Search This Blog

Tuesday, July 16, 2013

Polisi asimulia wanajeshi walivyouawa Darfur

Wakati Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio hilo.
Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.
Askari wa JWT ambao ni Majeruhi Dafur
Gazeti hili limepata majina ya askari hao waliofariki kutoka vyanzo tofauti lakini limeshindwa kuwataja leo kwa kuwa JWTZ kupitia kwa msemaji wake, Kanali Kapambala Mgawe limesisitiza kuwa haliwezi kutangaza majina hayo hadi litakapowasiliana na jamaa za askari waliofariki.
Tukio lilivyotokea
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia, walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”
Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur, Kanali Mgawe alisema wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye msafara wa kusindikiza walinzi wa amani.
Makundi yanayopambana
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”
Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji hayo, askari huyo alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa amani wamepatwa na ganzi... “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu askari hao wauawe hali haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali walimohifadhiwa), tunasubiri uhakika.”
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana vifaa vya kisasa kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na wenzao kuwa na silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za mapambano yao,” alisema.

Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala ya amani.
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na kuwafundisha masuala mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja na wananchi waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi kushika silaha, wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na kutusindikiza wakati wa doria,” alisema.
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”
Kauli ya JWTZ
Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha uvumi wa majina yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu uliopo, jeshi haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu watakapotaarifiwa. “Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi ya kubadilisha kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa silaha za moto pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni namba saba ya Sheria za Majeshi ya Kulinda Amani.
Source:  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1916496/-/13b9r33/-/index.html

LEO 16/7/1995 NI SIKU YA PROF. KIGOMA ALI MALIMA

Mwaka 1995 ndiyo mwaka ambapo vyama vingi vilianza nchini Tanzania, lakini ni mwaka huu ambapo mwanachama wa CCM na aliyekuwa waziri katika serikali ya awamu ya Pili alipoamua kujiondoa CCM.
Nakumbuka ilikuwa 16/7/1995 siku hii CCM walipata mtikisikiko Mkubwa na kumfanya mwalim Nyerere kudondosha chozi hadharani kwani KADA wa CCM na aliyekuwa Waziri wa Elumu wa wakati huo Profesa Kighoma Ali Malima alipotangaza uwamuzi wake wa kuihama CCM. Katika uamuzi huo Mgumu kwake na mchungu kwa CCM na Mwalim Nyerere.
Lakini maskini hakudumu kwani baada ya kujiunga na chama cha NAREA (NRA) National Reconciliation Alliance na kufanya mkutano mkubwa huko Tabora, siku chache baadaye alifariki nje ya nchi.
Maswali bado ni mengi juu ya nini kilimsibu......., lakini leo tunakumbuka haya.

WITO WA KUSITISHA TOZO/KODI YA LAINI YA SIMU KILA MWEZI KUFUATIA MABADILIKO YA SHERIA YA KODI 2013

Sisi wananchi wa Tanzania:
• Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na serikali kufuta tozo/kodi mpya ya laini za simu iliyoanza kutumika baada ya sheria kupitishwa na Bunge Juni 2013.
• Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea maendeleo endelevu nchini kwetu.
• Bila mjadala mpana na mawazo chanya yaliyochambua masuala kwa undani kama msingi wa maamuzi, nchi itafanya maamuzi dhaifu yasiyosimama kwenye misingi ya hoja na ukweli wa mambo.
• Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linakandamiza wananchi na huenda likaturudisha nyuma kimaendeleo, ni kushindwa kuwajibika kama wananchi.
Waziri wa Fedha Mgimwa


Tunapinga kodi ya laini za simu
KWA SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.

KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.

KWA SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake. Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.

KWA SABABU:- Kodi hii ni juu ya ongezeko la kodi mbalimbali katika huduma za simu za mkononi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ushuru kutoka 12% kwenda 14.5% na pia kodi hii kutozwa kwa huduma zote ingawa awali ilitozwa kwa huduma ya matumizi ya kuongea. Hivi sasa utumiaji wa internet, kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu za mkononi unatozwa kodi. Ongezeko hili pekee limeshafanya huduma za simu za mkononi kupanda gharama kwa kiasi kikubwa. Ongezeko hili la shs 1,000 litazidi kuwaumiza wananchi.

KWA SABABU: - Kodi hii pekee inampunguzia mtumiaji muda wa maongezi na huduma zingine za simu za mkononi ikiwa ataendelea na matumizi yake ya mwezi kama kawaida. Kwa mfano mtumiaji akitumia kifurushi cha bei ya shs 475 inayompa dakika 20 za maongezi, 50 MB za data, na sms 100 kwa masaa 24, kwa kodi ya shs 1,000 kwa mwezi ni sawa na serikali kuchukua siku mbili za kifurushi hiki kila mwezi au ni sawa na kuchukua dakika 40 za maongezi, 100MB za data na sms 200 kila mwezi.

