Search This Blog

Wednesday, August 14, 2013

Ninani aliyeruhusu Ujenzi wa Ghorofa karibu na Ikulu ya Dar es salaam?



JENGO la ghorofa 19 lililojengwa karibu na Ikulu ya Dar es Salaam linadaiwa kuhatarisha maisha ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, UWAZI limefuatilia kwa umakini.
WALINZI WA OBAMA WADAIWA KUWA CHANZO
Kuna habari kwamba, ujio wa  Rais wa Marekani, Barack Obama nchini Tanzania Julai Mosi, mwaka huu ndiyo ulioibua mambo mengi juu ya kuwepo kwa jengo hilo kwani maafisa wake wa usalama walikataza watu kupanda hadi ghorofa ya 19 kwa maelezo kuwa wamegundua ni hatari kwa maisha ya viongozi, hasa Rais Obama aliyekuwa ikulu na Jakaya Kikwete.

Kikosi cha Majasusi wa Marekani (FBI) waliotangulia nchini miezi minne kabla ya ujio wa Obama ndiyo walioishtua serikali kwa kuwaambia watu wa usalama kuwa urefu wa jengo hilo ni hatari kwa ikulu kwa vile maadui wanaweza kulitumia.
FBI WALITEGA MITAMBO YAO JUU YA JENGO
Uchunguzi unaonesha kwamba, kwa vile FBI waliamini usalama wa ikulu ni mdogo kutokana na jengo hilo hivyo walilazimika kuweka mitambo yao juu yake na kuendelea kuwepo hapo kwa saa ishirini na nne kipindi chote cha ziara ya Obama.
FBI WALIONDOA MAGARI CHINI YA JENGO
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya ikulu vililitonya Uwazi kuwa, mbali na FBI kuweka mitambo yao ya kiusalama, pia walilazimika kuondoa magari yote yaliyokuwa yamepaki chini ya jengo hilo na kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuwa makini na ghorofa hilo.  Habari zaidi zinasema FBI hao walipendekeza jengo hilo livunjwe ama liwe la serikali na waishi wana usalama wanaolinda viongozi wa kitaifa.
“Baada ya FBI kutoa taarifa hizo ikulu ndipo ‘mchawi’ alipoanza kutafutwa hadi kufikia hatua ya kukamatwa walioruhusu ujenzi huo,” kilisema chanzo.
Waandishi wetu wamegundua kuwa pamoja na tahadhari iliyotolewa na FBI juu ya jengo hilo, lakini bado shughuli za kila siku zinaendelea sambamba na watu kuishi.

WALIOTOLEWA ‘KAFARA’ NI HAWA
Hivi karibuni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mwandamizi wa Majengo, Richard Maliyaga walipandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya kwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa hilo karibu na ikulu.
Washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo.
Washitakiwa walikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini watatu wafanyakazi wa serikali waliosaini hati ya shilingi milioni 50.
Souce: Global Publishers
http://paparaziblog.blogspot.com/2013/08/maisha-ya-rais-kikwete-yako-hatarini.html?spref=fb   

Thursday, August 8, 2013

India yaikopesha Tanzania magari 675 ya Kijeshi

Jeshi la Wananchi (JWTZ) limepokea magari 675 kutoka India kwa mkopo na mengine bure ambayo yatafanya kazi kusaidia sekta ya afya.
Hafla ya kukabidhiwa magari hayo ilifanyika jana ambapo ilielezwa kwamba magari yote yatagharimu dola 36.56 za Marekani .
Akipokea magari hayo jana Dar es Salaam, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema magari hayo yametolewa kwa mkopo uliosainiwa Januari 26, 2012 kati ya Tanzania na India kupitia Benki ya Exim.
Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani kikicheza ngoma na Msewe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari hayo
“Mpaka sasa tumeshapokea magari 592 na makontena 16 yenye vifaa vya akiba. Magari 88 yaliyobaki tunatarajia kuyapokea Septemba 2013,” alisema Nahodha.
Alisema Serikali ya India imetoa magari manne kama zawadi kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya jeshini na kwa wananchi wa kawaida.”
Nahodha alisema magari hayo yamefika katika wakati mwafaka kwa kuwa yatasaidia kupunguza tatizo la usafiri na kwamba hayatatumika katika shughuli za ndani za kijeshi pekee bali yanatarajiwa kutumika kusomba mahindi katika mikoa mbalimbali nchini.
Alisema mkataba kati ya Tanzania na India ulifikiwa kutokana na uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili ambao ulianza tangu miaka ya 1950 chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Rais Jawaharlal Nehru.
Nay Balozi wa India nchini, Debnath Shaw alisema magari hayo ambayo yametengenezwa na Kampuni ya Ashok Leyland ya India, baadhi yao yatatumika kulinda amani katika nchi ya Democratic Republic of Congo (DRC).
“Magari haya yametengenezwa kustahimili hali ya nchi zinazoendelea…tunatarajia yatatumika kulinda amani DRC,” alisema Shaw.
Akizungumzia ulijo wa magari hayo, Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini, Meja Jenerali Davis Mwamunyange alisema kati ya magari yaliyopokelewa yapo maalumu kwa ajili ya shughuli za kijeshi.
Source:  http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/India-yakopesha-Tanzania-magari-675-ya-Jeshi/-/1597568/1940880/-/9htc9z/-/index.html

