusha, Theresia Mponeja alipulizwa na gazeti hili wiki iliyopita alikanusha kuzuiwa kwa malori hayo na kwamba hakuna taarifa hizo.
Lowassa na elimu
Katika hafla ya jana mjini Mbeya, Lowassa aliendelea kuipigia chapuo elimu akisema: “Ni vizuri vijana wetu wakazingatia elimu kwani bila elimu watashindwa kuhimili ushindani wa ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.”
“Msipozingatia elimu mtabakia kuwa wachota maji na wakata kuni daima. Ni vizuri vijana wetu mkafahamu kwamba bila ya elimu hamtaweza kufika kokote,”alisema kiongozi huyo.
Aliwaasa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili kuweza kuboresha maisha yao na kuisaidia jamii, huku akitaka wajiepushe vishawishi ambavyo vimekuwa kikwazo katika masomo yao. “Hata vitabu vitakatifu vya Mungu elimu imepewa umuhimu mkubwa, Biblia inasema mshike sana elimu na usimwache aende zake kwani huko ndiko uliko uzima wenu, kwa wenzetu Waislamu Quran inasema itafuteni elimu kwa bidii hata Uchina, maana ni kwamba itafute elimu hiyo hata kama utaipata mbali kiasi gani,’’ alisisitiza Lowassa.
Akitoa taarifa ya chuo hicho, Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania, Askofu Alinikisa Cheyo alisema ujenzi wa hosteli hiyo ulianza 2011 na unatarajiwa kuwa na vyumba 87 vitakavyotoa fursa kwa wanachuo 348.
Alisema katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo, kanisa liliomba mkopo kutoka mamlaka ya elimu Tanzania na kukubali kupewa Sh500 milioni na kwamba awamu hiyo iliyoanza Julai 2011, iligharimu Sh580 milioni.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Serikali inaunga mkono juhudi za sekta binafsi hususan madhehebu ya kidini katika kuchangia elimu.
Alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu, madhehu ya dini yanaongoza kwa kuwa vyuo vikuu vingi. Chuo kikuu hicho cha Theofilo Kisanji kilianzishwa 2004, ingawaje kulikuwa na chuo cha Theolojia tangu miaka ya 1960.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1629230/-/item/2/-/9eae0lz/-/index.html

Sunday, November 25, 2012

Waliotumia ARV feki kuiburuta Serikali mahakamani

MIEZI mitatu baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kukamata dawa bandia za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa Ukimwi (ARVs), sasa walioathiriwa na dawa hizo wanajipanga kuifikisha mahakamani Serikali ili kudai fidia.

Wakizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wamedai kuwa Serikali inahusika katika suala hilo, hivyo haiwezi kujichunguza yenyewe na ndiyo maana imeshindwa kuwafikisha mahakamani wahusika hadi sasa.

Shehena ya dawa hizo aina ya TT-VIR 30 yenye toleo namba OC.01.85 zilizotengenezwa na Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd (PTI), iligundulika ikiwa katika hospitali mbalimbali nchini zikiendelea kutolewa kwa wagonjwa.

Hali hiyo ilifanya Serikali ichukue hatua ya kuzuia usambazwaji wa dawa hizo huku ikiwasimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Ubora na Ofisa Udhibiti Ubora wa Bohari hiyo ili kupisha uchunguzi kwa madai ya kuruhusu kusambazwa kwa dawa hizo.

Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Shidepha), Joseph Katto alisema wanajipanga na wakati wowote watakutana na wataalamu huru wa masuala ya afya, wanasheria na wadau wengine kujadili na kuchukua hatua za kulifikisha suala hilo mahakamani.

"Tuna kawaida ya kukutana na wataalamu huru wa masuala ya afya kila linapotokea jambo lisilo la kawaida katika sekta ya afya, hilo ndilo ambalo tunatarajia kulifanya wakati wowote kuanzia sasa," anasema.

Alisema waliotumia dawa hizo walikumbwa na athari nyingi, ikiwa ni pamoja na kuvimba matumbo, ngozi kuharibika na wengine kukumbwa na hali ya kusikia kichefuchefu.

Ofisa Uhusiano wa wizara hiyo, Nsachriss Mwamaja alisema kuwa suala hilo linashughulikiwa na vyombo tofauti,  likiwa tayari kila kitu kitawekwa wazi na kwamba, ikibainika kuna tatizo hatua za kisheria zitafuatwa.


"Suala hili linashughulikiwa na mamlaka nyingi, nafikiri ni vizuri kuvuta subira," alisema Mwamaja.

Katto alifafanua zaidi kwamba, athari za dawa hizo zinaendelea kujitokeza kwa baadhi ya watu wanaoishi na virusi hivyo.