KWA SABABU:- Huduma ya simu za mkononi siyo anasa na ni sehemu muhimu ya mawasiliano na kiungo kinachochangia kurahisisha harakati za maendeleo. Kwa mfano wakulima hutumia huduma hizi katika kuuza mazao yao na kupokea fedha; akina mama wajawazito hupelekewa taarifa muhimu kuhusu afya zao; wanafunzi kupitia internet wanaweza kupata habari muhimu zinazohusiana na masomo yao nk. Kodi hii itawanyima fursa ya kutumia huduma hizi muhimu.

KWA SABABU:- Serikali inaweza punguza matumizi yake mengineyo (safari, posho, semina, manunuzi ya magari na kudhibiti ufisadi) hivyo kufidia pengo litakalosababishwa na kusitisha tozo/kodi ya laini ya simu.

KWA SABABU:- Pia, utafiti uliofanywa na Interfaith Standing Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja (takriban shs trilioni 1. kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi. Tunaitaka Serikali yetu iongeze ufanisi wa kukusanya kodi kutoka vyanzo vilivyopo tayari na kuondoa misamaha kwa hivyo itaziba pengo la shs billioni 264 kutoka kwa kodi ya laini ya simu za mkononi.

MWISHO
Tunakuomba ufikishe ujumbe kwa wengine kwa kuwapa link ya hii petition ili nao washiriki maamuzi haya muhimu.
Tembelea: http://www.avaaz.org/en/petition/WITO_WA_KUSITISHA_TOZOKODI_YA_LAINI_YA_SIMU_KILA_MWEZI_KUFUATIA_MABADILIKO_YA_SHERIA_YA_KODI_2013/?pv=4

Monday, July 15, 2013

Analysis ya Matokeo ya Udiwani katika Uchaguzi wa Udiwani hivi karibuni.

WILAYA
KATA
CCM
CHDM
CUF
NCCR
DP
APPT
ADC
NRA
TOTAL
WINNER
former
Loser
Nachingwea
Stesheni
806
327
480
-
-
-
-
-
1613
CCM
CCM

Sengerema
Nyampulukano
1073
1476
38
45
-
-
-
-
2632
CHDM
CCM
CCM lost
Sengerema
Lugata
2214
1044
-
-
-
-
-
-
3258
CCM
CCM

Muheza
Genge
347
326
6
-
-
-
-
-
679
CCM
CCM

Muheza
Tingeni
362
244
4
-
-
-
-
-
610
CCM
CCM

Bahi
Ibungule
863
248
-
-
-
9
-
-
1120
CCM
CCM

Chemba
Dalai
1361
1027
377
-
-
-
-

2765
CCM
CCM

Mbinga
Langiro
-
-NO
-
-C
-O
-N
-T
-E
-ST
CCM
CCM

Serengeti
Manchilla
676
625
16
-
-
-
-
-
1317
CCM
CCM

Mbeya
Iyela
1163
1918
-
12
20
-
-
-
3113
CHDM
CCM
CCM lost
Mufindi
Mbalamaziwa
1420
184
-
-
-
-
-
-
1604
CCM
CCM

Kilolo
Ng'ang'awe
686
217
-
-
-
-
-
-
903
CCM
CCM

Bukombe
Runzewe west
612
529
-
-
-
-
153

1294
CCM
CCM

Temeke
Mianzini
1283
315
494
-
-
-
25
9
2126
CCM
CCM

Ulanga
Minepa
1196
1029
-
-
-
-
-
-
2225
CCM
TLP
TLP lost
Kilombero
Ifakara
3746
4106
-
-
-
-
-
-
7852
CHDM
CCM
CCM lost
Kilosa
Masanze
948
638
-
-
-
-
-
-
1586
CCM
CCM

Monduli
Makuyuni
1547
360
-
-
-
-
-
-
1907
CCM
CCM

Arusha
Themi
326
678
313
-
-
-
-
-
1317
CHDM
CHDM

Arusha
Kimandolu
1169
2665
-
-
-
-
-
-
3834
CHDM
CHDM

Arusha
Kaloleni
389
1019
169
-
-
-
-
-
1577
CHDM
CHDM

Arusha
Elerai
1239
1715
213
-
-
-
-
-
3167
CHDM
CHDM

Babati
Bashnet
1130
2008
-
-
-
-
-
-
3138
CHDM
CCM
CCM lost
Mbulu
Dangobesh
968
1558
5
-
-
-
-
-
2531
CHDM
CCM
CCM lost
Singida
Iseke
791
831
96
-
-
-
-
-
1718
CHDM
CHDM

Mtwara
Mnima
918
206
626
414
-
-
-
-
2164
CCM
CUF
CUF Lost

Kura kata zote
27233
25293
2837
471
20
9
178
9
56050




Asilimia
49%
45%
5%
1%
0%
0%
0%
0%
100%




Positions of the Parties before and After.


