Search This Blog
Monday, January 28, 2013
Msanii Lulu (Elizabeth Michael) aachiwa kwa dhamana
Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maaarufu kwa jina la Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba.
Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.
Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.
Lulu ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani, kuripoti mahakamani kila siku ya kesi yake ikiwa ni pamoja na wadhamini wake kuweka bondi ya Shilingi mil 20.
Saturday, January 26, 2013
Serikali yapata Mkemia mkuu mpya
KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. HUSSEIN A. MWINYI AMEMTEUA PROF. SAMWEL VICTOR MANYELE, KUWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.
WAZIRI WA
AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. HUSSEIN A. MWINYI AMEMTEUA PROF. SAMWEL VICTOR
MANYELE, KUWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.
KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO WAZIRI, AMEMTEUA PROF.
MANYELE KUTUMIKIA NAFASI HIYO KUANZIA TAREHE 21/1/2013. AWALI PROF. MANYELE
ALIKUWA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
NAFASI HIYO ILIKUWA WAZI BAADA YA ALIYEKUWA MKEMIA MKUU
WA SERIKALI MAREHEMU DKT. ERNEST MASHIMBA KUFARIKI TAREHE 19 SEPTEMBA,
2010.
NSACHRIS
MWAMWAJA
MSEMAJI WA
WIZARA
25/01/2013
Thursday, January 24, 2013
Tibaijuka atenganisha Mji wa Kigamboni na Temeke
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ameanzisha Wakala wa Kuendeleza Mji wa Kigamboni (KDA). Kwa
maana hiyo, mji huo hautakuwa tena chini ya mamlaka ya Manispaa ya
Temeke.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Profesa Tibaijuka alisema Serikali imeamua kuanzisha wakala huo
ili pamoja na mambo mengine, upange na kusimamia ujenzi wa mji wa kisasa
katika eneo hilo.
“KDA imeanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa
Serikali ya 1997 ili iweze kuhakikisha mji unajengwa na unakuwa bora,”
alisema Profesa Tibaijuka.
Alisema kutokana na kuanzishwa kwa KDA, kata zote
za Kigamboni, zitaungana na madiwani wake pamoja na mbunge wao watakuwa
wakikutana katika Baraza la Ushauri la KDA.
“Kutakuwa na Baraza la Kigamboni ambalo madiwani na mbunge wao wataingia humo kujadili maendeleo ya mji huo na leo (jana), kutakuwa na kikao cha kwanza,” alisema Profesa Tibaijuka.
“Kutakuwa na Baraza la Kigamboni ambalo madiwani na mbunge wao wataingia humo kujadili maendeleo ya mji huo na leo (jana), kutakuwa na kikao cha kwanza,” alisema Profesa Tibaijuka.
Alizitaja kata hizo kuwa ni Kigamboni, Tungi,
Mjimwema, Vijibweni, Kibada, Pemba Mnazi, Kimbiji, Kisarawe II,
Somangila, Kendwa, Sinda Chini na Sinda Juu.
Profesa Tibaijuka alisema eneo lote la Kigamboni lenye hekta 50,935, litaendelezwa na wananchi 80,000 wa eneo hilo watanufaika.
Profesa Tibaijuka alisema eneo lote la Kigamboni lenye hekta 50,935, litaendelezwa na wananchi 80,000 wa eneo hilo watanufaika.
Profesa Tibaijuka alisema wananchi wa Kigamboni
ambao wako kwenye maeneo ambayo yatahitajika kwa ajili ya ujenzi huo
watashirikishwa ipasavyo katika mchakato mzima ikiwa ni pamoja na
kulipwa fidia zao kwa wakati.
Alisema fidia itatolewa kwa kila mwananchi na
wahusika watahamishiwa katika maeneo mengine ndani ya mji huohuo wa
Kigamboni, ili kupisha ujenzi.
“Mwananchi yeyote ambaye hatajisikia kubaki
Kigamboni atalipwa fedha zake na kwenda kuishi kokote anakotaka iwe ni
Kimara au Kibaha ataamua mwenyewe na tayari majengo ya kuwahamishia
yameshaanza kujengwa,” alisema.
Profesa Tibaijuka alisema ni wakati wa Watanzania
wanaoweza kuendeleza eneo la Kigamboni kujitokeza ili wapewe ‘blocks’ na
kuondokana na suala la viwanja.
Alisema zaidi ya Sh11 trilioni zitatumika kujenga mji huo mpya ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo 2032.
Alisema zaidi ya Sh11 trilioni zitatumika kujenga mji huo mpya ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo 2032.
“Bajeti ya mwaka huu tulihitaji Sh600 bilioni,
lakini tukapewa asilimia 10 ya fedha hizo ambayo ni Sh60 bilioni.
Tunajipanga na hii ni moja ya mipango yetu kufanikisha ujenzi huo.
Katika awamu ya kwanza tutahitaji kiasi cha Sh3 trilioni ili
kuifanikisha.”
Mbunge hataki
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile amepinga kuanzishwa kwa KDA na kueleza ni kuongeza gharama kwa Serikali akataka Manispaa ya Temeke iwezeshwe ili isimamie mji huo.
Mbunge hataki
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile amepinga kuanzishwa kwa KDA na kueleza ni kuongeza gharama kwa Serikali akataka Manispaa ya Temeke iwezeshwe ili isimamie mji huo.
“Walishakuja na kutueleza hilo suala hata hivyo,
sisi na manispaa tulikataa kwa kuwa uwezo wa kufanya kazi hiyo manispaa
inayo hivyo hatuikubali mamlaka hiyo,” alisema Dk Ndugulile.
Aidha, alikanusha taarifa ya Profesa Tibaijuka
kuwa angekutana nao katika mkutano wa Baraza jana akieleza kuwa hakuna
mkutano kama huo kwa kuwa yeye na madiwani wenzake hawajataarifiwa.
“Hakuna kikao chochote na sisi hatujahusishwa. Kikao kilichokuwapo leo ni cha Kamati ya Fedha ya Manispaa tu,” alisema Dk Ndugulile.
Chanzo:Mwananchi
“Hakuna kikao chochote na sisi hatujahusishwa. Kikao kilichokuwapo leo ni cha Kamati ya Fedha ya Manispaa tu,” alisema Dk Ndugulile.
Chanzo:Mwananchi
Sunday, January 20, 2013
Maskini DCI Manumba!
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la
Polisi (DCI), Robert Manumba bado ni tete na jana Rais Jakaya Kikwete
alikwenda tena ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika Hospitali ya Aga
Khan, Dar es Salaam alikolazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi
(ICU), kumjulia hali.
DCI Robert Manumba |
Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine waliofika hospitalini hapo kumjulia hali DCI Manumba ni Mke wa Rais, Salma, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Said Mwema na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni. Pia walikuwapo ndugu, jamaa na marafiki ambao walikusanyika hospitalini hapo takriban siku nzima jana wakifuatilia afya yake.
Rais Kikwete alifika hospitalini hapo jana saa 11:15 na alitumia takriban dakika 10 tu kwani alitoka saa 11:26 huku akionekana mnyonge na alielekea kwenye gari lake na kuagana na IGP Mwema na Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee kisha kuondoka.
Juzi, Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo mara baada ya kumsindikiza Uwanja wa Ndege mgeni wake Rais wa Benin,Thomas Boni Yayi aliyekuwa nchini kwa ziara ya siku moja.
Jana, Mke wa Rais alikuwa wa kwanza kufika hopitalini hapo saa 10:20 na aliondoka saa 10:45 muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufika.
Habari zilizopatikana jana zilieleza kwamba kutokana na afya yake kuwa mbaya, wageni wengi wakiwamo viongozi waandamizi, walizuiwa kuingia kumwona.
Uongozi wa Aga Khan watoa tamko
Jana mchana, uongozi Aga Khan ulitoa taarifa rasmi kuzungumzia afya ya kiongozi huyo wa Polisi huku ukieleza kuwa kimsingi siyo nzuri na bado anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.
“Uongozi wa Hospitali ya Aga Khan ungependa kuujulisha umma kwamba Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Manumba bado yupo hospitalini Aga Khan ambako anaendelea kupatiwa matibabu. Hali yake bado inahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Juzi, Dk Dharsee alisema Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na malaria huku hali yake ikiwa mbaya na hajitambui.
Msemaji wa familia atoa mafumbo
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, msemaji wa familia ya DCI Manumba, James Kilaba alisema: “Maisha ndivyo yalivyo, huwezi kuzua ugonjwa na huwezi kubadili uhalisia wa mambo. Sisi kama familia, tunaamini Mungu yuko na ndugu yetu na ndiye atatenda yake na naomba Watanzania wamuombee.”
Hata hivyo, alikataa kuzungumzia ugonjwa wake zaidi ya kusema kuwa alipelekwa Jumanne iliyopita hospitalini hapo kwa ajili ya vipimo zaidi.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza yadaiwa kuitapeli fedha NSSF
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza chini ya
Mkurugenzi wake Willson Kabwe, imeingia katika kashfa baada ya kulipwa
Sh1.6 bilioni na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa lengo wa
kununua viwanja 692 katika eneo la Bugarika na Kiseke, lakini
haikufanya hivyo.
Kashfa hiyo iliibuliwa juzi wakati Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Kashfa hiyo iliibuliwa juzi wakati Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo iliwakutanisha maofisa wa NSSF na
uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo
hilo lililodumu kwa miaka mitano.
Akitoa maelezo kwa wabunge hao, Kaimu Mkurungenzi
wa NSSF, Ludovick Mroso, alisema mfuko wake uliingia mkataba na
halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Kabwe na kwamba hiyo ilikuwa
mwaka 2008.
Alisema mkataba huo ulikuwa ni kwa ajili ya
kununua jumla ya viwanja 692 ili kujenga nyumba za kuuza, lakini licha
ya kuwalipa, bado hawajatoa viwanja kwa NSSF.
Kwa mujibu wa nyaraka za makubaliano baina ya NSSF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza wa Agosti 18, 2008, NSSF iliingia mkataba wa jumla ya Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kupewa viwanja.
Kwa mujibu wa nyaraka za makubaliano baina ya NSSF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza wa Agosti 18, 2008, NSSF iliingia mkataba wa jumla ya Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kupewa viwanja.
Katika mkataba huo uliosainiwa na Kabwe na
mwanasheria wa Jiji John Wanga (wakati huo), utaratibu wa malipo ulikuwa
ni katika awamu tatu.
Awamu ya kwanza ilihusisha fedha Sh943 milioni sawa na asilimia 50 mara baada ya mkataba kusainiwa zikiwa ni kwa ajili ya kulipa fidia.
Awamu ya kwanza ilihusisha fedha Sh943 milioni sawa na asilimia 50 mara baada ya mkataba kusainiwa zikiwa ni kwa ajili ya kulipa fidia.
Awamu ya pili ya malipo ilikuwa ni Sh755 milioni
sawa na asilimia 30 zikiwa ni fedha zilizopaswa kulipwa baada ya ujenzi
wa barabara katika viwanja na malipo ya awamu ya tatu na ya mwisho
ilikuwa ni asilimia 20.
Kwa upande wa NSSF waliweza kukamilisha asilimia
80 ya malipo kwa awamu ya kwanza na ya pili kwa kulipia jumla ya Sh1.6
bilioni hadi kufikia Juni 2011, lakini Halamshauri ya Jiji hakuweza
kuwakabidhi viwanja hadi jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji alidai kuwa mpango huo wa
viwanja 300 vya NSSF huko Bugarika ulikwama kutokana na eneo hilo
kuibuka vurugu baada ya wananchi wamiliki wa mashamba kuhamasishwa na
Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (Chadema) kuanza vurugu. Nkamia
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho alisema
maelezo ya Jiji yamekataliwa na wabunge na kwamba sababu za kudai
walikwamishwa na mbunge wa Chadema ni za uzushi na kuwaomba kuandaa
maelezo zaidi ili wawasilishe katika kikao maalumu mjini Dodoma mbele ya
waziri wao.
