Search This Blog
Sunday, July 21, 2013
NEMC KUBOMOA HOTELI YA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingiza (NEMC) linakusudia
kubomoa hoteli ya Royal Sunset Beach mali ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es
salaam Willson Kabwe kutokana na kujenga ndani ya eneo la mita 60 kutoka Ziwa
Victoria kinyume na sheria ya usimamizi wa Mazingira kifungu cha 57 pia kumtoza
faini ya Sh10 milioni.
Mbali na hatua hiyo pia NEMC inaweza kuwatia mbaroni watu
wawili ambao ni Wakurugenzi wa Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO) kutokana na
kudaiwa kughushi mihuri, nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa vyeti
bandia vya Tathimini ya Mazingira (EIA) kwa makampuni ya mane ya Jijini Mwanza
na kujipatia fedha kinyume cha sheria.
Mwanasheria wa NEMC Heche Suguta akieleza |
Akizungumza na Waandishi wa habari jana Mwanasheria wa NEMC,
Manchare Heche Suguta alisema watu hao wamekamatwa baada ya kuwekewa mtego na
kutokana na kubainika kuwa walitoa vyeti vya Tathimini ya Mazingira kwa
makampuni ya Bibiti Oil (T) ltd, Nyanza Road Works Ltd, Wang Hill Hotel pamoja
na Brichand Oil Ltd kwa kutozwa kati kiasi cha Dola za Kimarekani 10,000.
Suguta alisema kwamba Vyeti hivyo ambavyo ni Bandia
vilivyotolewa na Mwanza Environment and Conservation of Nature (MEC) pamoja na
Mwanza Region Environment Conservation zote za jijini Mwanza na kubainisha kuwa
wahusika wake wametiwa mbaroni baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa NEMC kama
wateja waliokuwa wakihitaji cheti na kukubaliana nao kutoa cheti kwa Sh5
milioni.
“Kawaida vyeti hivi
hutolewa na kusainiwa na waziri na wala siyo NGO, lakini wao wamekuwa
wakijifanya ni maafisa wetu na kukagua viwanda ama Hetali zilizojengwa ndani ya
maeneo ya Mito, Vyanzo vya maji na ndani ya eneo la Mita 60 kutoka ziwani na
hivyo kujipatia fedha kwa udanganyifu,” alieleza na kuongeza kuwa NGO hizo
mbili zimefungiwa kuendelea na shughuli zake..
Alisema ofisi yake kwa sasa ambao imeunda Kitengo cha Polisi
wa Mazingira kinachosimamiwa na Afisa wa wanaoshughulika na Mazingira kutoka
Jeshi la Polisi, ameanza msako na kwamba watawakamata wale wote wenye vyeti
Bandia vya Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale
wote waliojenga kinyume cha sheria kwa kuwavunjia nyumba zao.
Alisema vyeti hivyo hutolewa na Waziri anayehusika na
Mazingira na kusainiwa naye lakini hivyo vilikuwa vikitengenezwa na NGO hizo na
kutolewa kwa Makampuni hayo jambo ambalo alisema ni kosa na kuwataka wale wote
wenye vyeti bandia kuvisalimisha katika ofisi zao ikiwa ni pamoja na wale
wanaohitaji pia.
Aidha katika zoezi la kuwachukulia hatua waliojenga nyumba
katika maeneo ya fuko za Ziwa Victoria, NEMC tayari inakusudia kubomoa Hoteli
ya Royal Sunset Beach inayomilikiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
na sasa Jiji la Dar es salaam.
“Tayari tumeshamwangia Barua Julai 10, tukimtaka kubomoa
mwenyewe eneo la Hoteli yake ambalo lipo ndani ya MIta 60 ikiwa ni pamoja na
kulipa Faini ya Sh10 milioni kwa kutiririsha maji ndani ya ziwa Victoria,”
alieleza na kubainisha kwamba iwapo atashindwa kubomoa NEMC itabomoa yenyewe na
kumtoza gharama zake.
Akizungumza na Gazeti hili kwa njia ya Simu, Mkurugenzi wa
Jiji la Dar es salaam Wilison Kabwe alieleza kwamba amejenga kwa mujibu wa Sheria na kubainisha
kwamba inaruhusu kujenga vitu ambavyo ‘water related activity’ pamoja na
Majengo ya Muda badala ya kudumu.