Alisema kuwa dawa hizo zilikamatwa na kuondolewa katika zahanati, vituo vya afya na katika hospitali lakini kwa walaji ziliachwa bila hatua zozote kuchukuliwa wala kutolewa maelekezo yoyote jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu.

"Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wamekumbwa na athari za dawa hizo wapo njiapanda na hawajui wafanye nini.  Kibaya zaidi hakuna mbadala wa dawa hizo feki ambazo Serikali ilikuwa inatoa ruzuku kwa watengenezaji," Katto alisema.

Mwenyekiti huyo alisema anashangazwa na kigugumizi cha Serikali katika kuwafikisha mahakamani wahusika huku wanashuhudia ikiwafukuza  na kuwasimamisha kazi baadhi ya watuhumiwa bila hatima ya waathirika wa dawa hiyo kufahamika kwa wahusika.

Katto alisema anashangaa na wala hajui ni nini majukumu ya Bodi ya Viwango (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kwani Tanzania hivi sasa limekuwa jalala la dawa feki ambazo zinatengenezwa na kusambazwa hadi kwa walaji.

Mwenyekiti wa Shirikisho na Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Tanopha), Julius Kaaya alisema kuwa anashangaa Serikali kwa miezi mitano inamlipa fedha mtu ambaye anawapa dawa feki za kurefusha maisha bila kugundua lolote hadi ilipobainika hivi karibuni.

"Mimi nasema kuwa, Serikali inahusika katika sakata hili, hivyo haitaweza kumsimamisha mtu yeyote mahakamani, labda kiwepo chombo huru," alisema Kaaya.

Alisema kuwa Wizara ya Afya kuna watu hawawezi kuishi bila Ukimwi kuwapo na hao ndio ambao wameitumbukiza Serikali katika biashara hiyo ya dawa feki za kurefusha maisha ambazo tayari zimewaathiri maelfu ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

"Kama Serikali haihusiki basi iwapandishe kizimbani wanaohusika kwani ni kipindi kirefu sasa tangu kiwanda kifungwe na baadhi ya watendaji kusimamishwa ajira," alisema.

Kaaya alilalamika kuwa dawa hizo zimewasababishia  athari kubwa waliozitumia, lakini hadi sasa hakuna mamlaka yoyote iliyochukua hatua.

"Tupo mbioni kukutana na hakuna cha zaidi isipokuwa kuipeleka Serikali mahakamani kwa kuruhusu dawa hizo kuingia sokoni," alisema Kaaya.

Waziri wa Afya

Mara baada ya kukamatwa kwa dawa hizo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema Serikali itawachukulia hatua wahusika wote na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi  yao.

Naibu Waziri huyo alikiri dawa hizo kuingia katika mzunguko na kuwatoa hofu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuwa dawa zilizopo sasa katika mzunguko (baada ya kukamatwa zile za awali) ni salama.
Source: Mwananchi

Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

Waziri wa Nishati na Madini
Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.
2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.


Thursday, November 8, 2012

TAARIFA KAMILI YA ZITTO BUNGENI JUU YA WALIOFICHA FEDHA NA MALI HARAMU NJE YA NCHI

HOJA BINAFSI YA KABWE ZUBERI ZITTO(MB) KUHUSU KULITAKABUNGE  KUCHUNGUZA NA KUILEKEZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA DHIDI YA RAIA WA WATANZANIA WALIOFICHA FEDHA NA MALI HARAMU NJE YA NCHI

[Chini ya Kanuni ya 54(1) na (2)]
UTANGULIZI:
Mheshimiwa Spika,
Mnamo tarehe 2 Novemba 2012 niliwasilisha barua ya kusudio la kuwasilisha Bungeni Hoja binafsi kuhusu suala hilo hapo juu. Lengo la Hoja binafsi hiyo ni kuitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwasiliana na Taasisi ya Benki ya Dunia kupitia kitengo cha ‘Assets Recovery’ kurejesha fedha haramu zilizofichwa na Raia wa Tanzania katika mabenki huko nchini Switzerland. Ofisi yako ilinitaka nilete maelezo ya ziada kuhusu hoja hiyo ili ipatiwe nafasi ya kupangwa kwenye ratiba za Bunge. Baada ya kuleta maelezo hayo Ofisi yako imenipa nafasi kuwasilisha hoja hii mbele ya Bunge lako tukufu. Kwa heshima na taadhima ninawasilisha mbele ya Bunge lako tukufu hoja hii muhimu sana katika kuhakikisha kwamba Taifa letu linaziba mianya ya ufisadi na hususani utoroshwaji wa fedha za kigeni za Tanzania.