Obama aahidi Kenya msaada ukarabati uwanja wa JKIA


Uchunguzi ungali unaendelea kubaini chanzo cha moto huo,Ndege za kimataifa zimeanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Nairobi JKIA, siku moja tu baada ya kitengo cha kuwasili wageni kuchomwa na moto mkubwa.
Ndege ya kwanza ya kimataifa kuwasili katika uwanja huo ni ile iliotoka Uingereza na baadaye nyengine kutoka Tanzania na Bangkok zikawasili.
Wachunguzi hata hivyo wanatafuta mabaki ya moto huo ili kutathmini chanzo chake.
Wakati huo huo Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ataisaidia serikali ya Kenya katika kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya moto mkubwa kuuteketeza hapo jana.
Katika ujumbe wake wa simu, Obama alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuisadia Kenya katika hali ile yoyote kutokana na ushikiano wake na Kenya.
Obama pia aliwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya bomu ya Agosti 1998 mjini Nairobi.
Manmo Jumatano, moto mkubwa uliotokea majira ya asubuhi, uliharibu kitengo cha kuwasilia wageni wa kimataifa.
Vikundi vya wachunguzi viliwasili katika uwanja huo kufanya uchunguzi wao kubaini kilichosababisha moto huo.
Abiria walikwama kutokana na mkasa huo ingawa waliweza kuondolewa nje ya uwanja kwa ajili ya usalama wao huku baadhi wakiangalia mizigo yao ikiteketea wasijue la kufanya. .
Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja huo na kujionea uharibifu uliotokea na kiisha kutoa taarifa yake kupitia kwa msemaji wake Esipisu aliyesema kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa.

Wanawake waingereza washambuliwa Zanzibar kwa Tindikali

Maji ya Tindikali (Acid)
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi yao wanaume hao.
Wanawake hao, wanasemkana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi halo haijulikani.

Wednesday, August 7, 2013

MFANYABIASHARA WA MADINI JIJINI ARUSHA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

Pichani juu askari wakikagua mwili wa  Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa  nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia.

Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.

Uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kujua chanzo cha mauaji yake.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

JOHN CHEYO ALAZWA, RAIS KIKWETE AMTEMBELA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo. (Picha Freddy Maro)

Moto uwanja wa ndege wa Kenya wadhibitiwa

Moto mkubwa katika uwanja mkuu wa ndege jijini Nairobi ambao umeharibu eneo muhimu la kurukia na kutulia ndege na kuilazimisha serikali ya Kenya kuzizuia ndege zote kutua, sasa umedhibitiwa, huku uchunguzi ukiendelea.
Waziri wa Usafiri na Miundombinu, Michael Kamau, anaongoza upelelezi huo. Rais Uhuru Kenyatta na mawaziri kadhaa wamekuwapo kwenye uwanja huo wa ndege tangu mapema asubuhi ya leo (Jumatano, 7 Agosti) , mara tu baada ya taarifa za moto kusambaa.
Moshi mzito na cheche za moto zimeonekana mapema asubuhi kwenye anga la uwanja huo wa ndege, zikitokea kwenye sehemu za kuwasili na kusafiri abiria wa ndege za kimataifa.
Hakuna taarifa za watu waliouawa ama kujeruhiwa hadi sasa, na abiria waliokuwa kwenye ndege ambazo zilikuwa tayari zimeshatua wakati moto huo ulipozuka, walifanikiwa kuondolewa salama.
Maafisa wa serikali wanasema sehemu ya paa la Kitengo Namba 1 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta lilianguka kutokana na moto huo, na kuwapa tabu sana wafanyakazi wa kikosi cha uokozi kupambana na moto huo ulioanza mapema asubuhi.
Abiria wako salama
Mionzi ya moto ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi. Mionzi ya moto ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.
Ndege zote zilizokuwa zituwe kwenye uwanja huo, sasa zimeelekezwa kutua kwenye viwanja vya ndege vya Mombasa na Eldoret, huku mamlaka nchini Kenya zikiwashauri abiria kuwasiliana na mashirika yao ya ndege kutokana na hofu ya kupanguka kwa ratiba za safari zao.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Kenya, Titus Naikuni, amewahakikishia wasafiri kwamba ajali hii ya moto haijaondosha usalama wao.
"Abiria wetu wote wanaoingia na kutoka Kenya wako salama. Kutakuwa na athari kidogo kwenye operesheni zetu na mara tutakapojua kiwango hasa cha madhara kwenye operesheni hizo, tutamueleza kila mtu kile tunachokusudia kukifanya," alisema Naikuni.
Uwanja huo wa ndege jijini Nairobi ni kituo cha watalii wanaotembelea taifa hilo la Afrika ya Mashariki na pia unatumia kama kituo cha kubadilishia ndege za kimataifa kwa wasafiri wanaoelekea maeneo mengine ya Afrika.
Ulikuwa moto mkubwa sana
Mionzi ya moto ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi. Mionzi ya moto ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imesema moto huo ulikuwa "mkubwa sana" na kwamba chanzo chake bado hakijafahamika. Shirika la habari la Ujerumani, dpa, limemnukuu msemaji wa polisi nchini Kenya, David Kimaiyo, akitaka kuwepo kwa utulivu.
"Ninatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu katika wakati ambapo serikali inachunguza sababu ya moto huu. Tayari upepelezi umeanza," ameandika Kimaiyo kupitia akaunti ya Twitter ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Moto huu umetokea katika siku ambayo Kenya inakumbuka mwaka wa 15 tangu mashambulizi ya mabomu kwenye ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.
Mashambulizi kama hayo yalifanyika pia siku na muda huo huo kwenye ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo matukio hayo mawili yaligharimu maisha ya watu 220.
Hadi sasa hakujawa na taarifa zozote za kuihusisha ajali hii ya moto na mashambulizi ya kigaidi.
Mwandishi: Mohammed Khelef/DPA/Reuters