“Sheria ina niruhusu kujenga majengo ya muda, miundombinu
yote pale Hotalini siyo ya kudumu ni ya muda. Ninavyo vibali vingine
vinavyoniruhusu kujenga,” alieleza Kabwe.
Hata hivyo mwanasheria wa NEMC alisema sheria ipo wazi na
kubainisha kwamba Hoteli hiyo imejenga Majengo ya Kudumu na kwamba
walichomwagiza katika barua yao ni kumtaka avunge eneo la Mita 60 kutoka ndani
ya Ziwa Victoria.
Ludovick afunguka aeleza uhusiano wake na Mwigulu
Ludovick Josseph |
*Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare
*Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka KATIKA MTANDAO WA MABADILIKO na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.
Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake. Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;
KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWIGULU
Akielezea uhusiano wake na Mwigulu baada ya kuulizwa swali na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Dello, Ludovick alisema ni wa kawaida na kwamba haufikii kama ule wa Lwakatare na Maggid Mjengwa.
“Tumejuana kwenye mitandao ya kijamii na tukadevelop ukaribu, ilitokana na mimi kukosoa mijadala yake na kumpinga.
“Ninayo mahusiano na watu wengi tu nje ya Chadema. Mfano ni huyo Mwigullu, Sixtus Mapunda, Mbunge Kangi Lugora, nk.na sidhani kama ni dhambi hii. Wapo wengi tu wenye uhusiano kama huu. Wote hawa katika nyakati tofauti tumesaidiana mengi.
Katika swali lake lingine, Abdul Dello alihoji: “Ludo, Mwigulu Nchemba alithibitika kukutumia m-pesa ya elfu 50 ilikuwa ya kazi gani?
Ludovick alijibu akieleza kuwa: “Nilikuwa na tatizo binafsi la kifamilia, nilihitaji msaada.”
KUHUSISHWA NA USALAMA WA TAIFA
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hamad alimuuliza akisema:
“Ludo, unasemwa sana mtaani kuwa wewe ni TISS Agent (wakala wa usalama wa taifa) uliyepachikwa pale Chadema kwa ajili ya kuiua kifo cha kawaida na ndiyo maana unafanya kazi nyingi za kujitolea badala ya kwenda kufundisha kama taaluma yako ya ualimu inavyokuruhusu, kweli?
Majibu ya Ludovick yalikuwa hivi: “Nchi hii tunapenda majungu tuuu, na magazeti yetu yamebobea kusambaza majungu na kupakazia watu. Huwezi kuelewa dhana hii hadi ikukute. Juu ya kazi ni tofauti za kimtazamo, so wengine wanapenda kuajiriwa na wengine hawapendi, so haicount hii. Ni uamuzi tu. Niliijua Chadema 2006 na kujiunga rasmi 2009. Hakuna aliyenipachika huko. Ni by conviction, nakuhakikishia hata matatizo yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.”
AELEZA ANAVYOMFAHAMU LWAKATARE
Boniface Magessa alimuuliza hivi: “Ludovick, elezea kidogo unavyomfahamu Lwakatare. Siku ya tukio la kurekodiwa ulikuwa wapi? Kama mlikuwa wote siku hiyo, ulikaa mbele yake au nyuma yake?
Ludovick: “Magessa, Lwakatare tumekutana Bukoba 2010 wakati wa kampeni. Tumefahamiana kwa sababu ya Chadema tu. Na ameendelea kuwa rafiki yangu na kiongozi wangu.
Siku ya tukio la kurekodiwa nilikuwa nyumbani kwake Lwakatare. Siyo muhimu juu ya location”.
MASWALI MENGINE
Leila Sheikh alimuuliza hivi; “Ludo, eti uliwahi kuruka ukuta usiku fulani?
Ludovick: “Da Leilah umefunga wewe? Sasa haya ya kuruka ukuta usiku fulani ni nini tena? Teh teh, hebu fafanua? Marcois, siku hizi kibwagizo changu ni kuwa natazama yote haya nayo ni ubatili mtupu, ni sawa na kufukuza upepo”.
Swali lake lingine lilisomeka hivi: “Kama wewe ni mwanachama hai wa Chadema kwa nini umeitwa 'msaliti' na shabiki wa Chadema kuwa ile kanda ya Lwakatare ulitumwa na Mwigulu kuipiga? Je, ile kanda ni ya kweli?
