![]() |
| Mbowe akiwa na Mawakili wake Polisi |
Search This Blog
Monday, July 15, 2013
Mbowe atinga Polisi Makao Makuu kwa mahojiano
Kwa wale ambao mnakumbuka kuwa siku ya ijumaa usiku wa manane Polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiongozwa na RCO wa Kinondoni walienda nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba usiku kwa lengo la kumkamata, Mbowe alikuwa safarini na alipitia Airport ya Dsm Hivyo kwenda kwake usiku ni jambo la kushangaza sana , leo amerejea kupitia Airport ya Dar na akaamua kwenda moja kwa moja Polisi ili kujua kulikoni.
Sunday, July 14, 2013
CHADEMA YASHINDA KATA ZOTE NNE UCHAGUZI MADIWANI ARUSHA
Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka Mshindi katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliokuwa ukizihusisha kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni pamoja na Elerai ushindi ambao umeonyesha wakazi wa Arusha kuwa na imani kubwa na chama hicho.
Matokeo hayo yamepokelewa kwa furaha kubwa sana na wafuasi wa chama hicho, viongozi pamoja na wafuatiliaji wa masuala ya siasa na wapenda mabadiliko kwa ujumla huku wakisema ushindi huo ni ishara ya wananchi kupaza sauti kwa chama kikongwe cha CCM kuwa wamechoshwa na mambo yalivyo kwa sasa.
1. Kata ya Themi
Chadema= 678
CCM =326
CUF =313
2.Kata ya Kimandolu
Chadema=2665
CCM =1169
3. Kata ya Kaloleni
Chadema =1019
CCM =389
COF =169
4.Kata ya Elerai
Chadema=1715
CCM=1239
CUF =213
Kauli ya Nape kabla ya Matokeo:
Katika majira ya 1:40 alasiri katika hali inayoonyesha Nape Nnauye kutambua matokeo mapema aliandika katika Mtandao wa Kijanii wa Jamiiforums akionyesha kukubali kushindwa mapema.
Aliandika haya: "Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)".
Matokeo hayo yamepokelewa kwa furaha kubwa sana na wafuasi wa chama hicho, viongozi pamoja na wafuatiliaji wa masuala ya siasa na wapenda mabadiliko kwa ujumla huku wakisema ushindi huo ni ishara ya wananchi kupaza sauti kwa chama kikongwe cha CCM kuwa wamechoshwa na mambo yalivyo kwa sasa.
![]() |
| Maskikitiko upande wa CCM |
Chadema= 678
CCM =326
CUF =313
2.Kata ya Kimandolu
Chadema=2665
CCM =1169
3. Kata ya Kaloleni
Chadema =1019
CCM =389
COF =169
4.Kata ya Elerai
Chadema=1715
CCM=1239
CUF =213
Kauli ya Nape kabla ya Matokeo:
Katika majira ya 1:40 alasiri katika hali inayoonyesha Nape Nnauye kutambua matokeo mapema aliandika katika Mtandao wa Kijanii wa Jamiiforums akionyesha kukubali kushindwa mapema.
Aliandika haya: "Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)".
Waziri mkuu apokea shehena ya mabomba ya gesi.
Shehena ya kwanza ya mabomba ya mradi wa gesi Mtwara imepokelewa bandarini leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Waziri Mkuu amesema kuwa anashangaa kuona baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wanapotosha ukweli wa mambo kuhusu mradi wa gesi Mtwara. Amesema lengo la serikali ni kuhamasisha uchumi wa gesi ili kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umaskini.
Aidha Waziri Mkuu ameishukuru serikali ya watu wa China kwa kuiwezesha serikali ya Tanzania kupata mkopo wa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa gesi Mtwara. Ametoa wito kwa wananchi, wanasiasa, wanahabari na mashirika ya dini na yale yasiyo ya kiserikali na wanaharakati wote kuungana na serikali katika kufanikisha kukamilika kwa mradi huu.
