Mwili wa mwandishi mashuhuri wa vitabu barani Afrika Chinua
Achebe umewasili nyumbani kwake katika jimbo la Anambra nchini Nigeria. Mwandishi huyo mashuhuri alifariki mjini Boston,Marekani,
akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Jamaa na maafisa wa serikali walikuwa katika uwanja wa ndege
Kusini mwa Nigeria kumpokea marehemu. Hayati Achebe, anasifika sana kwa kuwa
mwanzilishi wa fasihi ya kiafrika kwa kiingereza.
Kitabu chake alichokianda cha kwanza, mwaka 1958, Things
Fall Apart, ambacho kilizungumzia sana athari za ukoloni barani Afrika, aliweza
kuuza zaidi ya vitabu milioni kumi.
Mwandishi huyo na msomi, aliendelea na uandishi wake na
kuandika vitabu vingine 20 baadhi vikikosoa sana wanasiasa na kile alichokitaja
kama ukosefu wa uongozi nchini Nigeria. Alikuwa anaishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 baada ya
ajali ya barabarani kumjeruhi kiasi cha kumlemaza.
Makundi ya kitamaduni yalifanya tamasha mbali mbali nje ya
uwanja wa ndege wa Enugu, huku ndege iliyokuwa inambeba marehemu Achebe
ilipotua. Inaarifiwa kuwa licha ya kuwa watu wana majonzi tele, lakini
pia wanasherehekea maisha ya mwandishi huyo.
Achebe atazikwa karibu na nyumbani
kwa familia yake mjini Ogidi, mji mdogo kwenye vilima vya jimbo la Anambra. Achebe aliandika sana vitabu vya kukosoa serikali ya Nigeria kwa uongozi duni
No comments:
Post a Comment