“Hapa tumebaini kuna uhuni mwingi sana. Tumekataa upuuzi huu, Jiji walilipwa fedha ili kutoa viwanja kwa NSSF lakini viwanja hivi wameviuza kwa watu wengine huku wakidai kisa ni Mbunge.
Sasa tumewaita mjini Dodoma mwezi ujao wakati wa
vikao vyetu vya Bunge ili waje waeleze mbele ya waziri wao,” alieleza
Nkamia na kubainisha hata hivyo alisikitishwa na kukosekana kwa
mkurugenzi mwenyewe.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1670262/-/xl8quy/-/index.html
Wednesday, January 16, 2013
Opresheni Linda Tembo. Pambana na Ujangili
Na Zitto Kabwe
Mabaki ya Mzoga wa tembo aliouawa hifadhi ya Buligi |
Mwaka
mzima uliopita, 2012, ulijaa habari za kukamatwa kwa shehena za meno ya
Tembo kutoka Tanzania huko HongKong zikielekea China. Mwezi Disemba
shehena yenye tani 1.3 ya meno ya Tembo iliyofichwa kwenye magunia ya
Alizeti ilikamatwa na Maafisa wa Forodha wa HongKong. Shehena hii
ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni moja na nusu. Wiki
mbili kabla ya hapo takribani tani nne za meno ya Tembo zilikamatwa huko
huko HongKong. Kwa matukio haya mawili, hawa ni sawa na Tembo 900
waliouwawa.
Mwezi
huo huo wa Desemba, 2012 Polisi mkoani Arusha walikamata nyara nyingi
za Serikali katika eneo la Kisongo. Nyara hizi ni pamoja na ngozi za
Simba na wanyama wengine, pembe za ndovu na wanyama wengine na vichwa
vya wanyama. Nyara hizi zilikuwa tayari kwa kuuzwa nje ya Nchi. Mkoani
Katavi walikamatwa majangili kadhaa na kuachiwa huru kwa amri kutoka juu
kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa wanyama pori.
Ujangili
umeshamiri sana na kwa kasi ya kutisha. Takwimu za Serikali zinaonyesha
kuwa mwaka 2010 jumla ya Tembo 10,000 waliuwawa hapa Tanzania peke
yake. Hii ni sawa na Tembo 37 kila siku. Hali imekuwa mbaya zaidi mwaka
2012 ambapo jumla ya Tembo 23,000 waliuwawa sawa na wastani wa Tembo 63
kila siku. Kwa hesabu ya haraka, kutokana na kasi hii ya ujangili,
ifikapo mwaka 2017/2018 Tanzania haitakuwa na Tembo hata mmoja. Hivi
sasa Tanzania ina Tembo kati ya 150,000 na 170,000. Maafisa wengine wa
Wanyama pori wanasema Tembo wanafika 250,000 na nusu ya Tembo hao wapo
pori la Selous kusini mwa Tanzania. Sote tuna wajibu wa kulinda urithi
huu tulioachiwa na MwenyeziMungu.
Kasi
ya ujangili imechangiwa na mambo mengi sana lakini kubwa ni kukua kwa
uchumi wa China na nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa Asia. Kwa hiyo
takribani nchi zote za Afrika zenye Tembo zinaathirika na Biashara hii
ya Pembe za Ndovu. Tanzania, Kongo-Kinshasa na Msumbiji zipo kwenye
hatari zaidi ya Tembo wake wote kumalizika kutokana na nguvu kubwa
waliyonayo wafanyabiashara haramu wa Pembe za Ndovu. Kenya na Nigeria
inasemekana jumla ya Tembo 25,000 waliuwawa mwaka 2011 peke yake.
Inasemekana kuwa kuongezeka kwa wafanyabiashara wengi kutoka China na
hivyo wafanyakazi kwenye makampuni ya Kichina kuzagaa Afrika kunachangia
kwa kiasi kikubwa sana Ujangili na biashara hii haramu.
Pembe za ndovu zilizokamatwa katika operesheni dhidi ya biashara ya magendo huko Hong Kong zikioneshwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari |
Mtandao
wa Ujangili ni mpana na wenye nguvu sana za pesa, kisiasa na kimamlaka.
Mtandao huu huanzia chini kabisa kwenye Mapori na Hifadhi ambapo wauaji
ni watu masikini wa vijijini na wengine hutumia magobole tu. Hawa
hulipwa kwa kuua tu. Wakataji nao huingia hapo na kukata meno na kuandaa
usafiri ambao hufanywa wakati mwingine na magari ya Serikali. Hivi
karibuni gari za polisi, muhimbili na hata magari ya viongozi wa dini
yamekamatwa na meno ya Tembo huko mkoani Iringa. Baada ya kusafirishwa
na kufikishwa maeneo ya mijini hufungwa na kusafirishwa kupitia bandari
ya Dar es Salaam. Katika mtandao huu kuna watu wa Vijijini, masikini
ambao hutumia ujangili kama sehemu ya kupata kipato. Pia kuna watu wa
kati kama maafisa wa Polisi, maafisa wa wanyama pori, madereva wa magari
ya Serikali wenye tamaa tu kuongeza kipato. Juu kabisa kuna
wafanyabiashara wakubwa na inasemekana pia wanasiasa ambao hulinda
biashara hii.
Nina karibia kumaliza kitabu cha kurasa 301 kiitwacho “Killing for Profit: Exposing the illegal Rhino Horn Trade” ambacho kimeandikwa na Mwandishi wa habari Julian Rademeyer wa Afrika Kusini.
Kitabu hiki ni cha uchunguzi ambapo mwandishi amechunguza mtandao mzima
wa biashara haramu ya meno ya Faru. Mwandishi anasema, kule nchi za
Kusini Mashariki mwa Asia kama Vietnam, meno ya Tembo na Meno ya Faru
yana bei kubwa kuliko dhahabu na madawa ya kulevya. Anasema Biashara hii
imejaa tamaa za mali na rushwa ya kiwango cha juu. Mwandishi anaonyesha
kwa ushahidi namna biashara hii ilivyotumika kuendeleza vita Msumbiji
na Angola kwa nguvu ya Serikali ya Makaburu. Hata baada ya ukaburu
kuisha anaonyesha namna ambavyo wanasiasa watawala wanaendeleza biashara
hii na kupata fedha za kampeni.
Katika
kitabu hiki Mwandishi anathibitisha kuwa Meno ya Tembo na Meno ya Faru
huko Asia hutumika kama mapambo kwa kutengeneza bangili zenye bei aghali
na kwa matajiri na mapambo mengine kwenye mikufu, herein nk. Hata hivyo
anasema meno haya hutumika kama dawa na hasa dawa za kuongeza nguvu za
kiume kwa wanaume na hivyo kusababisha bei yake kuwa kubwa sana. Jinsi
uchumi wa Mataifa hayo unavyokuwa na kuongeza watu wa tabaka la kati,
ndivyo mahitaji wa Meno ya Tembo na Faru yanaongezeka. Mwandishi
anaonyesha kwamba mwaka 1960 kulikuwa na Faru 100,000 katika nchi za
Zimbabwe na Afrika Kusini. Hivi sasa kuna Faru 2400 tu. Nadhani ni
muhimu kupata pia takwimu za Tanzania kuonyesha hali upande wetu ipoje.
Watafiti waliofanya tafiti kwenye eneo hili watujuze.
Jambo
moja lipo wazi hapa Tanzania ni kwamba maeneo ya Hifadhi za Taifa
takwimu za Ujangili ni chache kuliko maeneo ya mapori ya Akiba kama
Selous. Hii inatokana na ukweli kwamba maeneo ya mapori ya Akiba uwezo
wan chi kulinda wanyama ni mdogo sana maana hakuna askari wa kutosha na
waliopo maslahi yao ni madogo sana. Hivyo moja ya pendekezo la dhati
kabisa ni kuimarisha ulinzi kwenye mapori ya Akiba. Pori kama Selous
ambalo ni urithi wa Dunia ni vema liundiwe mamlaka yake (Selous Games
Authority) kama ilivyo Mamlaka ya Ngorongoro. Mapori mengine yawekwe
chini ya wakala wa Serikali na yawezeshwe kutokana na mapato ya uwindaji
wa Kitalii. Lazima kutoa motisha ya kutosha kwa Askari wa wanyama pori
na pia kutoa adhabu kali sana kwa askari atakayejihusisha na ujangili.
Hata
hivyo, wataalamu wa wanyamapori wanasema ‘kuua majangili hakuleti
mafanikio yeyote. Kuna watu wengi sana masikini wapo tayari kuingia kuua
Tembo ili wapate pesa kidogo. Hata ukiua mamia yao, hawatamalizika.
Suluhisho pekee ni kuua soko la biashara hii haramu’. Soko hili litakufa
kwa kuusambaratisha mtandao wa ujangili kwa kuanzia na wafanyabiashara
wakubwa. Hii ndio opresheni. Operesheni linda Tembo. Sasa ianze.
Tafuta
namba ya simu ya Mbunge wako au mbunge yeyote mwandikie “nataka ulinde
Tembo wetu #OperesheniLindaTembo kwa kuihoji na kuiwajibisha Serikali”.
Mabadiliko ni Mimi, Ni wewe, Ni sisi. Tumia simu yako kutaka viongozi
wako wawajibike. Ni wajibu wetu kikatiba kulinda urithi wetu.
Thursday, January 10, 2013
Mtikila: Kagame amepenyeza Wanyarwanda 35,000 nchini
MAANGAMIZI YA KUTISHA YA WANANCHI WA BULIGI
Hii ni Taarifa ya kuteketezwa zaidi ya nyumba 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma kwa moto, pamoja na tani nyingi za mazao yao ambayo ni pamoja na mpunga, mahindi, maharagwe, mtama, dengu, uwele, serena, pamoja na mali zao zingine, katika eneo liitwalo Buligi, katika Wilaya ya Muleba. Unyama huu wahusika wamejaribu kuuficha kwa jina la ‘Opresheni Okoa mazingira’.(Wanyarwanda wahusika na unyama dhidi ya Wasukuma)
Mchungaji Mtikila |
Ni lengo la Katiba ya Nchi yetu na Sheria pamoja na taarifa ifuatayo, kwamba wote waliohusika na maangamizi haya waadhibiwe vikali, na wananchi wote waliofanyiwa unyama huu ni lazima walipwe fidia za mali zao na mateso ya kutisha waliyopata. Baada ya kuchomewa nyumba zao na mali zao zote wananchi wengi wamelundikana makanisani, na wengi wako maporini wakikimbia unyama wa kutisha na kuporwa mali zao. Vijiji vilivyoteketezwa ni pamoja na Nyamiranda, Itunzi, Kasharara na Kiteme. Uharamia uliendelea mpaka maeneo ya Karagwe na Biharamulo kama alivyoeleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika vyombo vya habari, kama gazeti la Mtanzania Toleo nambari 7142 la tarehe 17/11/2012. Utetezi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe wa maangamizi ya kutisha ya Wasukuma, kama ulivyokuwa ule wa Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, kwamba ilikuwa opresheni maalum iliyolenga kuondoa wahamiaji haramu wenye maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi ya Taifa ya Buligiuna ukweli. Lakini Wasukuma si wahamiaji haramu, kwa sababu ni wazawa katika nchi yao, na hayo maelfu ya ng’ombe katika hifadhi si ya Wasukuma bali ni ya Watusi wa Rwanda.