Inadaiwa kuwa ile kanda inaonesha nia/mpango wa kumuumiza Msacky.
Katika majibu yake Ludovick naye alijibu “Leila, mimi ni Mwanachadema hai. Kuitwa msaliti ni hali halisi ya sasa. Lakini inawezekana kuwa mimi wanayeniita msaliti, siku moja wakaona kuwa ndiye mwokozi. Fikiria kama ningekuwa natumika kama mnavyosema, kwa nini kesi ya ugaidi imefutwa? Si ningesema tu kuwa kulikuwa na watu wengine kadhaa? Kama ninatumika, kwa nini nikamatwe Iringa na kusafirishwa usiku tena chini ya ulinzi mkali? Leila teh teh kwamba nilitumwa kurekodi ile kanda!!! Yaani na Lwakatare naye akatumwa ili aongee haya tunayotuhumiwa kuyapanga? Na je, suala hili ikionekana kuwa ni kweli Lwakatare alilifanya, nani atakuwa msaliti kwa Chadema? Je, chama chetu kinazo sera za kudhuru waandishi? Sasa msaliti ni yule anayechafua chama kwa kupanga mambo yasiyoendana na sera za chama? Au ni yule anaye kilinda chama? Haya si nyote mnajua concept ya whistle blowers? Hamtegemei wawemo ndani ya Chadema?
Na je, kama Mahakama itaamua kuwa tuhuma zetu ni kweli bila chembe ya shaka, ninyi mtaendelea kusema nini, kuwa mimi msaliti au wote sasa tutakuwa wasaliti? Naomba tuachie mahakama suala hili. Kuitwa msaliti wakati unaumia kwa ajili ya hao wanaokuita wasaliti, kibinadamu inaumiza sana. Na hilo ndilo linanitokea.
Kuhusu kwa nini watu wote wananilaumu, si kweli. Wapo wasioona hivyo, ila in a great party propaganda chafu za CCM na za Chadema zimenifanya muhanga wa mambo haya. Uhusiano wangu na Lwakatare kwa sasa ni wa mashaka sana.
Swali jingine la Sheila ni hili: “Je, wewe bado mwanachama wa Chadema? Kama ndiyo, mbona walikutema kwa muda ukakaa rumande bila dhamana? Kwa nini wewe ambaye ni volunteer wa Chadema ulikanwa pale baada ya kushikiliwa na polisi? Huo ndiyo u****wa kafara.
Alijibu hivi: “Mimi ni mwanachama wa Chadema na nakuhakikishia mateso yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.
Masharti ya dhamana hayakuwa wadhamini wawekwe na Chadema, bali watu wawili. Sasa sidhani kama Chadema walikuwa na kesi mahakamani hadi watafute wadhamini. Kuhusu kuwa volunteer wa Chadema ni majungu niliyoyazungumza. Sijawahi kuwa volunteer wa Chadema. Mimi ni mwanachama wa kawaida.
Nyoni Magoha alimuuliza hivi: “Wewe bado una imani na Chadema? Utaendelea kuwa mwanachama hai au umeshajitoa/utajitoa?
Majibu ya Ludovick: “Ninayo imani kubwa sana na isiyotetereka kwa Chadema. Nitaendelea kuwa mwanachama hai”.
Hata hivyo, Ludovick ambaye anatajwa kuhusika na tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alikwepa kuzungumzia jambo hilo na hata alipoulizwa baadhi ya maswali yenye mwelekeo huo.
Kuhusishwa Ludovick na tukio la Kibanda kunatokana na utata wa kauli na mwenendo wake siku ambayo Mhariri Mtendaji huyo alijeruhiwa
Source: http://www.mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=8376:ludovick-afunguka-&catid=25:siasa&Itemid=41
Tuesday, July 16, 2013
Chadema: Tendwa alibariki kuanzishwa ‘Red Brigade’
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alibariki kuundwa kwa makundi ya vijana ndani ya chama hicho, yanayoitwa ‘Red Brigade’.
Hatua hiyo ya Chadema imekuja baada ya Tendwa
kutishia kuifuta Chadema, iwapo wataendelea na mpango wao wa kuanzisha
kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchini.