Mheshimiwa Spika,
Mwezi Juni mwaka 2012, Benki Kuu ya Switzerland (National Bank of Switzerland) ilitoa taarifa kwa umma kuhusu raia wa mataifa mbalimbali duniani wenye dhamana kwenye mabenki nchini humo. Benki hiyo ilitangaza kwamba Jumla ya dola za Kimarekani milioni 196 (milioni mia moja tisini na sita) zilikuwa zimehifadhiwa kwenye akaunti za mabenki mbalimbali nchini humo na kwamba wenye fedha hizo ni Raia wa Tanzania. Fedha hizo ni zaidi ya shilingi bilioni 314 (mia tatu kumi nanne bilioni) ukizibadilisha kwa thamani ya fedha za Tanzania.

Mheshimiwa Spika,
Mazungumzo yangu ya mwisho niliyoyafanya jana  usiku na wachunguzi waangu binafsi yameongeza taarifa ya ziada muhimu. Kwanza, kiwango cha fedha kinacho milikiwa na watanzania nchini Switzerland peke yake ni takribani mara 20 ya kiwango kilicho tangazwa na Benki ya Tanifa ya nchi hiyo. Kwa mfano, Benki ya UBS peke yake ina maofisa 240 wanaohusika na Tanzania peke yake. Kila ofisa mmoja husimamia mteja mwenye kiwango kisicho pungua dola za marekani milioni 10.

Fedha hizi ni sehemu tu ya fedha ambazo watanzania wanazificha katika mabenki mbalimbali ya nje ya nchi, na ndani ya hesabu hizi hamna fedha zilizo nchi nyingine,kama visiwa Jersey, Mauritius na Cayman Islands maana nchi nyingine hazina utaratibu huu wa kuweka wazi kama ilivyo kwa nchi ya Swistzerland kwa mwaka huu.

Mheshimiwa Spika,
Gazeti la The Guardian On Sunday la tarehe 23 Juni 2012 lilimnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ndugu Edward Hosea akisema kwamba siku ya jumatatu tarehe 24 Juni mwaka 2012 angeandika Barua kwenda Mamlaka za Switzerland kutaka kupewa orodha ya majina ya raia wa Tanzania wenye fedha katika akaunti zilizotajwa. Hata hivyo mpaka ninaleta maelezo haya umma wa Watanzania haujalezwa kama barua hiyo iliandikwa na majibu yake yalikuwa ni nini. TAKUKURU ndio mamlaka pekee hapa nchini ambayo inaweza kupata orodha ya majina ya watu wenye mabilioni haya kwa njia za halali na hasa kwa watu ambao ni ‘Politically Exposed Persons’kama Wabunge na waliowahi kuwa wabunge, Mawaziri na waliowahi kuwa Mawaziri na viongozi wengine wa ngazi za juu katika Taifa letu.

Mheshimiwa spika,
Nchi nyingine duniani zimetumia njia mbali mbali kuhakikisha fedha haramu zinazo toroshwaa zinarejea nchini kwao. Marekani na Ujerumani wao waliamua kununua CDs kutoka kwa waliokua wafanyakazi wa mabenki ya Switzerland, wakagundua Raia wao walioficha fedha nje na kuwatoza kodi kutokana na fedha hizo. Ujerumani wao wameingia mkataba wa kupashana taarifa za kikodi na nchi ya Switzerland ili kuwatoza kidi raia wao wenye fedha huko. Hata hivo mkataba huu wa kikodi haujapitishwa na Bunge la Ujerumani Bundesrat kwani chama kikuu cha upinzani cha SPD kinapinga, na tayari chama hicho kimenunua CDs zenye majina ya Raia wa Ujerumani wenye akiba nje.
Hivi  karibuni gazeti moja nchini Ugiriki limechapisha orodha ya wagiriki walioficha fedha zaio huko Switzerland. Orodha hii inatokana na orodha ambayo alie kua Waziri wa Fedha wa Ufaransa Christine Lagarde aliipa serikali ya Ugiriki, lakini serikali hiyo haikuifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika,
Kiufupi, toka taarifa za Benki ya Taifa ya Switzerland kutangazwa, Serikali haijachukua hatua yeyote ya maana kuhakikisha kuwa suala hili linafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua stahili dhidi ya watoroshaji wa fedha hizo zinachukuliwa ikiwemo kurejeshwa kwa fedha hizo nchini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Ikumbukwe kwamba katika watanzania wenye fedha huko nje wapo ambao fedha zao wamezipata kihalali kutokana na shughuli za kibiashara na wapo ambao wamepata fedha hizi kwa njia za rushwa. Uchunguzi wa kina ni muhimu sana ili kuweza kutofautisha kati ya Fedha haramu na fedha halali. Vilevile uchunguzi unatakiwa kutofautisha katika watu wenye fedha halali kama walifuata taratibu za kisheria za nchi zinazoruhusu raia wa Tanzania wanaoishi Tanzania kuwa na akiba ya fedha za kigeni nje ya Tanzania. Kitendo cha Serikali kukaa kimya bila kuchukua hatua kinaashiria ama kutotimiza wajibu au kwamba wanaopaswa kuchukua hatua ni washirika wa utoroshaji huu wa fedha za nchi na kuzificha katika mabenki ya nje.