Hakuna asiyejua kuwa malengo makuu ya kuanzishwa Umoja wa Mataifa ni pamoja na kulinda haki na usawa wa binadamu wote ulimwenguni, ili idumu amani na kuleta maendeleo katika kuboresha maisha ya binadamu. Ndiyo maana ile sera ya Makaburu ya udhalilishaji wa mtu mweusi au ubaguzi wa rangi waliyoiita apartheid ilipigwa vita na dunia yote, mpaka ikatokomezwa. Hata ushujaa wa Nelson Mandela unaopita umaarufu wa kiongozi mwingine yeyote duniani, aliupata kwa sababu ya uhanga wake katika kutetea usawa wa binadamu wa rangi zote duniani. Lakini apartheid ya Makaburu haikuweza kuufikia ushetani wa Watusi, jinsi wanavyowadhalilisha Wahutu na Wabantu wengine, kwa imani yao chafu sana kwamba wao eti waliumbwa kwa ajili ya kutawala tu, na kwamba Wahutu waliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao! Ni makufuru yanayojulikana wazi ya Watusi kuwatema mate Wahutu au Wabantu wengine kwa kinyaa kama vile ni mavi mbele zao. Na imani yao hii ya kishetani ndilo chimbuko la mbinu na mikakati yao yote ya kutawala siyo tu Maziwa Makuu bali hatimaye hata Afrika yote ya ‘watumwa’ wao! Tabia ya Watusi ya kula wao kwanza, halafu kuwatupia makombo watumwa wao (Wahutu), tena baada ya kuyatemea mate na makohozi, ni historia inayojulikana na kila mzawa wa Maziwa Makuu. Hata maendeleo yalipozidi kutowesha giza hili, bado wanawake Watusi walilazimika kudumisha udhalili wa Wabantu kwa kuolewa na wale wenye mali lakini mimba wapate kwa Watusi wenzao, ikibidi hata kwa ndugu zao wa damu kama hakuna Watusi wengine karibu. Historia itamuenzi shujaa Gregory Kayibanda wa Rwanda kuliko inavyomuenzi Nelson Mandela wa Afrika Kusini, kwa kutokomeza ile apartheid chafu kupindukia ya Watusi nchini Rwanda mwaka 1959. Ukweli ni budi uheshimiwe na dunia kwamba Watusi wengi walikimbia kutoka Rwanda kufuatia mapindizi yale, kwa sababu ya kukwepa balaa ya kuwa chini ya watumwa wao! Watusiwalikimbilia Burundi na Tanganyika kwa baba yao Julius Nyerere, kujipanga kwa ajili ya “kurudisha ubwana wao juu ya watumwa wao” Rwanda. Kwa imani ya kishetani ya Watusi, Watanganyika kwao wao ni mataahira tu kama Wabantu wenzao yaani Wahutu. Hata bila kupayuka Watusi wanarithishana imani kwamba sisi tuliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao. Ubwana wa Watusi uliimarishwa kwa kupandikizwa utwana katika mioyo ya Watanganyika, wa kuwaona Watusi kuwa bora kuliko Wahutu pamoja na hata sisi wenyewe! Hali hii ndiyo iliyowezesha Watusi kujipenyeza katika sehemu zote nyeti za utawala wa Nchi yetu, pamoja na uhodari wao katika matumizi ya rushwa ya mapesa na chambo cha wanawake zao (the Tutsi sexual diplomacy). Ndivyo Watusi walivyofanikiwa hata kuiteka kifikra jumuiya ya kimataifa, ikabariki na kuwasaidia kuangamiza Wahutu zaidi ya milioni sita, na hata kugeuza kibao kuhusu genocide ya Rwanda kwamba Wahutu ndio walioangamiza Watusi! Ndiyo maana nchi yetu ilipokuwa na wakimbizi wa Kitusi na wa Kihutu, Watusi walipendelewa kwa kuhudumiwa kama wafalme na kuandaliwa kurudi “kuikomboa” Rwanda. Kwani ingawa Rwanda ilikuwa na utawala wa kidemokrasi wa Wahutu walio wengi kwa asilimia 85% Watusi wakiwa asilimia 14% tu, ni haramu Watusi kuwa chini ya Wahutu kwavile eti ni watumwa wao! Ni kweli kwamba matokeo ya ufisadi na utwana wa watawala wetu wanaoamini katika ubwana wa Watusi, ni pamoja na kufurahisha Watusi na baba yao Nyerere kwa kuhusika kwa serikali yetu katika yafuatayo: 1. Maangamizi ya Wahutu zaidi ya 6,000,000, 2. Uvamizi wa Jamhuri ya Rwanda kupitia Uganda na Burundi, ambapo maandalizi kwa sehemu kubwa yalifanyikia nchini mwetu kwa mkono wa Serikali ya CCM. 3. Kuhusika kikamilifu na mauaji ya kinyama ya marais watatu Wahutu wa Burundi na Rwanda yaani Melchior Ndadaye, Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamira pamoja na ujumbe wao wote, na ushetani mwingine wa kutisha. 4. Kujiuza utumwani kwa Watusi, na kutumika kuliingiza eneo la Maziwa Makuu katika Himaya yao, kwa kuwasaidia kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati hawana sifa kabisa kulingana na Mkataba wa Uundaji wa Jumuiya(EAC), kwa unyama wa ‘apartheid’ na genocide yao. 5. Kusaidia uvamizi wa DRC uliofanywa na Kagame na Mseveni, watawala wetu wakaivika aibu kubwa Nchi yetu kwa kukataa kushiriki katika Jeshi la SADC (SADC Alliance) la kusaidia ndugu zetu dhidi ya maharamia, Nchi yetu ikaongopea dunia bila aibu kwamba eti haiko upande wowote kati ya wavamizi na mnyonge aliyevamiwa! 6. Kuwarudishia RPF Wahutu takriban milioni moja kwa unyama usiosemeka, waliokuwa wameyakimbia mauaji ya kinyama ya RPF baada ya kuvamia nchi yao, RPF wakawapokea na kuwaangamiza wote, na kumwaga maiti zao kwa maelfu katika mto Kagera, zikawa zinafunika Ziwa Victoria mpaka General Mboma alipotoa Tamko la kuvamia Rwanda kukomesha ushetani huu wa RPF, kama wasingeacha unyama huo mara moja. Nchi yetu inakabiliwa na kisasi cha Mwenyezi Mungu! Na ishara tayari zinaonekana! Kuna kuacha upumbavu na kutengeneza na Mwenyezi Mungu, ama mapigo makali kuliko yaliyoipiga Misri, yatakayosimuliwa vizazi vyote! Kwa ufisadi na utwana wa watawala wa nchi yetu kwa Watusi, bila chembe ya aibu wala hofu kwa Mwenyezi Mungu waliikaribisha katika ardhi yetu ICTR, ikiwa nyenzo maalum ya kuwasaidia Watusi kuangamiza Wahutu wote wenye uwezo kiuchumi na kifikra duniani! Kenya iliikataa ICTR katika ardhi yake, kwa kumwogopa Mungu kwa sababu ni nyenzo ya genocide iliyoangamiza mamilioni ya Wahutu, ikawafuata mpaka na wale milioni 2.5 waliokuwa wamekimbizia uhai wao Mashariki ya Congo, na kuwateketeza kinyama! Kupenyezwa kwa Watusi katika ngazi zote nyeti za utawala wa nchi yetu kumewezesha Utusi kuteka nyara sera za nchi yetu zitumikie maslahi ya Watusi, kwa gharama ya heshima ya utaifa wetu na maslahi ya nchi yetu. Na siyo siri kwamba msingi wa laana hii yote iliyoonywa na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati, ulijengwa na dikteta Julius Nyerere, ambaye leo anawekwa mahali pa Mwenyezi Mungu na kufanyiwa ibada ya ‘ubaba’ wa Taifa! Utekelezaji wa ndoto ya Nyerere ya kuweka eneo lote la Maziwa Makuu chini ya Himaya ya Watusi unasimamiwa na vijana wake, madikteta Yoweri Museveni na Paul Kagame aliyeangamiza mamilioni mengi ya binadamu duniani kuliko Adolf Hitler. Propaganda za ‘Jumuiya au Shirikisho la Afrika Mashariki’ zinazopigiwa debe kwa nguvu na hawa Watusi, ni katika ujenzi wa hiyo Himaya yao. Dikteta Yoweri Museveni ametangaza mara kadhaa haki yake ya kustahili kuwa Rais wa kwanza wa shirikisho la Maziwa Makuu (Himaya ya Watusi), na anacho kikosi cha majasusi zaidi ya 400 ndani ya Nchi yetu, yanaoiyeyusha nchi yetu kwa ajili ya kumezwa katika Himaya hiyo, na mafanikio yanaonekana kwa jinsi utawala wetu wa CCM unavyonyenyekea Watusi na kujidhalilisha kwao.KIINI CHA MATATIZO YA WATUSI DUNIANI
Mwuaji wa kutisha Paul Kagame alikwishaikamata DRC baada ya kufanikiwa kumwua Rais Laurent Kabila, akampenyeza madarakani Mnyarwanda Hypolite Adrien Christophe Kanambe kwa jina bandia la ‘Joseph Kabila’. Wauaji wa Rais Laurent Kabila baada ya kutoroshewa Rwanda walikimbiziwa hapa, ambapo walihamishiwa Norway kimya kimya. Mnyarwanda “Joseph Kabila” anayetawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama Gavana wa dikteta Paul Kagame, ni ndugu wa damu wa Mkuu wa Majeshi ya Kagame, yaani James Kabarebe, ambaye pamoja na Kayumba Nyamwasa ndio waliosimamia yale mauaji ya kutisha ya wale Wahutu milioni 2.5 waliokuwa wamekimbilia DRC, ilipovamiwa nchi yao na wauaji wa RPF. Ni sera ya Rwanda kuhakikisha kuwa DRC haiwi na Jeshi imara, mpaka hapo mkakati wa Himaya yao utakapokamilika. Ndiyo sababu maafisa wa juu 7,000 wa Jeshi la DRC ni Wanyarwanda. Hypolite Kanambe (Joseph Kabila) anatumikia maslahi ya Rwanda kwa uzalendo wa hali ya juu, na Rwanda inapovamia DRC pilika za Hypolite A. C. Kanambe huwa ni usanii tu wa kuhadaa ulimwengu. Vinginevyo lazima DRC ingewapa silaha askari Wahutu waliojichimbia Congo, ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuutokomeza unyama wa Watusi. Hata uvamizi wa Rwanda wa RPF ulifanikiwa kwa kutanguliza vikwazo vikali sana, vilivyohakikisha kuwa majeshi ya Hayati Rais Habyarimana hayawi na silaha. Historia ni budi iwe sahihi, kwamba vijana wa Nyerere yaani Museveni na Kagame walivamia Zaire kwa maelekezo ya baba yao, bila hayati Laurent Kabila, kwa malengo ya kupanua Himaya yao na kuteka tani za dhahabu na madini mengine mengi ya thamani Gbadolite, Kilomoto, Kinshasa, Kisangani na kwingine, kwa ajili ya kujipatia mabavu ya kiuchumi ya kupanulia Himaya yao, na kugharamia propaganda kali inayohadaa jumuiya ya kimataifa. Dunia ilipoanza kupigia kelele uvamizi huo, ndipo Nyerere alipomtafuta Laurent Kabila haraka, zikiwa zimepita wiki mbili baada ya uvamizi kuanza, na kumtanguliza yeye mbele katika kuhadaa ulimwengu, kwamba ni Wakongo wenyewe walikuwa wanaikomboa nchi yao kutoka kwa dikteta Mobutu! Uvamizi ulipoingia Kinshasa Kabila aliwageuka Watusi kizalendo, na kuwaambia sasa warudi kwao wawaachie Wakongo nchi yao. Kwani aliyekusudiwa na Watusi kuwa gavana wa Rwanda wa koloni hilo ni Bizimana Karahamheto au ‘Bizima Karaha’ kwa jina la hadaa. Uporaji wa kutisha wa utajiri wa DRC ndio mtaji wa jeuri yote ya Kagame leo, ya kuchezea amani ya Maziwa Makuu, na kusambaza maelfu ya majasusi katika nchi za kusini mwa Afrika, kuzifanyia kazi chafu ili hatimaye zimezwe katika Himaya yao, mbali ya kugharamia kikosi chake cha Escadron de la mort kinachoua wapinzani wake popote walipo duniani. Siri ya mkakati wa Nyerere wa Himaya ya Watusi ilionekana tangu alipotaka kuchelewesha uhuru wa Tanganyika, eti mpaka majirani wapate wao ili mkakati ufanikiwe, uhuni ambao ulishindwa kuuhadaa ushujaa kama wa Jomo Kenyatta. Mzee Jomo Kenyatta alipogundua jinsi Nyerere anavyochezea uhuru wa wana wa Tanganyika, hatimaye akaunajisi kwa ‘Muungano’ kwa ajili ya maslahi ya Wamarekani katika vita baridi, alilaani kwamba “Hakika Nyerere anatawala maiti” Ndiyo maana ni Watanganyika peke yao duniani wasiojali uhuru wao, wala hatima yao na vizazi vyao vijavyo, wala maslahi ya Nchi yao! Hii ni baada ya kupigika vizuri vichwani mwao ili wawe kama makondoo ya mtawala, waweze kuvikwa kwa ulaini kongwa la utumwa kwa Watusi, kwa maslahi ya kifisadi ya watumwa walio madarakani, wanaouza utu wao na hatima ya Nchi yao kwa utamu wa tende na halua, zinazomung’unyika mara moja na kupotea! Saa ya ukombozi ni sasa! Ndivyo utaahira wetu unavyoonekana kwa dunia yote ya wenye akili kuhusu kongwa la utumwa la Watanganyika liitwalo “Muungano”, lenye maslahi ya kifisadi ya watwana wachache sana wanaotawala, kama si mmoja tu, lakini kwa gharama ya Uhuru wa Watanganyika, heshima yao na utambulisho wao kama Taifa takatifu la heshima tangu katika Unabii wa Mwenyezi Mungu, tena kwa gharama ya raslimali za Watanganyika na matrilioni ya fedha ya damu yao! Utaahira wetu sisi Watanganyika unaonekana zaidi baada ya Zanzibar kujitoa rasmi katika huo ‘muungano’ kikatiba, ambapo kwa ajili ya maslahi ya kifisadi watawala wetu wanafumbia macho ukweli kwamba muungano umebatilika! Na kwa ujinga kama wa kuku anapodhani haonekani kwavile amefunika macho yake kwa bawa lake, hawa nao wamekazana kuudanganya ulimwengu kwamba muungano bado upo, na hata kulazimisha raia waukiri kiwendawazimu usanii huo! Lakini ukweli ni kwamba baada ya Zanzibar kujitoa rasmi yaani kikatiba katika muungano, Wazanzibari ni wachache sana mafisadi na wasaliti waliohongwa madaraka watetee bila haya usanii wa muungano batili, kwa maslahi yao ya kibinafsi, huku wakisingizia maslahi ya ukupe wa Taifa lao (parasitic advantages) katika damu ya Watanganyika.. Kama chatu anavyomvunjavunja mnyama ili awe rahisi kumezeka, ndivyo Nyerere alivyowahasi kifikra Watanganyika na kuwafisha ari ya ukombozi wao na utaifa wao, mpaka kwa kafara ya mwenge, ili wawe rahisi kuvishwa kongwa la utumwa la Watusi. Upofushaji wa jinsi hii huua kabisa uzalendo ndani ya dhamiri ya kila raia katika nchi, na kuwaacha wananchi katika minyororo ya woga tu akilini mwao, badala ya uhanga kwa ajili ya Taifa lao.KUMEZWA KWA DRC KATIKA HIMAYA YA WATUSI