Katika taarifa yake, aliyoitoa kwa vyombo vya
habari jana, na kusainiwa na Naibu Msajili, Rajab Juma kwa niaba yake,
Tendwa alieleza kushangazwa na kusikitishwa na hatua hiyo ya Chadema kwa
kuwa walishakatazwa mpango huo tangu mwaka 2004.
“Msajili anavikumbusha vyama vyote vya siasa hasa
Chadema kuwa, kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya siasa kinampa uwezo
wa kufuta usajili wa chama chochote kinachokiuka masharti ya usajili au
kifungu chochote cha sheria ya vyama vya siasa. Kifungu cha 20 cha
sheria ya vyama vya siasa kinasema uamuzi wa msajili ni wa mwisho na
hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani,”
alisema Msajili.
alisema Msajili.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema: “Tendwa alikuwepo
kwenye mkutano wa Chadema wa Agosti 13, 2006 uliopitisha katiba mpya ya
chama hicho.
“Katika katiba mpya tuliweka kifungu kinachosema, Chadema itakuwa na chombo cha kulinda
uongozi na mali za chama kikiitwa Red Brigade...Tendwa katika mkutano aliipongeza Chadema kwa mabadiliko hayo ya katiba.
“Katiba ya Chadema ilisajiliwa katika ofisi yake kwa mujibu wa sheria mwaka 2006 na kusema Chadema imekidhi matakwa yote,”
Kuhusu madai ya Chadema kwamba CCM kina kambi ya
namna hiyo, Tendwa alisema hayana msingi, badala yake amekitaka
kuwasilisha ushahidi katika taasisi husika ikiwamo ofisi yake
unaoonyesha kambi za mafunzo za vijana wa CCM, ili suala hilo liweze
kushughulikiwa kisheria.
“Kwa kuwa hivi sasa sheria zinakataza suala hili,
hazijabadilika na viongozi wa Chadema ni walewale waliositisha
kutekeleza mpango huo mwaka 2004, haieleweki nia yao sasa ni nini.
Kama ni kupima matokeo iwapo watatekeleza mpango huo, utakuwa si uamuzi wa busara kwa uhai wa chama chao,’’ alisisitiza msajili.
Alisema kuwa mwaka huo 2004 hata Chama cha
Wananchi(CUF)kupitia kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilfred
Lwakatare kiliwahi kuomba ufafanuzi kwa msajili kuhusu nia yao ya kutaka
kuanzisha mafunzo ya ukakamavu wa kujilinda kwa vijana wake kila
wilaya, ambapo walikataliwa kwa kuwa ni kinyume cha sheria.Msajili pia alitumia fursa hiyo kuviasa vyama vyote vya siasa kutumia
muda wao kufanya shughuli za siasa,ili kuchangia maendeleo ya nchi,
badala ya kutumia uwezo wao na muda kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na
kuhatarisha amani na utulivu nchini.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1916520/-/a5icxkz/-/index.html
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1916520/-/a5icxkz/-/index.html
Polisi asimulia wanajeshi walivyouawa Darfur
Wakati Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa bado
halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko Sudan,
askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio hilo.
Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.
Askari wa JWT ambao ni Majeruhi Dafur |
Gazeti hili limepata majina ya askari hao
waliofariki kutoka vyanzo tofauti lakini limeshindwa kuwataja leo kwa
kuwa JWTZ kupitia kwa msemaji wake, Kanali Kapambala Mgawe limesisitiza
kuwa haliwezi kutangaza majina hayo hadi litakapowasiliana na jamaa za
askari waliofariki.
Tukio lilivyotokea
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari
polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema
mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari
yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa
zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni.
“Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita
waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne
bila kuua mtu.
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena
katika doria waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki,
waliyafuatilia, walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,”
alisema askari huyo na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban
kilometa 70 kutoka katika kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la
kusini na hiyo kambi ya Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”
Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur,
Kanali Mgawe alisema wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye
msafara wa kusindikiza walinzi wa amani.
Makundi yanayopambana
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi
yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja
linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika
katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na
mengineyo.”
Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji
hayo, askari huyo alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa
amani wamepatwa na ganzi... “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu
askari hao wauawe hali haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali
walimohifadhiwa), tunasubiri uhakika.”
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana
vifaa vya kisasa kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na
wenzao kuwa na silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za
mapambano yao,” alisema.
Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema
hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala
ya amani.