Mheshimiwa Spika,
Kabla ya kueleza kwa kina vyanzo viwili vikubwa vya fedha kwa raia wa Tanzania wanaomiliki fedha na mali katika mabenki nje ya nchi nieleze kwamba, Watu hufungua akaunti nje ya nchi au kumiliki mali nje ya nchi kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuficha fedha haramu zilizopatikana kwa njia zisizo halali na mbili kukwepa kodi kutokana na mapato yao. Njia ya kwanza hutumiwa zaidi na wanasiasa na watendaji wa Serikali (Politically exposed Personalities – PEPs) na njia ya pili hutumiwa na wafanyabiashara wakubwa na hasa wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi. Harakati zozote za kuchukua hatua dhidi ya makundi haya yana faida ya kuzuia ufisadi kwa kuonyesha kwamba hakuna pa kujificha iwapo ukifanya ubadhirifu , na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuhakikisha Raia wote wakazi wanalipa kodi inavyostahili.


Uchunguzi wa chanzo cha Fedha.
Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa Taarifa ya Global Financial Integrity (GFI) ya mwaka 2008, jumla ya dola za kimarekani bilioni 8 (dola bilioni nane) zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 mpaka 2008. Kwa bei ya sasa ya dola za kimarekani fedha hizi ni sawa na shilingi trilioni 13 (trilioni kumi na tatu). Mpaka Mwezi Julai mwaka 2012 Deni la Taifa kuanzia mwaka 1961 lilikuwa ni dola za kimarekani bilioni kumi. Hii maana yake ni kwamba fedha zote zilizotoroshwa kutoka Tanzania katika kipindi cha miaka 38 kingeweza kulipia asilimia themanini ya Deni la Taifa. Mwaka 2012/2013 Bunge limeidhinisha jumla ya shilingi trilioni 1.9 kulipia Deni la Taifa.Suala hili ni changamoto kwa nchi mbalimbali za kiafrika ambapo mabilioni yafedha hutoroshwa kila mwaka na watawala wala rushwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwenda nje ya Afrika na kuliacha bara la Afrika likiwa na ufukara wa kutupwa.

Mheshimiwa Spika,
Sehemu ya Fedha hizi zilizotoroshwa zilitokana na ufisadi, nyingine zilitokana na ukwepaji wa kodi na nyingine zilitokana na madeni ambayo Serikali iliingia ambapo sehemu kubwa ya Madeni ilibaki huko huko ughaibuni lakini bado Watanzania wanalipa madeni hayo. Hata hivyo Fedha zilizotokana kutokana Ufisadi na zile za ukwepaji kodi ni nyingi zaidi katika fedha zilizotoroshwa kutoka Tanzania.

Mheshimiwa Spika,
Kwa mfano kati ya mwaka 2003 -  2005 Tanzania iligubikwa na ufisadi mkubwa sana wa Fedha kutoka Benki ya Tanzania ambapo jumla ya shilingi bilioni 155 zililipwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwenda Benki ya NedBank ya Afrika Kusini kama malipo ya mkopo ambao Serikali iliudhamini kwa ajili ya mradi wa uchimbaji dhahabu wa meremeta. Fedha hizi zilikuwa ni mara kumi na tano ya mkopo uliodhaminiwa na Serikali. Uchunguzi wetu unaonesha kuwa asilimia 70 ya fedha za mradi wa meremeta ziliishia kwenye Benki nchini Switzerland kupitia nchi ya Mauritius.

Mheshimiwa Spika,
Kampuni ya Meremeta ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa TanGold ilianzishwa kama mradi wa kutorosha mabilioni ya fedha za nchi kwenda kwa uhusika mkubwa sana wa Serikali. Nawasilisha mezani kwako barua kutoka Ofisi ya Rais Ikulu ya tarehe 20 Agosti 2001, yenye kumbukumbu nambari SHC/M.100/4/A kwenda Benki ya Deutsche Bank tawi la Uingereza kuitambulisha Kampuni ya Meremeta na Kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika ya Kusini ili ipewe mkopo. Barua hiyo inatambulisha miradi miwili ya dhahabu (mgodi wa Tembo na Mgodi wa Buhemba) kwamba ni miradi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Baada ya barua hii yaliyotokea ni mtandao mpana wa kuiba fedha za Tanzania kwenda Afrika Kusini, baadaye Mauritius na kisha kuishia kwenye akaunti za watu binafsi nchini Switzerland na visiwa vingine vya ukwepaji kodi (tax havens). Kufuatilia barua hii kutoka Ikulu, mkopo wa dola za kimarekani milioni kumi zilipatikana. Hata hivyo Serikali ya Tanzania kupitia Benki Kuu ya Tanzania iliilipa Benki ya NedBank jumla ya dola za Kimarekani 138 milioni, dola milioni kumi kati ya hizi zililipwa kupitia kampuni ya Deep Green Finance.