Uharamia anaoufanya Kagame kule Mashariki ya Congo hapa kwetu alifanikiwa siku nyingi. Tofauti ya DRC Mashariki na mikoa yetu ya Kagera na Kigoma ni kwamba wenzetu wanayo hata majeshi ya mgambo ya uzalendo wao yanayotetea ardhi yao na uhuru wao, kama vile Mai Mai. Lakini sisi tuliuawa kabisa uhanga wetu kwa ajili ya Nchi yetu. Tumebaki kuwasujudia wageni wanaoteka na kuipora nchi yetu, na kututia utumwani katika nchi yetu wenyewe. Hii ndiyo raha ambayo Nyerere aliwaandalia Kagame na Mseveni kwa Watanganyika. Kagame tayari ameingiza katika Nchi yetu Wanyarwandazaidi ya 35,000 wenye silaha, wengi wakiwa katika mapori ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi na maelfu ya ng’ombe waliowaingiza kutoka kwao Rwanda na Uganda. Kwani kule kwao wamejiwekea sheria kali ya kuokoa mazingira yao, kwamba ni marufuku mtu kumiliki zaidi ya ng’ombe tano (5). Kwahiyo mamia ya maelfu ya ng’ombe zao wameziingiza katika ardhi yetu kwa njia za porini, na wapo Wanyarwanda wenye ng’ombe mpaka 10,000 mtu mmoja ndani ya Nchi yetu. Maelfu mengi ya ng’ombe hao wa Wanyarwanda wanajulikana kuwa mali ya dikteta Paul Kagame mwenyewe na mawaziri wake, na wengine ni mali ya dikteta Yoweri Mseveni, wengi wakiwa hata na mihuri ya NRA! Mbali ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi, maelfu mengi ya ng’ombe wao wamewaswagia katika mapori yetu ya Kasindaga, Katete, Kinesi (Karagwe), Nyakerera, Kyobuheke na Misambya na kwingineko, ambako Wanyarwanda wamejikatia mabuloku makubwa sana (Blocks) ambayo wazawa hawaruhusiwi kukanyaga, na wakithubutu ni kuuawa. Kitendo cha Kagame na Museveni cha kuifanya Nchi yetu kwamba haina Utaifa na heshima ya mipaka yake (sovereignty and territorial integrity) kama zilivyo nchi zao, ni Tangazo la Vita! Ni lazima tujibu mapigo kwa nguvu kuliko tulivyomjibu dikteta Idd Amin Dadah. Majeshi yetu yaanze mazoezi makali ya vita, na raia waanze upya mafunzo ya mgambo kwa ajili ya Nchi yetu. Kama lilivyoanza tatizo la uvamizi wa Kagame DRC Mashariki, maelfu ya Wanyarwanda tayari wamekamata ardhi yetu kubwa sana, kwa kutumia vibali bandia vya kuishi nchini, na makaratasi ya uraia bandia wa Nchi yetu. Jasusi la Kagame liitwalo Athanas Kafurama mara nyingi hudhalilisha wazawa wa nchi yetu kwamba hawana kitu vichwani, na kwamba Tanzania inamjali mtu mwenye pesa yaani kama wao, na siyo raia wake walalahoi! Kagame amefanikiwa kwa sehemu kubwa kuiteka kimya kimya mikoa yetu ya Kagera na Kigoma! Hata Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe unamwuma moyo, jinsi Kagame na Mseveni walivyopenyeza askari zaidi ya 35,000, waliojichimbia na maelfu ya ng’ombe, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Buligi. Wanyarwanda wamekamata ardhi yetu kubwa sana, bila kuwa hata na vibali vya kuwepo nchini mwetu. Kabla ya kueleza zaidi juu ya uvamizi wa Buligi mkoani Kagera, tunapenda ifahamike kwamba Mkoa wa Kigoma umeingiliwa na Wanyarwanda na Warundi zaidi ya 100,000, ambao tayari wameteka sehemu kubwa ya ardhi ya Taifa letu, katika upanuzi wa Himaya yao. Tena wanajipenyeza kupitia katika makanisa maalum yanayoeleweka. Tayari wameanza kufanikiwa kukamata utawala wa Nchi yetu, kama vile Mnyarwanda aitwaye Peter Serugamba alivyoteka Jimbo la Kigoma Mjini, au Diwani John wa Kata ya Gungu. Watusi wamegundulika kuwamwagia rushwa viongozi wa vijiji na vitongoji ambao wanawatumia kuiteka ardhi yetu, na nafasi hizo wamepanga kuzichukua wao katika kuijenga Himaya yao. Vikao vya Watusi vya mikakati yao ya kuitwaa Nchi yetu katika Himaya yao mjini Kigoma hufanyikia katika hoteli ya Coast View, iliyojengwa kwa mtaji uliotoka Rwanda, ambao ni utajiri ulioporwa Congo. Watusi hawafichi katika majigambo yao, kwamba wanaweza wasilazimike kutumia nguvu za kijeshi kuitwaa ardhi ya Tanzania, kwa sababu eti wanaweza kutumia rushwa tu na akili kuichukua yote bila shida! Wanaujua udhaifu wetu kwa sababu walijipenyeza katika ngazi zote za utawala wa Nchi yetu, katika majeshi yetu, Uhamiaji, Taasisi zetu za fedha, Usalama wa Taifa n.k. Ndiyo maana Nchi yetu takatifu imetumika katika unyama wa kutisha kwa maslahi ya Watusi. Ni kweli pia kwamba nchi yetu inao watawala wanaoweza kununuliwa kirahisi kwa mapesa ya Wanyarwanda, ng’ombe zao na au mabinti wa Kitusi. Ndiyo maana wanampigia debe na kumwinamia mwuaji wa kutisha Paul Kagame, wakati wanajua kabisa kwamba: 1. Kagame amemwaga kinyama sana damu ya mamilioni ya Wahutu, ambao bado anaendelea kuwaua usiku na mchana, kuliko Adolf Hitler alivyowaua Wayahudi. 2. Kagame anaendesha mauaji dunia nzima, kwa kutumia kikosi chake maalum cha Escadron de la mort, ambacho ndicho alichotumia hata kumwangamiza Bingwa wetu wa Sheria, Hayati Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kosa la kuweka wazi katika ICTR kwamba mtuhumiwa mkuu wa genocide katika Maziwa Makuu ni dikteta Paul Kagame. Kagame alihofia kwamba kutokana na majumuisho ya mwisho ya Mwanasheria huyo, lazima Ulimwengu ungelazimisha kukamatwa kwake na kufikishwa mbele ya Sheria. 3. Kagame akiwa na cheo cha Meja alikuwa mstari wa mbele kumwua Rais Thomas Sankara wa Burkina Faso, kule Uagadougou. 4. Kagame alikuwa Burundi kwa ushirikiano wake muhimu na Jean Bikomagu, katika mauaji ya kikatili sana ya marehemu Rais Melchior Ndadaye. 5. Kagame ndiye aliyehusika kikamilifu na utunguaji wa ndege iliyomchukua Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda pamoja na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi. 6. Kagame analaaniwa na dunia nzima kwa kumfanyia unyama wa kutisha mwanasiasa mwanamke, shujaa Victoire Ingabire, ambaye amemtupa gerezani kwa kosa la kugombea Urais wa Rwanda akiwa Mhutu, na kosa la kuwa na kibali kwa wananchi wa Rwanda kuliko yeye aliyeloa damu ya mamilioni ya binadamu aliowaua kinyama. 7. Kagame amemwaga majasusi zaidi ya 1,000 katika Nchi yetu, wanaotumia ufisadi wa mapesa, ngono n.k katika kutengeneza mazingira ya kutekwa utawala wa nchi yetu na Watusi na hatimaye nchi yetu kuwa mkoa wa Himaya yao. Kama ilivyoelezwa juu, maelfu yao wamefanikiwa kujipenyeza katika taasisi zote nyeti za dola ya Nchi yetu. Walipoishika Uhamiaji waliitumia kujipa uraia na kukamata nafasi nyeti na ardhi yetu pia. 8. Maelfu ya majasusi wa Kagame wanajifanya wanashughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda, wengine wanajifanya wafanyabiashara au wanatafuta kuwekeza, wengine wanajifanya wanafunzi. Lakini ukweli ni kwamba Taifa letu liko uchi kwa Kagame, kwa sababu kila tunachokifanya katika Nchi yetu kinaripotiwa Rwanda masaa 24. Katika Jiji la Dar es Salaam, Mikocheni ndiko walikojaa Wanyarwanda hao kama kwao. ANGALIZO: Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 kwa sababu moja tu kwamba ilishindikana viongozi wa nchi tatu wananchama yaani Tanzania, Kenya na Uganda kukutana pamoja, kwa ajili ya kupitisha maamuzi yote muhimu ya uendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya. Kwa sababu Rais Julius Nyerere alikataa kukaa meza moja na Rais Idd Amin Dadah wa Uganda, kwa sababu Amin alikuwa mwuaji. “Siwezi kuchangia meza moja na mwuaji aliyeloa damu” alitamka Rais Nyerere, ulimwengu wote ukamuunga mkono hata mgomo wake uliposababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki! SWALI: Ikiwa Nyerere alikataa kukaa meza moja na dikteta Idd Amin kwavile aliua binadamu takriban 350,000, Jumuiya ya Afrika Mashariki ikavunjika kwa sababu ya kuthamini uhai wa binadamu kuliko vitu vingine vyote, hawa watawala wetu wa leo wa CCM ni binadamu wa jinsi gani, ikiwa wanaweza kulikumbatia na kulipigia debe na hata magoti liuaji la kutisha kama Paul Kagame, lililoua kinyama binadamu zaidi ya 6,000,000 Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Kenya, na kuwapelekea wengine kifo kule kule Ulaya walikokuwa wamekimbizia uhai wao? Watu wa hatari kuliko wote kuhusu amani katika Maziwa Makuu ni hawa madikteta, Paul Kagame na Yoweri Museveni, walioangamiza mamilioni ya raia wa Maziwa Makuu, wakavamia Jamhuri dada za Rwanda na Zaire (DRC) na kuangusha tawala za mataifa hayo huru, na kuipora Congo mpaka dunia nzima inawapigia mayowe kama majambazi ya hatari! Watawala wetu wanakuwa katika akili za namna gani wanapokwenda Kampala na Kigali, na kukaa na Kagame na Museveni na kuzungumzia eti amani katika eneo la Maziwa Makuu, wakati hao ndio wavunjaji makatili wa hiyo amani? Hivi ni kweli akina Kikwete hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu, kiasi cha kuamua kumsaliti jirani mwema aliyevamiwa na kuangamiziwa mamilioni ya raia wake kwa kosa tu la kuwa Wahutu, na kuwasaidia maharamia waliomvamia? Ni aibu kubwa zaidi kwamba watawala wetu waliishia kukubali umamluki, wa kuwasaidia Kagame na Museveni majeshi eti yakawasaidie kuangamizia Wahutu waliopokonywa nchi yao ya Rwanda, na mashujaa wanaopinga udikteta wa damu wa Yoweri Museveni nchini Uganda! Huku ndiko kuhimiza kisasi cha Mwenyezi Mungu juu ya nchi yetu!KAGAME NA MUSEVENI - HATARI SANA KWA TAIFA LETU!
