Search This Blog

Thursday, August 8, 2013

India yaikopesha Tanzania magari 675 ya Kijeshi

Jeshi la Wananchi (JWTZ) limepokea magari 675 kutoka India kwa mkopo na mengine bure ambayo yatafanya kazi kusaidia sekta ya afya.
Hafla ya kukabidhiwa magari hayo ilifanyika jana ambapo ilielezwa kwamba magari yote yatagharimu dola 36.56 za Marekani .
Akipokea magari hayo jana Dar es Salaam, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema magari hayo yametolewa kwa mkopo uliosainiwa Januari 26, 2012 kati ya Tanzania na India kupitia Benki ya Exim.
Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani kikicheza ngoma na Msewe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari hayo
“Mpaka sasa tumeshapokea magari 592 na makontena 16 yenye vifaa vya akiba. Magari 88 yaliyobaki tunatarajia kuyapokea Septemba 2013,” alisema Nahodha.
Alisema Serikali ya India imetoa magari manne kama zawadi kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya jeshini na kwa wananchi wa kawaida.”
Nahodha alisema magari hayo yamefika katika wakati mwafaka kwa kuwa yatasaidia kupunguza tatizo la usafiri na kwamba hayatatumika katika shughuli za ndani za kijeshi pekee bali yanatarajiwa kutumika kusomba mahindi katika mikoa mbalimbali nchini.
Alisema mkataba kati ya Tanzania na India ulifikiwa kutokana na uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili ambao ulianza tangu miaka ya 1950 chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Rais Jawaharlal Nehru.
Nay Balozi wa India nchini, Debnath Shaw alisema magari hayo ambayo yametengenezwa na Kampuni ya Ashok Leyland ya India, baadhi yao yatatumika kulinda amani katika nchi ya Democratic Republic of Congo (DRC).
“Magari haya yametengenezwa kustahimili hali ya nchi zinazoendelea…tunatarajia yatatumika kulinda amani DRC,” alisema Shaw.
Akizungumzia ulijo wa magari hayo, Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini, Meja Jenerali Davis Mwamunyange alisema kati ya magari yaliyopokelewa yapo maalumu kwa ajili ya shughuli za kijeshi.
Source:  http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/India-yakopesha-Tanzania-magari-675-ya-Jeshi/-/1597568/1940880/-/9htc9z/-/index.html

No comments:

Post a Comment