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na
kuwafundisha masuala mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja
na wananchi waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi
kushika silaha, wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na
kutusindikiza wakati wa doria,” alisema.
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”
Kauli ya JWTZ
Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha
uvumi wa majina yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu
uliopo, jeshi haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu
watakapotaarifiwa. “Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo.
Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of
kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi
ya kubadilisha kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa
silaha za moto pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni
namba saba ya Sheria za Majeshi ya Kulinda Amani.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1916496/-/13b9r33/-/index.html
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1916496/-/13b9r33/-/index.html
LEO 16/7/1995 NI SIKU YA PROF. KIGOMA ALI MALIMA
Mwaka 1995 ndiyo mwaka ambapo vyama vingi vilianza nchini Tanzania,
lakini ni mwaka huu ambapo mwanachama wa CCM na aliyekuwa waziri katika
serikali ya awamu ya Pili alipoamua kujiondoa CCM.
Nakumbuka ilikuwa 16/7/1995 siku hii CCM walipata mtikisikiko Mkubwa na kumfanya mwalim Nyerere kudondosha chozi hadharani kwani KADA wa CCM na aliyekuwa Waziri wa Elumu wa wakati huo Profesa Kighoma Ali Malima alipotangaza uwamuzi wake wa kuihama CCM. Katika uamuzi huo Mgumu kwake na mchungu kwa CCM na Mwalim Nyerere.
Lakini maskini hakudumu kwani baada ya kujiunga na chama cha NAREA (NRA) National Reconciliation Alliance na kufanya mkutano mkubwa huko Tabora, siku chache baadaye alifariki nje ya nchi.
Maswali bado ni mengi juu ya nini kilimsibu......., lakini leo tunakumbuka haya.

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013
Sisi wananchi wa Tanzania:
• Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
• Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
• Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.
• Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi.
Tunapinga kodi ya laini za simu
KWA SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.
KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.
KWA SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake. Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.
KWA SABABU:- Kodi hii ni juu ya ongezeko la kodi mbalimbali katika huduma za simu za mkononi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushuru kutoka 12% kwenda 14.5% na pia kodi hii kutozwa kwa huduma zote ingawa awali ilitozwa kwa huduma ya matumizi ya kuongea. Hivi sasa utumiaji wa internet, kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi unatozwa kodi. Ongezeko hili pekee limeshafanya huduma za simu za mkononi kupanda gharama kwa kiasi kikubwa. Ongezeko hili la shs 1,000 litazidi kuwaumiza wananchi.
KWA SABABU: - Kodi hii pekee inampunguzia mtumiaji muda wa maongezi na huduma zingine za simu za mkononi ikiwa ataendelea na matumizi yake ya mwezi kama kawaida. Kwa mfano mtumiaji akitumia kifurushi cha bei ya shs 475 inayompa dakika 20 za maongezi, 50 MB za data, na sms 100 kwa masaa 24, kwa kodi ya shs 1,000 kwa mwezi ni sawa na serikali kuchukua siku mbili za kifurushi hiki kila mwezi au ni sawa na kuchukua dakika 40 za maongezi, 100MB za data na sms 200 kila mwezi.
KWA SABABU:- Huduma ya simu za mkononi siyo anasa na ni sehemu muhimu ya mawasiliano na kiungo kinachochangia kurahisisha harakati za maendeleo. Kwa mfano wakulima hutumia huduma hizi katika kuuza mazao yao na kupokea fedha; akina mama wajawazito hupelekewa taarifa muhimu kuhusu afya zao; wanafunzi kupitia internet wanaweza kupata habari muhimu zinazohusiana na masomo yao nk. Kodi hii itawanyima fursa ya kutumia huduma hizi muhimu.
KWA SABABU:- Serikali inaweza punguza matumizi yake mengineyo (safari, posho, semina, manunuzi ya magari na kudhibiti ufisadi) hivyo kufidia pengo litakalosababishwa na kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu.
KWA SABABU:- Pia, utafiti uliofanywa na Interfaith Standing Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja (takriban shs trilioni 1. kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi. Tunaitaka Serikali yetu iongeze ufanisi wa kukusanya kodi kutoka vyanzo vilivyopo tayari na kuondoa misamaha kwa hivyo itaziba pengo la shs billioni 264 kutoka kwa kodi ya laini ya simu za mkononi.