Kwanza kabisa, Wanyarwanda hawatasahaulika walivyotikisa Mkoa wa Kagera walipoingia kule kwa uharamia wa kutumia silaha, wakajulikana kwa ufupisho kama Wanyaru. Wanyarwanda waliteka magari, walipora fedha na mali zingine za wananchi, na zaidi waliteka ng’ombe za wananchi na kuzikimbizia Uganda, ambako walizibadilisha na kuleta nchini wale ng’ombe wa kwao, ambao wako tofauti na wetu kimaumbile. Huu ni ujanja wa kawaida wa kijambazi. Uharamia wa Wanyarwanda ulishamiri mno mkoani Kagera, hapo Buligi pakawa kama makao yao makuu ya kutisha, ndiyo maana palipewa jina la Kosovo. Pori lote mpaka Kyamyorwa lilikuwa halipitiki kwa sababu ya hatari ya Wanyaru., ambao walikuja kutokomezwa na ulinzi wa jadi wa Wasukuma na ushirikiano wa dhati wa Kamanda mzalendo wa Polisi, Inspekta Samson ambaye hivi sasa yuko Wilayani Chato Mkoa wa Geita. Kutokana na umahiri wa Wasukuma katika kupambana na uharamia kwa ulinzi wao wa jadi au Sungusungu, Mheshimiwa Wilson Masilingi akiwa Waziri katika Ofisi ya Rais na Mbunge wa Muleba Kusini, alipopita mikoa ya Ukanda wa Ziwa aliwahamasisha Wasukuma kwamba wahamie maeneo ya Kyamyorwa na Kasindaga na kwingine mkoani Kagera, na kwamba wapewe na mashamba kwa sababu ni kweli kwamba Wasukuma kwa asili ni wazalishaji hodari. Wasukuma waliitika mwito huo na kuhamia huko, na ni kweli kwamba waligeuza eneo lile kuwa kitovu cha uzalishaji usio kawaida wa mazao ya mpunga, mahindi, dengu, mtama, ulezi, serena na mengine mengi, mbali ya ufugaji wao. Baadaye Wasukuma hao walihamishiwa Buligi kutoka hapo Kyamyorwa, kwa maombi ya Waziri wa sasa wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, kwa msingi kwamba eneo hilo ni la kampuni ya Itente ambayo yeye ni mhusika. Profesa Anna Tibaijuka aliandika hata katika kitabu chake cha kampeni yake ya Ubunge wa Muleba Kusini, kuwa Wasukuma wengi walikuwa wamepewa eneo la Kyamyorwa kwa makosa, kwavile eneo hilo lilikuwa la Kampuni hiyo. Waziri Anna Tibaijuka anakiri kwamba aliwaombea Wasukuma Serikalini wakapewa uhamisho kwenda Buligi, na kwamba yeye mwenyewe aliwasaidia hata usafiri wa kuhamia Buligi. Wazalishaji wa Kisukuma waliongezeka huko Buligi, baada ya ndugu zao waliokuwa wamewaacha nyuma kuvutiwa na ushuhuda mwema wa uzalishaji wa wenzao waliotangulia huko, baada ya mageuzi ya eneo lililokuwa ‘Kosovo’ kuwa paradiso ya amani na maendeleo. Ni kweli kwamba Wasukuma walipofika uhamishoni Buligi, kwa uhodari wao katika uzalishaji na umahiri wao katika ulinzi wao wa jadi, waliigeuza ‘Kosovo’, ikawa kihenge cha chakula cha Mkoa wa Kagera, wakizalisha mpunga, mahindi, maharagwe, dengu, mtama, ngano, uwele, mihogo, migomba, viazi ulaya, vitunguu, nyanya, mboga na hata miti kwa ajili ya hifadhi ya mazingira, kwa kadri walivyoshauriwa kitaalamu. KWAHIYO ukweli hauwezi kukwepeka kwamba : 1. Uchomaji wa nyumba zaidi ya 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma katika maeneo ya Buligi na mengineyo kwa kisingizio cha ‘Operation Okoa Mazingira’ ulilenga kuwaangamiza Wasukuma pamoja na mazao yao tele waliyokuwa nayo majumbani mwao pamoja na mali zao zingine zote. 2. Huko Buligi na maeneo mengine ambako Wasukuma wanazalisha kwa wingi mazao hayo yote, Wasukuma waliletwa na Serikali, si wavamizi. 3. Wasukuma hawakuvamia mapori ya Wanyarwanda au ya mtu mwingine yeyote. Kwani Vijiji vyote wanavyoishi vinawatambua, hata kwa mchango wao mkubwa sana katika uzalishaji. 4. Wasukuma hawajaingia katika Hifadhi ya Taifa, wala hawana ng’ombe hata mmoja katika Hifadhi, bali Wanyarwanda ndio wenye mamia ya maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi, ambamo hata wanyamapori wetu Wanyarwanda wamewamaliza. Wanyarwanda huhonga mamilioni ya fedha na ng’ombe kwa maafisa wa wanyamapori na watumishi wengine wa umma. 5. “Operation Okoa Mazingira” haikulenga wahamiaji haramu ambao ni Wanyarwanda, wala mamia ya maelfu ya ng’ombe zao kutoka Rwanda na Uganda hususan katika Hifadhi ya Taifa, kwa sabau Wanyarwanda hawakuguswa kabisa, bali walikuwa wakishangilia wanavyofanyiwa unyama Wasukuma, ambao wala hawana ng’ombe katika Hifadhi kunakoharibiwa mazingira! 6. Nyumba za Wasukuma zilizoteketezwa hazikuwa katika Hifadhi, bali katika vijiji na vitongoji rasmi vyenye serikali halali za Vijiji na Vitongoji. Mfano ni nyumba 105 za Kishonga B Barabara ya 9, katika Kijiji cha Nyamilanda Kitongoji cha Nyakabingo, na Kijiji cha Itunzi Kitongoji cha Miziro. Wenyeviti wa Vijiji vya Nyamilanda na Itunzi ni mashahidi, na wanalalamikia unyama wa kuchomewa nyumba wananchi wao. 7. Uteketezaji wa nyumba za Wasukuma uliambatana na unyang’anyi wa pesa zao, kuanzia shs 100,000/- hadi shs 4,000,000/- kwa Msukuma mmoja, na kuwapa stakabadhi feki zilizoandikwa “WAZABUNI WA MASOKO/ MIALO/VIVUKO. Eti ADHABU kwa ajili ya hatia zilizobuniwa zikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira, kufyeka misitu ovyo, zingine ziliandikwa ‘Kusafirisha mifugo bila kibali’ Tunaambatanisha vivuli vya stakabadhi feki zilizotumika (Nambari 135559, 135519, 135562, 135356, 135520,135367). Tena walipora mapesa mengi sana kuliko waliyoandika katika stakabadhi, na walio wengi hawakepewa hizo karatasi! Huu ni unyang’anyi na ujambazi wa wazi kabisa! Tunawaachia kazi DCI na Takukuru. 8. Maelfu ya wananchi waliofanyiwa unyama huu walilundikana makanisani, kwa ndugu zao na marafiki zao, na wengi walilazimika kuishi maporini, ambako wanawake wapatao watatu walijifungua kama wanyamapori. 9. Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lemberis Kipuyo, ambaye alikuwa ameonwa na Mnyarwanda aitwaye Athanas Habamungu Kafurama, na kibaraka wa Wanyarwanda ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana aitwaye Julius Rwechungura, baada ya kuchangwa shilingi milioni 100 katika kikao cha Wanyarwanda katika kanisa lao la Butera tareke 31/10/2012, kulingana na majigambo ya Wanyarwanda na Kafurama mwenyewe, ndiye aliyeonekana kusimamia unyama huo, ingawa yeye ndiye mwangalizi wa amani na usalama katika Wilaya! 10. Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu unyama huu wa kutisha, alikiri kwamba wamechoma moto nyumba eti zilizokuwa katika Hifadhi, eti kwa ajili ya kulinda mazingira ya Mkoa wa Kagera na kuhamisha wahamiaji haramu wanaoingia na makundi makubwa ya ng’ombe katika Hifadhi. 11. Kama alivyoeleza Lemberis Kipuyo, unyama huo wa kutisha uliosukwa na Wanyarwanda na kutekelezwa kwa usimamizi wake yeye mwenyewe Mkuu wa Wilaya, ulianza tarehe 3/11/2012 saa 3 asubuhi katika eneo la Buligi. Na kama alivyosema hata yeye Mkuu wa Wilaya, maharamia waliowafanyia wananchi wa kabila la Wasukuma unyama huu ni: Askari wa Jeshi la Polisi Usalama wa Taifa Takukuru Wafanyakazi wa Idara ya Misitu Wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Wanyamapori, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Jeshi la Ulinzi, waliotambulika kwa sare zao. Maharamia waliovaa sare za Mgambo. Lemberis Kipuyo alisema walikuwemo pia Wanasheria katika unyama huu. 12. Wananchi waathirika walipokusanyika Kituo cha Polisi Miziro, Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alifika hapo. Lakini alipoombwa afike ajionee makazi ya wananchi wake yalivyoteketezwa, aliwapuuza isivyo kawaida hata kibinadamu, ingawa umbali haufiki hata kilometa! 13. Kwa kuhofia makusanyiko ya vilio vya Wasukuma, jasusi Mnyarwanda Athanas Kafurama alikwenda kumchochea Mkuu wa Wilaya azidishe unyama kwa madai kwamba eti Wasukuma wamejiandaa kuvamia Kituo cha Polisi Miziro. Ndipo unyama ulipozidishwa maradufu kuwaangamiza Wasukuma, na kuwawinda wale wote wanaoogopwa kama waelewa, na wengi ikawabidi kukimbilia maporini na kuishi huko kama wanyamapori licha ya mvua nzito.UHARAMIA ULIOFANYWA NA WANYARWANDA BULIGI
