Sakata la Mabilioni ya Fedha Uswis sasa limeingia
katika hatua mpya baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuitwa
kuhojiwa katika kamati ya Bunge ya Uchunguzi.
Kuitwa kwa Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema,
kunaonekana kuwa kunatokana na kuanzishwa hoja hiyo nae Bungeni huku akieleza
kuwa na orodha ya majini ya vigogo hao wanaodaiwa kuficha mabilioni hayo nje ya
nchi.
Akielezea katika Mtandao wa Mabadiliko wakati akijibu swali
aliloulizwa na mmoja wa wanajukwaa hilo kuhusiana na hatama ya sakati hilo,
Zitto aliwataka wananchi kutulia kwa vile uchunguzi unaendelea na kwamba kesho
(leo) anakwenda kuhojiwa na kamati hiyo ya uchunguzi.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment