Kwa wale ambao mnakumbuka kuwa siku ya ijumaa usiku wa manane Polisi
kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiongozwa na RCO wa Kinondoni
walienda nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba usiku kwa lengo la
kumkamata, Mbowe alikuwa safarini na alipitia Airport ya Dsm Hivyo
kwenda kwake usiku ni jambo la kushangaza sana , leo amerejea kupitia
Airport ya Dar na akaamua kwenda moja kwa moja Polisi ili kujua
kulikoni.
Ameambatana na Mawakili wawili, Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala
majira ya saa tisa na nusu aliingia Makao Makuu ya Polisi na huko
wanaendelea na Majadiliano.
Jambo la kushangaza ni kuwa mahojiano yao yanahusu mambo yafuatayo;
1. Kuwa tamko la Kamati Kuu kuwa Polisi walihusika na mlipuko wa Bomu
Arusha... Itakumbukwa alishahojiwa tena na akina Chagonja na mpaka leo
hakuna taarifa zozote wazi.
2. Kuwa Polisi wanatumiwa na CCM ndio maana wanaisaidia CCM Katika
chaguzi mbalimbali ......na hata bomu la Arusha ilikuwa sehemu ya
mkakati huo.
3. Kwamba kauli kuwa JK na Bunge kutokuonyesha dalili zozote za
kusikitishwa na hata kushindwa kuhudhuria mazishi ni dalili za serikali
kuhusika katika tukio hilo.
Kwa ufupi hayo ndio majadiliano yanayoendelea tangu saa tisa na nusu
jioni. Hii , nitaendelea kuwapa updates kadiri nitakavyozipokea.
Maswali ya kufikirisha:
1. Hivi wakina Chagonja Ripoti ya bomu Arusha iko wapi mpaka ahojiwe tena leo upya.
2. Hivi kama Polisi hawatumiki kuisaidia CCM nini maana ya mahojiano ya leo kama sio kule kule kuendelea kutumika kwa Polisi?
3. Hivi, haya yataendelea mpaka lini kama hawa ndio polisi wetu, yaani
alihojiwa na wakina Chagonja, Mungulu, na Makamishina kibao wa makao
makuu ya polisi , leo anaitwa kuhojiwa na RCO wa Kanda ya Kinondoni na
Rpc wake , hivi huko polisi hakuna kuheshimu tena vyeo?
Chagonja kanyoosha mikono ndio maana wanaanza kutafuta pa kutokea?
No comments:
Post a Comment