Awali akizungumza kuhusu mradi huo Waziri wa Nidhati na Madini Sospeter Muhongo amesema kuwa sasa serikali imeanza safari ya maendeleo. Alisema sehemu ya kwanza ilikuwa ni kugundua rasilimali zilizopo kwenye ardhi yetu na kwamba sehemu ya pili ni kuanza kuzivuna hizo rasilimali.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC amesema shehena hiyo ni awamu ya kwanza tuu na kwamba zitakuja jumla ya meli nyingine kumi na mbili zenye shehena kama hiyo. Meli iliyowasili ina mabomba karibia 3,400.
Wanajeshi saba Watanzania wauawa Dafur
Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha
Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan,
wanadaiwa kuwa wameuawa.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilisema
kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi
yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.
Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa
ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa
kwa wakati mmoja.
Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu
vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia,
lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania
kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe
alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya
askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto
uliokuwa umefurika maji.
Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini
Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba
askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.
Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa
Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari
1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.
Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.
Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa
kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana
na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali
ya DRC.
Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani
chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini
na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka
wanajeshi 850.
“Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na
ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa
majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko
Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia
waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.
“Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1914214/-/13b8bno/-/index.html
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1914214/-/13b8bno/-/index.html
Sheikh wa wilaya Arusha amwagiwa Tindikali
Wakati vumbi la matukio ya kigaidi ya
milipuko ya bomu kanisani na kwenye mkutano wa kampeni za Chadema
halijatulia, tukio lingine linalohusishwa na ugaidi limetokea wilayani
Arumeru kwa Sheikh wa wilaya hiyo, Said Juma Makamba aliyejeruhiwa kwa
kumwagiwa usoni kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali.
Sheikh Makamba anayekaimu nafasi hiyo alikutwa na
hayo kati ya Saa 4:00 hadi 5:00 usiku wa kuamkia juzi akitoka kusali
Tarawei na alilazwa wodi namba nne katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya
Mount Meru kwa matibabu.
![]() |
| IGP Said Mwema |
Jicho la kushoto la Sheikh huyo limeathirika, huku akiwa amebabuka na kuvimba usoni, kifuani, mkono wa kushoto na mgongoni.
Akizungumza kwa taabu kitandani kwake alikolazwa,
Sheikh Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei wilayani Arumeru
alisema alimwagiwa tindikali muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake
akitoka kuswali.
“Nilipotoka Msikitini, nilisindikizwa hadi
nyumbani na vijana wawili nilioongozana nao kutoka msikitini ambao
walihakikisha nimeingia ndani salama. Lakini kabla ya kulala nilitoka
nje kwa ajili ya kujisaidia kwenye choo cha nje ndipo nilimwona mtu
amesimama pembeni ya nyumba nikiwa najitahidi kumwangalia ili nimtambue,
ghafla alinimwagia kitu cha majimaji usoni,” alisema Sheikh Makamba.
Ingawa hataki kuingia kwa undani kuhusu
anaowatuhumu na sababu za kumwagiwa tindikali, Sheikh Makamba alisema
anadhani jambo hilo linatoakana na ugomvi wa madaraka msikitini hapo.
Katibu wa Bakwata Wilaya ya Arumeru, Sheikh Yahaya
Husein Mwangela aliwaomba polisi kuchunguza tukio hilo ili kuondoa hofu
miongoni mwa viongozi wa Bakwata.
Hili ni tukio la pili kwa viongozi wa Bakwata
Arusha kumwagiwa tindikali baada ya Oktoba mwaka jana, Katibu wa Baraza
hilo Mkoa wa Arusha, Abdukarim Njonjo kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa
kuwa ni bomu. Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa hadi jana kulikuwa
hakuna mtu aliyekamatwa.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Sheikh-wa-wilaya-arushiwa-tindikali/-/1597296/1914272/-/xxpuox/-/index.html
Saturday, July 13, 2013
Polisi Dar wamvamia Mbowe usiku wa manane
KUNDI la polisi wenye silaha za moto jana usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.
Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.
![]() |
| Mbowe |
Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.
Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.
Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.
RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
“Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.
“Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo,” alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.
Kauli ya CHADEMA
Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.
Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.
Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. “Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu,” alisema Slaa.
Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.
Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.
“Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?” alihoji Slaa.
Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.
Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.
Subscribe to:
Posts (Atom)