Mheshimiwa Spika,
Nilifanya uchunguzi binafsi kuhusu suala hili. Nilijaribu kuwasiliana na Benki ya NedBank ili kuweza kupata uhakika wa watu waliofaidika na uchotaji huu mkubwa na wa kihistoria wa fedha za umma. Ufuatiliaji huu umeendelea vya kutosha ila haujafika mwisho Hata hivyo taarifa nilizokusanya hadi sasazimeonyesha hatari kubwa namna ambavyo watanzania wenzetu wenye mamlaka wanavyokwapua fedha za umma kwa faida yao. Nyaraka zote za wizi na utoroshaji huu wa fedha na mawasiliano yangu na watu wa Benki ya NedBank nitayawasilisha mbele ya Kamati ya Bunge ninayopendekeza kuundwa ili kutazama suala hili.

Mheshimiwa Spika,
Kuna masuala yanayohusu usalama wa nchi kutokana na kashfa hii ambayo pia ningependa kuyaonyesha katika Kamati ninayopendekeza kuundwa. Nyaraka hizo zinaonyesha silaha na aina za silaha zilizonunuliwa na kutoka nchi gani na kwamba silaha hizo ziliishia wapi. Nimeona kwamba kuyasema masuala haya waziwazi kunaweza kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Hata hivyo masuala haya ni lazima yafahamike ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi ya watendaji wa Serikali watakaokutwa na makosa.
Mheshimiwa Spika,
Fedha zilizoibwa na kutoroshwa kupitia kampuni ya Meremeta na kampuni ya Deep green ziliishia kwenye akaunti za watu binafsi nje ya nchi. Hata hivyo mara baada ya kuundwa kwa kampuni ya TanGold, jumla ya dola za kimarekani milioni kumi ziliwekwa kwenye akaunti ya Kampuni hiyo katika Benki ya NBC, Corporate Branch. Nambari ya akaunti hiyo pia itatolewa katika kamati ninayoomba kuunda kwa ajili ya uchunguzi wa kina.

Mheshimiwa Spika,
Mwaka 2004, 2006 na 2007 Tanzania iligawa vitalu vya kutafuta mafuta na Gesi katika maeneo mbalimbali nchini. Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 56 zililipwa kwenye akaunti za watu binafsi nchini Switzerland kutoka kwenye kampuni zilizoshinda zabuni ya kutafuta mafuta na gesi.

Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi nilioufanya kwa msaada wa wachunguzi waliobobea kwenye masuala ya mifumo ya kifedha ya Kimataifa umeniwezesha kupata nyaraka muhimu zinazoonyesha watu na namna walivyopata fedha walizoweka katika akaunti zao nje ya Tanzania.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2004 na 2005 Mwanasiasa wa Afrika Kusini kutoka chama cha ANC bwana Tokyo Sexwale alitembelea nchini katika ziara ya kibiashara. Alileta marafiki zake wawili na kuanzisha kampuni iitwayo Ophir Energy Tanzania limited. Kampuni hii inamiliki vitalu 3 katika pwani ya bahari ya Hindi blocks 1,3,4. Bwana Tokyo Sexwale alitambulishwa hapa nchini na raia wa Kongo aitwaye Moto Mabanga. Hivi sasa bwana Moto Mabanga ameishitaki kampuni ya Ophir Energy kwa kutotimiza masharti waliyokubaliana kuhusiana na kufanikisha kupatikana kwa vitalu hivyo vya mafuta. Moto Mabanga ndio alikuwa ‘deal maker’wa kampuni hii na ili kufanikisha hali hii alihonga sana wanasiasa na maafisa wa Serikali wanaohusika na ugawaji wa Vitalu vya kutafuta Mafuta na Gesi. Wakati Ophir wanapewa vitalu hivi sehemu ya hisa za kampuni hii ziligawiwa kwa baadhi ya watanzania ikionekana kuwa ni hisa kwa ajili ya chama cha CCM. Hata hivyo uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hisa hizo zilikuwa ni za watu binafsi. Hivi sasa hisa zimeuzwa na fedha kufichwa katika mabenki mbalimbali nje ya Tanzania. Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu umiliki wa kampuni ya Ophir Energy wakati wanaingia nchini na mabadiliko ya umiliki katika kipindi cha miaka minane iliyopita. Vile vile uchunguzi unapaswa kufanywa kwa vitalu vyote vilivyogawiwa katika ya mwaka 2003 mpaka 2008 na umiliki wa Watanzania katika makampuni yaliyopewa vitalu hivyo.