WANYARWANDA WALIVYOIPINDUA OPRESHENI DHIDI YAOWanyarwanda walipoijua ‘Opresheni Okoa Mazingira’ kwamba imeandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwatokomeza wahamiaji haramu yaani wao, na kwavile waliwashika mkononi viongozi wote kuanzia Mkuu wa Wilaya kama walivyokuwa wanajigamba, na kama walivyokuwa wanajihami kwa rushwa kwa uharamia wao wote wanaoifanyia Nchi yetu, ndivyo walivyojipanga kuwatoa kafara Wasukuma Serikali yetu ilikuwa na taarifa zote za mikakati ya dikteta Kagame na Museveni juu ya Nchi yetu, yaani uvamizi wenye lengo la kuiteka ardhi yetu kama vile wanavyofanya Congo Mashariki, uporaji wa raslimali zetu, na walivyohamishia mamia ya maelfu ya ng’ombe zao katika Hifadhi za Taifa letu na utekaji wa ardhi ya wananchi, na hata kulisha mifugo yao katika mazao ya wananchi, wakitetewa na vibaraka wao ambao ni viongozi wetu wala rushwa. Wamiliki halisi wa haya mamia ya maelfu ya ng’ombe ni marais na mawaziri wa Rwanda na Uganda, ambao wanayo mahusiano ya kifisadi na viongozi wetu mafisadi au Watusi kama wao. Ndiyo maana azma ya Serikali yetu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ imekuwa ikipozwa kwa ufisadi kwa muda mrefu, huku maadui wakizidi kujichimbia na kuangamiza mazingira. Lakini kwa nguvu ya wale viongozi wetu waliobaki na uzalendo, Serikali yetu ilikazana na mpango kabambe wa OPERATION ‘OKOA MAZINGIRA’, kwa ajili ya kutokomeza kabisa uvamizi wa Watusi katika Nchi yetu (wahamiaji haramu), na kutowesha ng’ombe zote zilizoingizwa katika Nchi yetu, zenye kuhatarisha uhai wa vizazi vyetu vijavyo kwa kuharibu vibaya sana mazingira. Kilio cha wananchi juu ya uvamizi wa ardhi yetu na kuingizwa maelfu ya ng’ombe katika Nchi yetu kutoka Rwanda na Uganda kilianza mwaka 2009. Wanyarwandawalipopata taarifa juu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ dhidi yao, walifanya mikutano kadhaa mizito katika kanisa lao la Butera, linaloongozwa na Mtusi wa hatari aitwaye Augens. Tawi la kanisa hilo liko Chanyamisa, Karagwe, ambako pia linatumika kwa mikakati hii ya Kagame. Opresheni Okoa Mazingira iliyokusudiwa kutokomeza wavamizi wa Nchi yetu na maelfu ya mang’ombe yao yanayoharibu mazingira ya Nchi yetu, iligeuzwa na walengwa, Wanyarwanda, kuwa unyama wa kutisha wa kutowesha katika eneo hilo wananchi wa kabila la Wasukuma, na kuwapora mali na ardhi wanayozalishia mavuno yaliyotia fora katika mkoa wa Kagera. Katika kuwatwika Wasukuma dhoruba ya ‘Operation Okoa Mazingira’ ambayo iliwalenga wao, Wanyarwanda walianza kwa kuwachonganisha kirahisi kabisa Wasukuma na ndugu zao Wahaya; Kwavile Mhaya mwenye kulima ekari nne au tano ndiye aliyeonekana kuwa mkulima stadi, lakini Wasukuma wakawa wanalima ekari mpaka 50 mkulima mmoja, Wanyarwanda walitumia kwa ufundi wao kigezo hicho kupandikiza mbegu ya kijicho miongoni mwa Wahaya, ambao wamekuwa wepesi kukabidhi kwa Wanyarwanda ardhi yetu. Hatimaye baadhi ya Wahaya walianza kuwanyoshea kidole Wasukuma kwamba eti wanakamata ardhi kubwa kuliko wao, ingawa mapori hayo yalikuwa yanakaa bure tangu uumbaji mpaka Wasukuma walipoyavamia kwa uzalishaji wa nguvu, hata wakawa wakivuna magunia ya mpunga mpaka 700 mkulima mmoja. Kwa hila za Wanyarwanda, Wahaya wa Muleba na sehemu zingine zilizofanyiwa kazi ya ufitini na Watusi, walianza kujikusanya vikundi vikundi kuandika barua za kuomba ardhi hiyo wanayozalishia Wasukuma, ili mashamba ya Wasukuma yamegwe na kupewa wao, kusudi Wanyarwanda wajipatie kutoka mikononi mwa Wahaya, ambao Watusi wanawachukulia kuwa wepesi zaidi wa kuwapasia wao. Kwa kuwatumia vibaraka wao kama Julius Rwechungura ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, Wanyarwanda siyo tu wameteka mamia ya ekari za ardhi yetu, bali wamekuwa wanapiga vita siku zote ya kuwafukuza Wasukuma ili wakamate wao maeneo yote. Uharamia huu ndio uliopelekea Mkurugenzi wa Wilaya kumwamuru Afisa Mtendaji Kata ya Kyebitembe kuitisha mkutano wa tarehe 27/3/2012 kuhusu malalamiko ya Wasukuma dhidi ya Wanyarwanda. Mkutano huo ulipiga marufuku kumega ardhi yoyote inayotumiwa na wananchi wa kabila la Wasukuma, kwa ajili ya mapinduzi ya uzalishaji waliyofanikisha katika mkoa, walioingia katika maeneo hayo tangu mwaka 2007 hadi 2011. Mkutano uliamuru pia kufutwa mashitaka ya kihaini yaliyofunguliwa na kibaraka wa Wanyarwanda Julius Rwechungura, akitaka Wasukuma wanyang’anywe mashamba yao ili wapewe Wanyarwanda. Kisha Wanyarwanda walifanya kikao muhimu tarehe 31/10/2012 katika kanisa hilo la Butera, chini ya uongozi wa Jasusi la Kagame liitwalo Innocent Mchunku Kapilipili. Agenda kuu ilikuwa kuchangisha shilingi milioni mia moja kwa ajili ya kujihami nahiyoOpreshenidhidi yao, kwa kuwanunua viongozi wote wa hiyo opresheni. Taarifa za uchunguzi wetu ni kwamba kweli mapesa hayo yalichangwa na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo na timu yake iliyoendesha unyama wa kutisha dhidi ya Wasukuma, badala ya wahamiaji haramu. Uchunguzi umethibitisha kuwa Mnyarwanda Innocent Mchunku Kapilipilialikuwa jambazi, katika lile genge la hatari la maharamia kutoka Rwanda waliojulikana kama “Wanyaru” chini ya kamanda wao aliyeitwa ‘Kamanda Dogo’. Mnyaru huyu ameteka zaidi ya ekari 400 za ardhi yetu katika Kijiji cha Nyamilanda, Kitongoji cha Nyakabingo, na Kijiji cha Kisana Kitongoji cha Butera. Mtusi huyu anamiliki zaidi ya ng’ombe 500. Mnyarwanda mwingine muhimu katika kikao cha kanisani Butera ni Francis Magege, ambaye amekamata ekari zaidi ya 400 katika Kijiji cha Nyamilanda, Kitongoji cha Nyakabingo. Kikao hicho kilishirikisha pia Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisana, msaliti aitwaye Johanson Shumuni, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, msaliti aitwaye Julius Rwechungura, na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyamtundu Abdon Krophas. Msaliti Johanson Shumuni ametoka katika kifungo cha nje cha mwaka mmoja, kwa kosa la kung’oa mazao ya mwananchi wa Kijiji cha Nyamilanda, kusudi Wanyarwanda wapitishe ng’ombe zao. Kibaraka huyu wa Wanyarwanda alilipishwa pia fidia ya shilingi 70,000/- kwa ajili ya mazao ya wananchi. Wasaliti Johanson Shumuni, Julius Rwechungura na Abdon Krophas kwa pamoja wana kashfa ya kukitapeli Kikotongoji cha Butera msitu wa asili wa mitundu, wakivunga kwamba ni ‘Hifadhi ya Kijiji’ lakini wakawa wanapasua wao mbao na kuzitoroshea nje ya nchi, mpaka moja ya malori ya mbao hizo lilipokamatwa mwaloni Katunguru na kifikishwa Polisi Muleba, mwezi Mei 2010. Lakini watuhumiwa hawajawahi kufikishwa mahakamani mpaka leo, Vibaraka hawa wa Wanyarwanda ndio wahusika wakuu katika kuwauzia ardhi yetu wahamiaji haramu. Mhusika mwingine katika uuzaji wa ardhi kwa Wanyarwanda ni Diwani wa Kata ya Karambi, Ngote, aitwaye Hamudi Abdalla, ambaye hivi sasa anamiliki zaidi ya ng’ombe mia mbili (200) kutokana na rushwa ya Wanyarwanda. Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, msaliti Julius Rwechungura alidiriki hata kuwafungulia mashitaka mahakamani wananchi wa kabila la Wasukuma, kwamba eti wamevamia ardhi ya machungio ya Wanyarwanda! Kisha aliwawekea dhamana yeye mwenyewe na kuwatoza shilingi 10,000/- kila mmoja. Lakini kibaraka huyo alilazimishwa na kikao cha tarehe 27/3/2012 kilichoamriwa na Mkurugenzi wa Wilaya kufuta kesi hiyo, kwa sababu haiwezi kuwepo ardhi ya Wanyarwanda ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Tanzania!(Kwa kuwageuzia kibao hicho Wasukuma)
Kwanza kabisa turejee mapokeo ya ile imani chafu sana ya Watusi, kwamba wao wana utu wa hali ya juu zaidi (superior race) kuliko Wabantu. Unyama wa Wanyarwanda ni pamoja na kuwateka nyara raia wetu, na kuwatumia kama watumwa wa kuswaga mifugo yetu waliyotupora. Mateka hawa huvuliwa nguo na kuvikwa vipande vya matambara vya kitumwa, na kubadilishwa majina. Mfano ni vijana wetu Opecatus Filipo wa Nsheshe, Kijiji cha Nyamilanda, Kata ya Kyebitembe ambaye aligeuzwa jina na kuitwa Peter, na Antelius wa Kabanga Kijiji cha Kasharara, Kata ya Karambi, aliyegeuzwa jina na kuitwa Rutashambya. Wanyarwanda waliishi porini na hawa ‘watumwa’ kwa miaka miwili. Mmoja wao hatimaye alifanikiwa kuwatoroka, akatoa taarifa Kituo cha Polisi Kyebitembe, ambapo Mkuu wa Kituo hicho shujaa Inspekta Samson alifuatilia kwa uhodari mpaka akafanikiwa kumwokoa yule kijana wetu wa pili. Wale watekaji walikimbia msako huo baada ya kutonywa na msaliti Afisa Mtendaji wa Rwabera, Karagwe, mwanamke aitwaye Alfredina. Raia wetu hao waliokombolewa wana ushuhuda wa kutisha wa unyama uliokuwa ukifanywa na Wanyarwanda. Wanaeleza njia za porini walizokuwa wakipitishia mifugo yetu, mawasiliano ya Wanyarwanda kwa redio na simu dhidi ya mipango yote ya serikali yetu ya kuwafuatilia na mifugo yetu waliyopora. Vijana wanaeleza jinsi walivyotumika kuficha hayo makundi ya ng’ombe zetu, na jinsi walivyoishi kama wanyamapori katika mvua kali na jua na mateso mengi yasiyosemeka. Vijana hawa wanashuhudia jinsi Wanyarwanda walivyomchoma raia wetu kwa upanga wa moto mwilini, kwa kuthubutu kudai ujira wa kutumiwa kikatili kutorosha ng’ombe waliopora katika nchi yetu mpaka huko maporini. Vijana wanashuhudia jinsi wenzao walivyouawa na Wanyarwanda kama wanyama. Zaidi ya yote, anaalaniwa vikali msaliti Johanson Shumuni ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kisana, kwa kumfichia siri mwuaji katili wa Kinyarwanda, ‘Mchungaji’ Augens mwenye hilo kanisa la Butera, alipomwua kinyama mfanyakazi wake aliyekuwa anasimamia boti yake iliyokuwa ikifanya kazi za magendo katika Ziwa Buligi, baada ya kumtuhumu kwa wizi wa injini ya hilo boti lake. Shahidi mmojawapo wa mauaji haya ni Benedicto Damian ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji hicho cha Butera. ‘Mchungaji’ hatari Augens pia anashughulika na uvuvi haramu wa kutumia makokoro, unaoangamiza mpaka mbegu ya samaki kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo, Mtusi