MWISHO
Tunakuomba ufikishe ujumbe kwa wengine kwa kuwapa link ya hii petition ili nao washiriki maamuzi haya muhimu.
Tembelea: http://www.avaaz.org/en/petiti on/WITO_WA_KUSITISHA_TOZOKODI_ YA_LAINI_YA_SIMU_KILA_MWEZI_ KUFUATIA_MABADILIKO_YA_SHERIA_ YA_KODI_2013/?pv=4
• Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
• Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
• Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.
• Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi.
Waziri wa Fedha Mgimwa |
Tunapinga kodi ya laini za simu
KWA SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.
KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.
KWA SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake. Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.
KWA SABABU:- Kodi hii ni juu ya ongezeko la kodi mbalimbali katika huduma za simu za mkononi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushuru kutoka 12% kwenda 14.5% na pia kodi hii kutozwa kwa huduma zote ingawa awali ilitozwa kwa huduma ya matumizi ya kuongea. Hivi sasa utumiaji wa internet, kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi unatozwa kodi. Ongezeko hili pekee limeshafanya huduma za simu za mkononi kupanda gharama kwa kiasi kikubwa. Ongezeko hili la shs 1,000 litazidi kuwaumiza wananchi.
KWA SABABU: - Kodi hii pekee inampunguzia mtumiaji muda wa maongezi na huduma zingine za simu za mkononi ikiwa ataendelea na matumizi yake ya mwezi kama kawaida. Kwa mfano mtumiaji akitumia kifurushi cha bei ya shs 475 inayompa dakika 20 za maongezi, 50 MB za data, na sms 100 kwa masaa 24, kwa kodi ya shs 1,000 kwa mwezi ni sawa na serikali kuchukua siku mbili za kifurushi hiki kila mwezi au ni sawa na kuchukua dakika 40 za maongezi, 100MB za data na sms 200 kila mwezi.
KWA SABABU:- Huduma ya simu za mkononi siyo anasa na ni sehemu muhimu ya mawasiliano na kiungo kinachochangia kurahisisha harakati za maendeleo. Kwa mfano wakulima hutumia huduma hizi katika kuuza mazao yao na kupokea fedha; akina mama wajawazito hupelekewa taarifa muhimu kuhusu afya zao; wanafunzi kupitia internet wanaweza kupata habari muhimu zinazohusiana na masomo yao nk. Kodi hii itawanyima fursa ya kutumia huduma hizi muhimu.
KWA SABABU:- Serikali inaweza punguza matumizi yake mengineyo (safari, posho, semina, manunuzi ya magari na kudhibiti ufisadi) hivyo kufidia pengo litakalosababishwa na kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu.
KWA SABABU:- Pia, utafiti uliofanywa na Interfaith Standing Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja (takriban shs trilioni 1. kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi. Tunaitaka Serikali yetu iongeze ufanisi wa kukusanya kodi kutoka vyanzo vilivyopo tayari na kuondoa misamaha kwa hivyo itaziba pengo la shs billioni 264 kutoka kwa kodi ya laini ya simu za mkononi.
MWISHO
Tunakuomba ufikishe ujumbe kwa wengine kwa kuwapa link ya hii petition ili nao washiriki maamuzi haya muhimu.
Tembelea: http://www.avaaz.org/en/petiti
Monday, July 15, 2013
Analysis ya Matokeo ya Udiwani katika Uchaguzi wa Udiwani hivi karibuni.
