Search This Blog

Wednesday, August 14, 2013

Ninani aliyeruhusu Ujenzi wa Ghorofa karibu na Ikulu ya Dar es salaam?



JENGO la ghorofa 19 lililojengwa karibu na Ikulu ya Dar es Salaam linadaiwa kuhatarisha maisha ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, UWAZI limefuatilia kwa umakini.
WALINZI WA OBAMA WADAIWA KUWA CHANZO
Kuna habari kwamba, ujio wa  Rais wa Marekani, Barack Obama nchini Tanzania Julai Mosi, mwaka huu ndiyo ulioibua mambo mengi juu ya kuwepo kwa jengo hilo kwani maafisa wake wa usalama walikataza watu kupanda hadi ghorofa ya 19 kwa maelezo kuwa wamegundua ni hatari kwa maisha ya viongozi, hasa Rais Obama aliyekuwa ikulu na Jakaya Kikwete.

Kikosi cha Majasusi wa Marekani (FBI) waliotangulia nchini miezi minne kabla ya ujio wa Obama ndiyo walioishtua serikali kwa kuwaambia watu wa usalama kuwa urefu wa jengo hilo ni hatari kwa ikulu kwa vile maadui wanaweza kulitumia.
FBI WALITEGA MITAMBO YAO JUU YA JENGO
Uchunguzi unaonesha kwamba, kwa vile FBI waliamini usalama wa ikulu ni mdogo kutokana na jengo hilo hivyo walilazimika kuweka mitambo yao juu yake na kuendelea kuwepo hapo kwa saa ishirini na nne kipindi chote cha ziara ya Obama.
FBI WALIONDOA MAGARI CHINI YA JENGO
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya ikulu vililitonya Uwazi kuwa, mbali na FBI kuweka mitambo yao ya kiusalama, pia walilazimika kuondoa magari yote yaliyokuwa yamepaki chini ya jengo hilo na kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuwa makini na ghorofa hilo.  Habari zaidi zinasema FBI hao walipendekeza jengo hilo livunjwe ama liwe la serikali na waishi wana usalama wanaolinda viongozi wa kitaifa.
“Baada ya FBI kutoa taarifa hizo ikulu ndipo ‘mchawi’ alipoanza kutafutwa hadi kufikia hatua ya kukamatwa walioruhusu ujenzi huo,” kilisema chanzo.
Waandishi wetu wamegundua kuwa pamoja na tahadhari iliyotolewa na FBI juu ya jengo hilo, lakini bado shughuli za kila siku zinaendelea sambamba na watu kuishi.

WALIOTOLEWA ‘KAFARA’ NI HAWA
Hivi karibuni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mwandamizi wa Majengo, Richard Maliyaga walipandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya kwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa hilo karibu na ikulu.
Washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo.
Washitakiwa walikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini watatu wafanyakazi wa serikali waliosaini hati ya shilingi milioni 50.
Souce: Global Publishers
http://paparaziblog.blogspot.com/2013/08/maisha-ya-rais-kikwete-yako-hatarini.html?spref=fb   

No comments:

Post a Comment