Mheshimiwa Spika, serikali yetu iagizwe na Bunge lako tukufu kupata taarifa za kina kupitia njia za kiserikali na njia za wachunguzi binafsi. Mimi kama Mbunge nilipofikia sasa nahitaji msaada wa Bunge kufanikisha jambo hili. Nilipofikia sasa ni kutoa taarifa na nyakara zote nilizo nazo na watu TAASISI zitakazo saidia kwa kamati teule ambayo Bunge litaunda kushughulikia suala hili mahususi.


Baada ya maelezo hayo, naomba kuwasilisha,
HOJA BINAFSI YA KABWE ZUBERI ZITTO (MB) KUHUSU KULITAKA BUNGE  KUCHUNGUZA NA KUILEKEZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA DHIDI YA RAIA WA WATANZANIA WALIOFICHA FEDHA NA MALI HARAMU NJE YA NCHI

[Inatolewa chini ya Kanuni ya 54(3)]
Mheshimiwa Spika,
KWA KUWAkumekuwa na uthibitisho kutoka Mamlaka za nchi ya Switzerland kwamba kuna raia wa Tanzania wanamiliki fedha za kigeni katika Benki nchini na kwamba kuna kanuni na taratibu za nchi zinazoendesha na kuongoza ufunguaji wa akaunti za fedha za kigeni nje ya Tanzania kwa Watanzania wakazi (residents). Na kwamba kitendo kilichofanywa na wahusika kuweka mabilioni ya fedha kwenye nchi za nje kinaweza kuwa ni kinyume na sheria ya “FOREIGN EXCHANGE ACT, 1992”

NA KWA KUWA sheria hiyo kifungu cha (10) cha Sheria ya Fedha za kigeni kinazuia utoroshaji wa fedha za kitanzania na isipokuwa kwa kibali cha Gavana wa Benki Kuu tu, hakuna mtu yeyote atakaye ruhusiwa  kusafirisha fedha nje ya Tanzania. Na kinaeleza kuwa kwa msafiri anayekwenda nje ya nchi hatoruhusiwa kuondoa na kiasi cha shilingi ambazo zinazidi dola za kimarekani hamsini. Vile vile kwa mujibu wa Sheria hiyo kifungu cha 6 na 7 na waraka uliotolewa na Gavana wa Benki Kuu kwamba Mtanzania yeyote mwenye kutaka kufungua akaunti kwenye mabenki nje ya Tanzania lazima apate kibali cha Gavana.

NA KWA KUWA masharti hayo ya sheria yanaweza kuwa yamekiukwa na wahusika kwa kuhifadhi fedha za kigeni katika mabenki ya nje,

NA KWA KUWA ukiukwaji huo ni dhahiri kuwa fedha zilizowekwa kwenye mabenki ya nje kwa kiasi kikubwa ni fedha ambazo hazikupatika kwa njia za halali na kwamba kuna uwezekano wa ukwepaji mkubwa wa kodi,

NA KWA KUWA, nchi yetu imekuwa katika matatizo makubwa ya fedha za kigeni, jambo ambalo limepelekea nchi kushusha thamani ya shilingi ili kukabiliana na gharama za manunuzi ya bidhaa nje ya nchi,