WILAYA |
KATA |
CCM |
CHDM |
CUF |
NCCR |
DP |
APPT |
ADC |
NRA |
TOTAL |
WINNER |
former |
Loser
|
Nachingwea |
Stesheni |
806 |
327 |
480 |
- |
- |
- |
- |
- |
1613 |
CCM |
CCM |
|
Sengerema |
Nyampulukano |
1073 |
1476 |
38 |
45 |
- |
- |
- |
- |
2632 |
CHDM |
CCM |
CCM lost |
Sengerema |
Lugata |
2214 |
1044 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
3258 |
CCM |
CCM |
|
Muheza |
Genge |
347 |
326 |
6 |
- |
- |
- |
- |
- |
679 |
CCM |
CCM |
|
Muheza |
Tingeni |
362 |
244 |
4 |
- |
- |
- |
- |
- |
610 |
CCM |
CCM |
|
Bahi |
Ibungule |
863 |
248 |
- |
- |
- |
9 |
- |
- |
1120 |
CCM |
CCM |
|
Chemba |
Dalai |
1361 |
1027 |
377 |
- |
- |
- |
- |
2765 |
CCM |
CCM |
||
Mbinga |
Langiro |
- |
-NO |
- |
-C |
-O |
-N |
-T |
-E |
-ST |
CCM |
CCM |
|
Serengeti |
Manchilla |
676 |
625 |
16 |
- |
- |
- |
- |
- |
1317 |
CCM |
CCM |
|
Mbeya |
Iyela |
1163 |
1918 |
- |
12 |
20 |
- |
- |
- |
3113 |
CHDM |
CCM |
CCM lost |
Mufindi |
Mbalamaziwa |
1420 |
184 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
1604 |
CCM |
CCM |
|
Kilolo |
Ng'ang'awe |
686 |
217 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
903 |
CCM |
CCM |
|
Bukombe |
Runzewe west |
612 |
529 |
- |
- |
- |
- |
153 |
1294 |
CCM |
CCM |
||
Temeke |
Mianzini |
1283 |
315 |
494 |
- |
- |
- |
25 |
9 |
2126 |
CCM |
CCM |
|
Ulanga |
Minepa |
1196 |
1029 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
2225 |
CCM |
TLP |
TLP lost |
Kilombero |
Ifakara |
3746 |
4106 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
7852 |
CHDM |
CCM |
CCM lost |
Kilosa |
Masanze |
948 |
638 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
1586 |
CCM |
CCM |
|
Monduli |
Makuyuni |
1547 |
360 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
1907 |
CCM |
CCM |
|
Arusha |
Themi |
326 |
678 |
313 |
- |
- |
- |
- |
- |
1317 |
CHDM |
CHDM |
|
Arusha |
Kimandolu |
1169 |
2665 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
3834 |
CHDM |
CHDM |
|
Arusha |
Kaloleni |
389 |
1019 |
169 |
- |
- |
- |
- |
- |
1577 |
CHDM |
CHDM |
|
Arusha |
Elerai |
1239 |
1715 |
213 |
- |
- |
- |
- |
- |
3167 |
CHDM |
CHDM |
|
Babati |
Bashnet |
1130 |
2008 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
3138 |
CHDM |
CCM |
CCM lost |
Mbulu |
Dangobesh |
968 |
1558 |
5 |
- |
- |
- |
- |
- |
2531 |
CHDM |
CCM |
CCM lost |
Singida |
Iseke |
791 |
831 |
96 |
- |
- |
- |
- |
- |
1718 |
CHDM |
CHDM |
|
Mtwara |
Mnima |
918 |
206 |
626 |
414 |
- |
- |
- |
- |
2164 |
CCM |
CUF |
CUF Lost |
Kura
kata zote |
27233 |
25293 |
2837 |
471 |
20 |
9 |
178 |
9 |
56050 |
||||
Asilimia |
49% |
45% |
5% |
1% |
0% |
0% |
0% |
0% |
100% |
Positions of the Parties before and After.
CCM |
CHADEMA |
CUF |
TLP |
TOTAL |
|
Wards
Before |
19 |
5 |
1 |
1 |
26 |
Wards
After |
16 |
10 |
0 |
0 |
26 |
Gainers and Losers
Losers
(Former Seats lost) |
Gainers
(New seats gained) |
Net
Final position |
TLP – Lost 1 to CCM |
CHADEMA – Gained 5 from CCM |
CHADEMA GAINED 5 |
CUF
– Lost 1 to CCM |
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF) |
CCM LOST 3 |
CCM – Lost 5 to CHADEMA |
TLP – LOST 1 |
|
CHADEMA - none |
CUF
– LOST 1 |
Ni matumaini yangu kuwa namba zinajieleza vizuri.
1. Asilimia ya Kura:
CCM wamepata 49%, Chadema 45%, CUF 5% vyama vingine 1%
2. Ushindi wa Jumla wa Kata:
CCM wameshinda kata 16 (moja wameshinda bila kupiga kura kwa kuwa hakukuwa na wagombea wa upinzani) na Chadema wameshinda kata 10.
3. MLINGANISHO NA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA UCHAGUZI 2010
- Chadema wameongeza viti 5
- CCM wamepoteza viti 3
- TLP na CUF wamepoteza kiti kimoja kimoja.
Subscribe to:
Posts (Atom)