Search This Blog

Tuesday, January 8, 2013

MWANDISHI WA HABARI ISSA NGUMBA AMEUAWA KIGOMA



MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na Bastora iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake porini.

Habari ambazo zimepatikana na kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo imedai mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu ambao hawajajulikana.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa waliwasiliana na waandishi wa wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus Ijumaa aliyeeleza kuwa mwili wa marehemu umenyonga ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi mkono wa kushoto.

Mwili wake umepatikana jana katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea Jumapili siku moja baada ya kutoonekana kwake.

“Sisi tunaelekea wilaya ya Kakonko toka Kigoma mjini, lakini walioshuhudia mwili huo huko eneo la tukio waneleza kwamba kando ya mwili wake kumekutwa Bastora moja, haijafahamika iwapo ilikuwa inamilikiwa na marehemu ama nani, simu zake mbili na kwa mujibu wa Dkatari maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi,” alieleza Sonkolo.

Imeelezwa kwamba bastora iliyokutwa eneo la tukio imekutwa na ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo lakini alisema kwa sasa jeshi lake linangoja taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi wa mwili wake ikiwa ni pamoja na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo toka eneo la tukio.

Aidha akizungumza na gazeti hili Naibu Mharari wa kituo cha Radio Kwizera kinachorusha matangazo kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu, alisema kwamba tokea Januari 5 mwaka huu walikuwa majira ya saa 11 walikuwa wakijaribu kuwasiliana naye na simu zake zilikuwa zikiita bila ya kupokelewa mpaka jana ambapo zilikuwa hazipatikani.

“Maelezo kutoka kwa mke wake Rukia Yunus ni kwamba Marehemu aliondoka nyumbani kwake jioni na kumuaga mkewe kuwa alikuwa akienda madukani (center) lakini tokea hapo hakurudi wala kuonekana ambapo ilipofika Jumapili serikali ya kijiji ilianzisha msako mkali kumsaka mpaka jana asubuhi walipokutana na mwili wake porini,” alieleza Mhariri huyo.
Kwa mujibu wa Naibu Mhariri wa Radio Kwizera ya Ngara Seifu Upupu, Story ya mwisho kuhusu mfugaji aliyekula nyama ya uso ya kijana aliyekuwa akichunga mifugo yake aliiandika Novemba 24, tukio lililotokea nove 23, kijiji cha Muhange, wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
Kijana aliyetajwa kwa jina moja la Susuruka akiwa na majeraha sehemu za uso 
-----------------------------------
STORY HII HAPA
-----------------------------------
Kijana aliyetajwa kwa jina moja la Susuruka amejeruhiwa kwa kuliwa nyama za sehemu ya uso wake na mwajiri wake aliyekuwa akimfanyia kazi ya kuchunga ng’ombe katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Saimon Anthony amesema kuwa tukio hilo limetokea jana usiku (Ijumaa Nov 23, 2012) ambapo aliyefanya unyama huo ni Bw Imani Paulo.
Amesema kabla ya kumla nyama za usoni mfanyakazi wake, Bw Paulo alimuua mbwa wake na kisha kula ulimi wa mbwa huyo Jeshi la polisi wilayani Kakonko limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo amekamatwa ambapo baada ya kuhojiwa amesema hajui chochote kuhusu matukio hayo.
Taarifa zinasema kuwa majeruhi huyo amepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya matibabu

No comments:

Post a Comment