NA KWA HIYO BASI, ninaliomba Bunge hili liazimie:
1.
Kwamba Bunge lako tukufu liunde Kamati Teule kuchunguza Raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni na mali nje ya Tanzania. Kamati Teule hiyo ifanye kazi zifuatazo:
-
Kuchunguza mfumo mzima wa utoroshaji wa fedha na kufichwa nje ya nchi,
-
kuchunguza na kupembenua mali na fedha haramu dhidi ya halalizinazomilikiwa na raia wa Tanzania katika taasisi za kifedha nje ya Tanzania,
-
kuchunguza utaratibu mzima wa kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi kati ya mwaka 2003 mpaka 2008,
-
kuchunguza mtiririko mzima wa utoroshaji wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania kupitia Kampuni ya Meremeta (pia Triannex pty ya Afrika Kusini na Deep Green Finance ltd) na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya wahusika wote wa utoroshaji wa fedha kwenda nje,
-
kuchunguza umiliki wa wa watanzania kwenye kampuni zote zenye mikataba ya utafutaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini na namna umiliki huo umekuwa ukibadilika, mapato (proceeds) zilizotokana na mabadiliko hayo ya umiliki na kama kodi stahili zimekuwa zikilipwa kutokana na kubadilika kwa umiliki huo,
-
kuchunguza kwa kina mali za Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za Uwaziri Mkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini, Uwaziri wa Ulinzi, Ukuu wa Majeshi, Ukatibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Uanesheria Mkuu wa Serikali, Ukamishna wa Nishati, Ukurugenzi Mkuu wa TPDC, Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi wa TPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.
2.
Kwamba Serikali ilete muswada wa Sheria Bungeni ifikapo Mkutano wa 11 wa Bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma au mume au mke wake au watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3.
Kwamba Serikali iwasiliane na Benki ya Dunia ili kupitia Kitengo cha Assets Recovery Unit mabilioni ya Fedha na mali zisizoondoshekazinazomilikiwa na Watanzania katika mabenki ya nchini Switzerland, Dubai, Mauritius na visiwa na maeneo mengine yote ambapo hufichwa fedha na Mali ili kukwepa kodi na kwamba mali hizo na mabilioni hayo yaliyopatikana kiharamu yarudishwe nchini mara moja
4.
Kwamba katika muswada tajwa hapo juu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aimarishiwe mamlaka ya kutoa kibali kwa Mtanzania yeyote anayetaka kufungua akaunti ya Benki nje ya nchi na kwamba kila mwaka Gavana atatangaza kwenye Gazeti la Serikali na magazeti yanayosomwa na wananchi wengi orodha ya Watanzania walioomba na walioruhusiwa kuwa na akaunti ya Benki nje ya Tanzania.
5.
Kwamba Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na TAKUKURU wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali.
6.
Kwamba Serikali, katika mkutano wa Bunge wa 11 na baada ya Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni kwneye mabenki na mali nje ya Tanzania ilete taarifa ya hatua ilizochukua ili kuziba mianya ya utoroshaji wa fedha nje ya Tanzania.
7.
Kwamba Serikali katika Bajeti ya mwaka 2013/14 itaanzisha kodi maalumu ‘financial transaction tax’ ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction’ ili kuweza kuwa na rekodi za uhakika za fedha ndani na zinazotoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika,

Naomba kutoa hoja,
…………………….
KABWE ZUBERI ZITTO(MB)
JIMBO LA UCHAGUZI-KIGOMA KASKAZINI
08.11.2012