mwingine aliyeua kinyama raia wetu ni Mchungaji wa kanisa la Mnyarwanda Francis Magege. Huyu alimwua aliyekuwa mchungaji wa ng’ombe zake, baada ya siku tatu akaenda kutoa taarifa ya uongo Polisi kwamba marehemu ameuawa na nyoka. Baada ya kugundulika mwili wa huyo marehemu machakani na kuchunguzwa na Dr. Mtumbi, iliripotiwa kwamba aliuawa kikatili sana kwa kitu kizito chenye ncha kali. NdipoMnyarwanda huyo ‘Mchungaji’ aligeuza kibao na kusema marehemu ameuawa na Msukuma eti aliyekuwa amegombana naye kwa sababu ya kulisha ng’ombe mazao yake. Lakini uchunguzi unaonyesha kuwa marehemu aliuawa baada ya kudaiana na huyo mwajiri wake ‘Mchungaji’. Mashahidi muhimu ni pamoja na huyo Daktari aliyefanya uchunguzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butera, na kijana aliyekuwa anachunga pamoja na marehemu, ambaye alikimbilia Ngara. KWAHIYO kwa ajili ya usalama wa Nchi yetu, na heshima na Uhuru wa kweli wa Taifa letu, na sifa ya Taifa letu ya kupigania HAKI na utu wa mwanadamu, tunasisitiza kwamba: 1. Watu wote waliohusika na unyama wa kutisha dhidi ya wananchi wa kabila la Wasukuma Mkoani Kagera, pamoja na Wanyarwanda wote waliohusika na unyama huu wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria. Watuhumiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lemberis Kipuyo . 2. Wananchi wote waliofanyiwa ukatili huu walipwe fidia ya mateso yote na hasara zote walizosababishiwa na unyama huu. 3. Mamia ya maelfu ya ng’ombe zilizoingizwa nchini mwetu kutoka Uganda na Rwanda zikamatwe na kupigwa mnada, ili fedha hiyo itumike kuboresha Hifadhi zetu na mazingira ya Nchi yetu.USHAHIDI WA UKATILI WA WANYARWANDA KWA RAIA WETU
4. Taifa letu lisimame kinyume kabisa na uharamia wa kuvamia Nchi yoyote huru duniani, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa Jamhuri ya Rwanda na uvamizi na uporaji wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, uliofanywa na Watusi wa RPF na Uganda. 5. Taifa letu lilaani imani chafu ya Watusi (apartheid nyeusi) kwamba wenzao eti waliumbwa kuwa watumwa wao, hivyo kudai usawa wa kibinadamu eti ni uasi wa kuangamizwa kama wanavyofanywa Wahutu. 6. Taifa letu liusaidie ulimwengu kujua ukweli kwamba Watusi ndio walioendesha genocide ya kutisha duniani, kwa kuangamiza Wahutu zaidi ya 6,000,000, zaidi ni mauaji yaliyofanywa na dikteta Paul Kagame wa Rwanda, ambaye ndiye mtuhumiwa Mkuu wa genocide ya Maziwa Makuu. 7. Taifa letu lihakikishe pia kwamba mwuaji Paul Kagame na wenzake wote wanafikishwa mbele ya Sheria kujibu mashitaka ya genocide. 8. Taifa letu lifanye TOBA kwa mwenyezi Mungu kwa kudhamini unyama wote uliofanywa na Watusi, ukiwa ni pamoja na mauaji ya marais watatu wa Kihutu wa mataifa ya Rwanda na Burundi, marehemu Rais Melchior Ndadaye, marehemu Rais Juvenal Habyarimana na marehemu Rais Cyprien Ntaryamira. 9. Taifa letu lifanye TOBA kwa kuikaribisha ICTR Arusha, na kuifukuza katika Nchi yetu mara moja, kwa sababu siyo siri kwamba ICTR ni nyenzo ya kusaidia genocide ya dikteta Paul Kagame ya kuwamaliza Wahutu.KUHUSU GENOCIDE MAZIWA MAKUU
10. Taifa letu lipige vita ukatili wa kuendelea kuwashikilia kifungoni Wahutu waliotamkwa na hiyo ICTR kwamba hawana hatia, na kuwatetea kwamba walipwe fidia kwa unyama wote waliotendewa na Kagame pamoja na ICTR na/au UNO. 11. Taifa letu lihakikishe kuwa Rwanda, Burundi na Uganda zinafutwa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa sababu sharti kuu la uanachama ni Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala wa Sheria, lakini hizi ni tawala za Udikteta wa kikatili na Umwagaji damu. 12. Taifa letu lihakikishe kwamba Dikteta Paul Kagame anamwachia huru mara moja mwanamke mpinzani wake, shujaa Victoire Ingabire, ili akakataliwe na wananchi wenyewe wa Rwanda au wampe uongozi kama wanaona atawafaa. Kutoona haya mbele ya dunia kwa unyama huu, kunadhihirisha Kagame kuwa si binadamu wa kawaida!
Liberty International Foundation
Reverend Christopher Mtikila
(0766 053081, 0713 435016 )
EXECUTIVE CHAIRMAN
Last edited by KING COBRA; 2
Barrick Gold Ends Chinese Talks to Sell African Unit
By Liezel Hill & Thomas Biesheuvel - Jan 9, 2013 12:47 AM GMT+0300
Barrick Gold Corp. (ABX),
the biggest producer of the precious metal, ended talks over the sale
of its 1.44 billion-pound ($2.32 billion) African unit to China National
Gold Group Corp. without reaching an agreement.
Barrick still sees “a lot of value” in the assets held by its African Barrick Gold Plc (ABG)
subsidiary, Toronto-based Barrick’s Chief Executive Officer Jamie
Sokalsky said yesterday in a phone interview. Shares of African Barrick
fell 21 percent in London yesterday.
African
Barrick “does have some opportunities to enhance that value, and when
we looked at that versus ultimately what China National Gold was talking
about, it just wasn’t the right fit,” Sokalsky said. “We would have
liked to have done this transaction, but it wasn’t about doing this at
any cost.”
Sokalsky
declined to comment on the specific issues that led to the end of the
talks. Discussions had stalled because of differences over taxes and
legacy issues, Chinese newspaper 21st Century Business Herald reported
yesterday, citing CNG Chairman Sun Zhaoxue.
The
deal would have been the largest gold-company takeover involving a
Chinese company, according to data compiled by Bloomberg. Barrick said
in August that CNG was in preliminary discussions about buying African
Barrick Gold, which would have given the state-owned Chinese company
four mines in Tanzania.
“This
is a big asset, it’s a significant transaction for anyone, it’s a
public company and ultimately over time multiple things came into the
equation,” Sokalsky said. “It just didn’t make sense for both of us to
transact, to ultimately complete a transaction.”
Rising Costs
Wu Zhanming, the vice president of CNG’s overseas investment unit, didn’t answer calls to his mobile phone.
African
Barrick slumped to 352.1 pence at the close in London yesterday, the
steepest decline since the shares were first sold in 2010. Barrick fell 1.3 percent to C$33.14 in Toronto.
Sokalsky,
who replaced Aaron Regent as CEO in June, is reviewing Barrick’s assets
in an effort to improve returns and cash flow as costs rise. The
company has received approaches from companies interested in some of its
other assets, he said yesterday.
“If
there are opportunities to divest assets that are worth more to someone
else than us, we will absolutely take a look at that,” Sokalsky said.
Barrick doesn’t “have anything to talk about at the moment.”
Illegal Miners
While
Barrick will consider new approaches for African Barrick if it gets
them, the company won’t actively solicit third parties for a sale of the
business, Sokalsky said.
Since
being spun off by Barrick, African Barrick has struggled to meet
production targets amid operational setbacks and disruption caused by
illegal miners. Selling African Barrick would have lowered Barrick’s
production costs, Brian Yu, an analyst at Citigroup Inc. in San Francisco, said in an Aug. 16 note.
In
October, African Barrick raised its 2013 forecast for average costs to
$900 to $950 per ounce of gold from a July projection of $790 to $860.
Barrick
“will continue to look for ways to realize value from the block,” Numis
Securities Ltd. in London said in a note to investors. “However, the
news will come as a disappointment to some who saw it as a potential
exit from this under- performing stock.”
Fewer Deals
Acquisitions
in the gold industry have declined as slowing global growth tightened
available credit. There were 175 completed deals worth $6.8 billion in
2012, the lowest in at least five years, according to data compiled by
Bloomberg.
There are probably other companies interested in buying African Barrick, said David West, a Vancouver-based analyst at Salman Partners Inc. He didn’t name potential buyers.
“I
wouldn’t be surprised to see another offshore entity maybe take a run
at it,” West said in a telephone interview. “This stuff goes on all the
time. I’m sure there are a lot more misses in terms of M&A activity
than hits and this is just one of those misses.”
To contact the reporters on this story: Liezel Hill in Toronto at lhill30@bloomberg.net; Thomas Biesheuvel in London at tbiesheuvel@bloomberg.net
To contact the editors responsible for this story: Simon Casey at scasey4@bloomberg.net; John Viljoen at jviljoen@bloomberg.net
SOURCE: BLOOMBERG
Wednesday, January 9, 2013
MAMBO YAZIDI KUIBUKA MAUAJI YA POLISI KARAGWE
Taarifa
za kuuawa kwa askari polisi wawili zimezidi kuchukua sura mpya wilayani
Karagwe baada ya wananchi kuanza kutoboa unaodaiwa kuwa ukweli wa tukio
hilo ambao wanadai umefichwa kwa makusudi na badala yake kuwatolea
lawama wananchi.