CCM
CHADEMA
CUF
TLP
TOTAL
Wards Before
19
5
1
1
26
Wards After
16
10
0
0
26

Gainers and Losers

Losers (Former Seats lost)
Gainers (New seats gained)
Net Final position
TLP – Lost 1 to CCM
CHADEMA – Gained 5 from CCM
CHADEMA GAINED 5
CUF – Lost 1 to CCM
CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
CCM LOST 3
CCM – Lost 5 to CHADEMA

TLP – LOST 1
CHADEMA - none

CUF – LOST 1

Ni matumaini yangu kuwa namba zinajieleza vizuri.

1. Asilimia ya Kura:
CCM wamepata 49%, Chadema 45%, CUF 5% vyama vingine 1%

2. Ushindi wa Jumla wa Kata:
CCM wameshinda kata 16 (moja wameshinda bila kupiga kura kwa kuwa hakukuwa na wagombea wa upinzani) na Chadema wameshinda kata 10.

3. MLINGANISHO NA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA UCHAGUZI 2010

  • Chadema wameongeza viti 5
  • CCM wamepoteza viti 3
  • TLP na CUF wamepoteza kiti kimoja kimoja.

Mbowe atinga Polisi Makao Makuu kwa mahojiano

Mbowe akiwa na Mawakili wake Polisi

Kwa wale ambao mnakumbuka kuwa siku ya ijumaa usiku wa manane Polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiongozwa na RCO wa Kinondoni walienda nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba usiku kwa lengo la kumkamata, Mbowe alikuwa safarini na alipitia Airport ya Dsm Hivyo kwenda kwake usiku ni jambo la kushangaza sana , leo amerejea kupitia Airport ya Dar na akaamua kwenda moja kwa moja Polisi ili kujua kulikoni.

Ameambatana na Mawakili wawili, Nyaronyo Kicheere na Peter Kibatala majira ya saa tisa na nusu aliingia Makao Makuu ya Polisi na huko wanaendelea na Majadiliano.

Jambo la kushangaza ni kuwa mahojiano yao yanahusu mambo yafuatayo;

1. Kuwa tamko la Kamati Kuu kuwa Polisi walihusika na mlipuko wa Bomu Arusha... Itakumbukwa alishahojiwa tena na akina Chagonja na mpaka leo hakuna taarifa zozote wazi.
2. Kuwa Polisi wanatumiwa na CCM ndio maana wanaisaidia CCM Katika chaguzi mbalimbali ......na hata bomu la Arusha ilikuwa sehemu ya mkakati huo.
3. Kwamba kauli kuwa JK na Bunge kutokuonyesha dalili zozote za kusikitishwa na hata kushindwa kuhudhuria mazishi ni dalili za serikali kuhusika katika tukio hilo.

Kwa ufupi hayo ndio majadiliano yanayoendelea tangu saa tisa na nusu jioni. Hii , nitaendelea kuwapa updates kadiri nitakavyozipokea.

Maswali ya kufikirisha:
1. Hivi wakina Chagonja Ripoti ya bomu Arusha iko wapi mpaka ahojiwe tena leo upya.
2. Hivi kama Polisi hawatumiki kuisaidia CCM nini maana ya mahojiano ya leo kama sio kule kule kuendelea kutumika kwa Polisi?
3. Hivi, haya yataendelea mpaka lini kama hawa ndio polisi wetu, yaani alihojiwa na wakina Chagonja, Mungulu, na Makamishina kibao wa makao makuu ya polisi , leo anaitwa kuhojiwa na RCO wa Kanda ya Kinondoni na Rpc wake , hivi huko polisi hakuna kuheshimu tena vyeo?

Chagonja kanyoosha mikono ndio maana wanaanza kutafuta pa kutokea?

Source:  http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/487362-mh-mbowe-afika-polisi-makao-makuu-kwa-mahojiano.html

Sunday, July 14, 2013

CHADEMA YASHINDA KATA ZOTE NNE UCHAGUZI MADIWANI ARUSHA

Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka Mshindi katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliokuwa ukizihusisha kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni pamoja na Elerai ushindi ambao umeonyesha wakazi wa Arusha kuwa na imani kubwa na chama hicho.

Matokeo hayo yamepokelewa kwa furaha kubwa sana na wafuasi wa chama hicho, viongozi pamoja na wafuatiliaji wa masuala ya siasa na wapenda mabadiliko kwa ujumla huku wakisema ushindi huo ni ishara ya wananchi kupaza sauti kwa chama kikongwe cha CCM kuwa wamechoshwa na mambo yalivyo kwa sasa.

Maskikitiko upande wa CCM
1. Kata ya Themi
Chadema= 678
CCM =326
CUF =313

2.Kata ya Kimandolu
Chadema=2665
CCM =1169

3. Kata ya Kaloleni
Chadema =1019
CCM =389
COF =169

4.Kata ya Elerai
Chadema=1715
CCM=1239
CUF =213


Kauli ya Nape kabla ya Matokeo:
Katika majira ya 1:40 alasiri katika hali inayoonyesha Nape Nnauye kutambua matokeo mapema aliandika katika Mtandao wa Kijanii wa Jamiiforums akionyesha kukubali kushindwa mapema. 

Aliandika haya: "Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)". 

Kauli ya JWTZ kwa Askari wake 7 waliouawa Sudan