Wednesday, November 7, 2012

Pingamizi rufaa ya Kesi ya Lema ni leo Nov. 8, 2012

USIKILIZWAJI wa uamuzi wa pingamizi za awali wa kesi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), umepangwa kutolewa leo Novemba 8, mwaka huu.
Habari za uhakika kutoka ya Mahakama ya Rufaa inayosikiliza kesi hiyo, zilisema kuwa uamuzi huo utatolewa jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo linasikilizwa na majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, Natalie Kimaro na Salum Massati.
Awali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama, Maximilan Malewo, uamuzi wa pingamizi hizo ulipangwa kutolewa Novemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ingawa wakati Jaji Mkuu Chande akiahirisha shauri hilo jijini Arusha baada ya kusikiliza hoja za pingamizi kutoka kwa mawakili wa wajibu rufaa na majibu toka kwa mawakili wa mleta rufaa, alisema uamuzi huo ungetolewa Oktoba wakati wa vikao vya mahakama hiyo.
Oktoba 2 mwaka huu, rufaa hiyo iliposikiliza kwa mara ya kwanza mjini Arusha, mabishano makali ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote yalitawala katika kesi hiyo ambayo Lema anapinga kuvuliwa na Jaji Gabriel Rwakibarila.
Mabishano hayo yalizuka baada ya upande wa wajibu rufaa kuwasilisha mahakamani hapo hoja zao za pingamizi za awali nne wakidai kuwa rufaa hiyo ni batili kwani imefunguliwa na tuzo ya Mahakama Kuu ambayo ina upungufu wa kisheria kwani haikugongwa muhuri wa mahakama.
Mawakili wa wajibu rufaa, Medest Akida na Alute Mughwai, waliwasilisha pingamizi hilo mbele ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na Jaji Mkuu, Othman Chande, Natalia Kimaro na Salum Massati ambapo upande wa waleta rufaa uliwakilishwa na mawakili, Method Kimomogoro na Tundu Lissu huku Mwanasheria Mkuu akiwakilishwa na mwanasheria wa serikali, Timon Vitalis.
Wakili Mughwai akiieleza mahakama kuwa tuzo iliyotolewa mahakamani haikubaliani na hukumu ya mahakama kwani imezingatia vifungu vya sheria tofauti ambapo kwenye hukumu ilitaja kifungu cha sheria za uchaguzi namba 113 kipengele cha namba moja mpaka saba wakati kwenye kukazia hukumu ilitaja kifungu namba 114 kipengele namba moja mpaka saba.
Aliieleza mahakama kuwa hati hiyo ya kukazia hukumu haikuandikwa kama inavyopaswa kisheria kwani ina upungufu wa baadhi ya maneno yanayoonesha imetolewa na nani, wapi na lini jambo alilodai kuwa imekiuka kanuni za masijala za Mahakama Kuu, hivyo kutaka rufaa hiyo itupwe na mahakama itoe fursa kwa upande wa waleta rufaa kujipanga upya kuleta upya rufaa yao mahakamani.
Katika pingamizi la nne, Mughwai alidai kuwa hati hiyo ya kukazia hukumu haikuwa na muhuri wa Mahakama Kuu jambo alilodai kuwa inaifanya ikose sifa kisheria kwani muhuri ndiyo uhalali wa nyaraka ya mahakama, vinginevyo inakuwa ni karatasi tu.
Akijibu pingamizi hizo za awali wakili Kimomogoro aliieleza mahakama kuwa baada ya Jaji Rwakibarila kutoa hukumu, jalada lilihamishiwa Dar es Salaam, hivyo hakukuwa na muda wa kupitia hukumu na hati ya kukazia hukumu hiyo kwani walikuwa wanaletewa nyaraka hizo kutoka huko.
“Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Rufaa, wakili mwenzetu, Mughwai, ametueleza hapa aliomba mara mbili tofauti apewe tuzo hiyo ikiwa imesahihishwa lakini hakupatiwa majibu, katika mazingira hayo alitegemea sisi tungeipata vipi?” alihoji wakili huyo huku akielezea kushangazwa na hatua ya mawakili wa wajibu rufaa kutowapa nakala ya barua hizo.
Akinukuu maamuzi mbalimbali ya mahakama hiyo kuhusiana na masuala ya hati ya kukazia hukumu pamoja na kanuni mpya za uendeshaji mashauri ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009, Wakili Kimomogoro alisema kuwa si kila hati ya kukazia hukumu yenye upungufu inaifanya iwe batili.
Alisema kuwa hati hiyo ya kukazia hukumu imekidhi vigezo vyote muhimu ikiwemo kuonyesha namba ya kesi, majina na hadhi ya wadau, mambo yaliyokuwa yakidaiwa, imeainisha kilichoamuliwa na mahakama pamoja na gharama.
Aliendelea kuieleza mahakama kuwa hata jaji aliridhika nayo ndiyo maana aliamua kuisaini jambo alilosema kuwa endapo jaji aliridhika kimakosa wao kama mawakili hawawezi kumfuata na kumwambia hapa umeridhika vibaya hebu ridhika vizuri ili tukakate rufaa bali wanachofanya wao ni kuendelea na hatua inayofuata ambayo ni kukata rufaa kama walivyofanya.
Hata hivyo, Kimomogoro alisema kuwa suala la tuzo hiyo kutogongwa muhuri si suala la jaji bali ni suala la utawala kwani anayegonga muhuri mara baada ya jaji kusaini ni msajili wa mahakama.
Alisema kuwa endapo mahakama hiyo itakubaliana na hoja ya pingamizi ya wajibu rufaa kuwa hati hiyo ya kukazia hukumu ni batili basi na mteja wake, Lema atakuwa ni mbunge halali wa Arusha Mjini.
Alisema kuwa makosa yaliyofanyika ni ya kawaida ambayo hayaathiri kiini cha tuzo hiyo kwa kile alichoieleza mahakama kuwa tuzo haiwezi kuwa batili kutokana na mchoro au mamlaka iliyoitoa, bali kinachoangaliwa ni maamuzi yaliyo ndani ya tuzo hiyo.
Aliomba mapingamizi hayo yatupwe kwa gharama za wajibu rufaa kwani kasoro zilizojitokeza zinaweza kurekebishwa wakati shauri hilo likiendelea au kila upande ubebe gharama zake kwenye usikilizwaji wa mapingamizi hayo kutokana na kuwa upande wa wajibu rufaa nao walishaandaa rufaa panda.
Kwa upande wake wakili wa serikali aliieleza mahakama hiyo kuwa anaunga mkono hoja za waleta rufaa huku akiweka wazi kuwa hati ya kukazia hukumu hutolewa kwenye mashauri ya madai ambapo alisema kuwa kazi ya kuweka muhuri si ya jaji bali ni ya masijala ya mahakama kuu.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Jaji Mkuu, Chande, alisema kuwa pande zote zitajulishwa siku ya kutoa uamuzi ambapo aliahirisha kikao hicho kilichoanza tokea Septemba 3, mwaka huu, ambapo tayari mahakama hiyo ilishatoa msimamo kuwa endapo hoja za pingamizi zitasikilizwa basi rufaa itasikilizwa jijini Dar es Salaam katika kikao kinachotarajiwa kukaa mwezi huu.
Source: Tanzania Daima