Ukweli unaoelezwa ni huu: Mtu mmoja (Raymond) wa kijiji cha Rugu (iko wilayani karagwe) alikuwa na
meno ya tembo; aliamua kwenda maeneo ya Benaco (iko wilayani Ngara) kutafuta
wanunuzi wa Meno ya Tembo na huko aliwapata watu wawili (Abubakari na Geofrey).
Baada ya makubaliano ya kulipwa shs 12 milioni wale wanunuzi
walimweleza kuwa kwa kuwa watakwenda usiku na njiani kuna pori la Kimisi
watakwenda na mtu wao mwenye bunduki ambaye huwa anawalinda mara kwa mara.
Walipofika Rugu wakauona mzigo, wakaupima na kukuta kilo walizokubaliana ndivyo
zilivyo.
Mzigo ulipakiwa kwenye gari lao; jamaa hao wakataka kuondoka
bila kulipa. Mwenye mali alipouliza mbona hawampi hela yake alijibiwa kuwa
'sisi ni polisi na haya meno ya tembo ni nyara za serilkali, ukileta fujo
tutakukamata!'
Kwa kuwa walikuwa na bunduki jamaa aliogopa lakini
alijitahidi kupambana na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo. Gari
lilipoondoka na mzigo jamaa akapiga simu kwa watu walio kwenye stesheni ndogo
ambayo ilikuwa lazima gari hilo lipitie akiwaeleza kuwa wamevamiwa na majambazi
lakini wamepambana nao na kupasua kioo cha gari, hivyo wajitahidi kulizuia
lisipite.
Raia hao walipanga mawe makubwa barabarani na mara gari hilo
likaja - kioo kimepasuliwa na halina namba. Gari liliposimama raia wakaanza
kuwahoji wanakotoka na wanakokwenda na walifuata nini.
Ikabidi kichapo kitembee kidogo. Jamaa kuona kichapo kinazidi
ikabidi waseme kuwa wao no polisi na kuna mhalifu walikuwa wamnamfuatilia.
Lakini raia wakaona hao polisi mbona hawawahamu?
Raia waliamua kupiga simu kwa OCS wa kituo cha karibu
(Chanyamisa) akawajibu kuwa hana taarifa zozote na watu hao; wakapiga simu
kituo cha Omukaliro, OCS akawajibu kuwa hana taarifa;. Walipiga simu polisi
wilayani lakini jibu likiuwa ni hilohilo!
Hao Polisi -majambazi kuona hivyo yule aliyekuwa na bunduki
akafyatua risasi hewani raia hawakuogopa wakataka wamkamate, akapiga risasi
nyingine ikampiga kijana mmoja kwenye mkono!. Hapo ndipo raia waliona kuwa
kumbe hawa tukiwalegezea watatuua. Kichapo kikaendelea lakini aliyekuwa na
bunduki alikimbia baada ya kufyatua risasi nyingine. Hao wawili waliobaki
walipigwa hadi kufa!
Raia waliamua kulitia gari moto, wakati likiendelea kuuungua
walifungua kwenye boot na kukuta meno ya tembo baadhi yakiwa yameanza kuungua
kidogo.
Huo ndio unaelezwa kama ukweli baada ya TBC kutangaza wakimkariri
msemaji wa jeshi la Polisi kuwa hao polisi walikuwa wanataka kumkamata mhalifu
na raia wakawaua ili wasimkamate, raia wamechukizwa sana uongo huo.
Ukweli huu umetobolewa na wananchi katika kipindi cha Radio Jana
majira ya saa 3 hadi saa 4:30 Usiku na kituo cha Radio ya kijamii (Radio Fadeco)
iliyoendesha kipindi kwa kuruhusu wananchi kupiga simu kueleza nani alaumiwe
kwa mauaji ya hao polisi?
Hongera walevi kuzaliana na kuzalishana
Mpayukaji wa Msemahovyo
KWA mujibu wa taarifa iliyosomwa na profesa, daktari, shehe,
gwiji, alhaji, kanali, father Njaa Kaya Kiwewe ni kwamba walevi kwenye kaya hii
wamezaliana na kuongezeka sana. Hili ni jambo la kujivunia.
Ni ushahidi kuwa sera ambazo baadhi ya fyatu huziita usanii
na uchakachuaji zimefanikiwa. Kila mtu anamchakachua mwenzake na kuzalisha
vitegemezi iwe halali au haramu. Unakumbuka yale matokeo ya kipimo cha vinasaba
cha DNA?
Kwa wasiojua maana ya DNA ni Deoxyribo-Nucleic Acid. Kipimo
hiki kilionesha kuwa katika ndoa na ndoana watoto wanaozaliwa asilimia zaidi ya
40 ni wa kuchakachua.
Mama anamchakachua baba na baba anachakachua nje sawa na
watawala wanavyochakachua sera. Usishangae siku moja ukiambiwa kuwa kaya yenu
ni kaya ya uchakachuaji.
Chakachua ngoma ya zama zile. Leo si ngoma bali mfumo ambapo
kila kitu kinachakachukuliwa kuanzia kura, elimu, afya hata familia! Mwe!
Msipojifunza na kujirudi mwesha mie simo bahati nzuri.
Kutokana na kuwa na shahada ya juu yaani PhD in Demography
and Chakuazation, leo nataka nifanye uchambuzi wa kina (deep and critical
analysis) juu ya ni kwanini walevi wamezaana na kuongezeka sana. Kuna sababu za
kisayansi ambazo nimezibaini ambazo zimesababisha kuongezeka kwa walevi.
Mosi, mgawo wa umeme. Utafiti uliofanywa na mtaalamu bingwa
na baba ya uchakachuaji unaoshuhudia aitwaye Profesa Alhaj Ally Hossein Mwinyi
ni kwamba watu wanazaliana sana kwenye giza kuliko kwenye mwanga.
Hii inatokana na ukweli kuwa wakati wa mgawo wa umeme watu
hukosa mambo muhimu ya kufanya au fursa ya kujishughulisha kama vile kusoma,
kuangalia taarifa za habari hata kuonekana.
Hivyo, wahusika hujikuta wakiwa na msongo wa mawazo na sononi
kiasi cha kujiburudisha kwa kula tunda lile. Hata kama huwa wahusika hawana nia
au hamu ya kula tunda, mazingira ya kiza huwalazimisha kufanya hivyo.
Umenielewa? Najua wengine watauliza tunda gani. Ni tunda lililo katikati ya
miiba. Kama ni nanasi au ‘whatever please ask me not.’
Sitaki uniulize miswali mingi hadi nikujibu kipuuzi kama Dk
Dugong bin Manatee Ben Willy Makapa aliyewahi kuwatolea watu uvivu kuwa wana
uvivu wa kufikiri asijue naye alikuwa nao hadi akaingizwa majaribuni na
Delillah wake akajimegea Kiwila. Anyways, tuyaache hayo si mwake humu leo
ingawa ujumbe umetua, msg sent au siyo?
Mbali na kuongeza idadi ya walevi, mgawo wa umeme hukuza
uchumi wa kaya kwa kuagiza na kuingiza jenereta nyingi ambazo huuzwa kwa bei
mbaya. Pia jenereta hizi husaidia kutunza mazingira kwa kutoa mimoshi
inayosaidia majani kuota na kusafisha anga. Najua kuna watakaoniona kama chizi.
Kama mgao wa umeme hauzalishi majenereta ambayo ni salama kwa mazingira chizi
ni nani kati yangu na wale wanaosababisha mazingira ya kuwepo madudu haya?
Kutokana na kukua uchumi hasa kwa kutoa ajira kwa
wafanyabiashara wengi wa Kihindi, taifa letu limeweza kuwekeza kwenye huduma
bora za afya ndani na nje. Kwa sasa tuna kile Wazungu huita cutting edge tech
kwenye mahospitali yetu maarufu kama vile Apollo. Hivyo, kuzaana si tatizo.
Huduma za afya zipo kwa wote wenye mshiko na viza ya kwenda India kutibiwa.
Faida nyingine ya mgawo licha ya kuzaliana ni kutoa fursa za
kuweza kuleta makampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ambayo mwisho wa siku
huzalisha dharura ya wizi na kutengeneza pesa nyingi hivyo kuacha baadhi ya
wanene kwenye kaya wakiwa mabilionea. Mara hii mmesahau Richmonduli na Dowans!
Ukosefu wa ajira hivyo kazi inakuwa hiyo hiyo. Usiniulize
hiyo hiyo ipi tafadhali. Ufisadi, watu wanachuma wasipopanda kiasi cha kujiona
matajiri hivyo kuzaliana bila kuogopa chochote wasijue neema yao ni ya muda.
Wakuu wetu kujizalia sana kiasi cha kutufanya tuwaigize. Hebu
waulize wao wana watoto wangapi na mali kiasi gani? Kila mmoja siri yake. Je,
unategemea nini hapa?
Maisha bora kwa wote. Baada ya walevi kungoja maisha bora kwa
wote wasiyaone wameamua kuongezeka ili wale watakaokufa kwa matatizo angalau
waache mbegu nyuma.
Sababu nyingine ya kuongezeka kwa walevi ni matangazo
yanayochochea ngono. Kwa sasa matangazo machafu ndiyo fasheni.
Magazeti ya uchafu yafichwayo kwenye jina la udaku, runinga
zenyewe wendawazimu wanaoitwa watangazaji na matangazo ya kusambaza ukimwi kwa
kisingizio cha kuupinga ndiyo usiseme.
Hili likiunganishwa na sheria kutowashughulikia wanaovunja
maadili ya taifa linafanya hali kuwa mbaya. Hapa hutujagusa wanaowatia mimba
watoto wa shule. Hivi kama dingi anasema wanaopata mimba wakiwa mashuleni ni
matokeo ya kiherehere chao unategemea nini?
Kubariki jinai. Kama halali imegeuzwa haramu na haramu halali
unategemea nini? Kila mtu anaendekeza libeneke akijua kuna siku ataukata kwa
vile kuukata hakuna kizuizi kisheria. Hivyo watu wanajenga kwenye ndoto zao
wakisahau kuwa kuna kubaunzi kwa ndoto na mipango yenyewe.
Ingawa kuzaliana na kuzalishana na kuongezana kwa walevi ni
jambo bora, halikosi kasoro. Baada ya walevi kuona wanaongezeka huku masahibu
yao nayo yakizaliana, wameanza kugombea utajiri. Hamkusikia wale wa kule
Zaainzibaa na Ntwara wakigombea nishati? Hamkuwasikia mawaziri wehu nao
wakichochea kadhia hizi kwa kutoa majibu ya kubabaisha?
Nawakumbuka waishiwa kama vile Billy Mgimwa na Sossy Muongo
wakisia urongo na upupu kuwa walevi wasiwe na wasi wasi kwa vile watawekezwa!
Hakuna aliyenichefua kama Murongo aliyesema eti wamachinga kule Ntwara hawana
sababu ya kudai kufaidi wese kwa vile nao wamekuwa wakifaidi nishati ya
Kihainsi!
Kwani walikuwa wakipewa bure? Mbona kila mlevi anajua magumu
ya kulanguliwa huduma mbovu kuanzia simu, umeme hadi hewa?
Kwa ufupi ni kwamba kama utawala na staili ya kutawala
vitaendelea kuwa hivi hivi, walevi wataongezeka hadi wageuke bomu linalotika.
Wataacha kuwa neema waishie kuwa balaa. Hata hivyo, inatupasa kushangilia
ufanisi huu wa kuzaliana sawa na mabalaa yetu. Nadhani ombaomba wetu wenye suti
wanachekelea kwa vile wamepata sababu ya kwenda kuzurura wakidai wanaomba
njuluku kwa ajili ya walevi huku njuluku zenyewe zikiishia kule Ususio au
Uswisi.
Acha niwahi home kwenda kuzalisha nami! Who cares if at all
what we’ve is but megalomania in the name of polity? Usiniulize tafsiri
Subscribe to:
Posts (Atom)