TASWIRA ZA ABSALOM KIBANDA AKIWA HOSPITALINI MUHIMBILI BAADA YA KUVAMIWA NA KUUMIZWA VIBAYA
Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi, akimjulia hali Absalom Kibanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Mwenyekiti
wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (kulia) akimpa pole, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Habari Corporation, Hussein Bashe.Baadhi ya majeraha aliyoyapata Kibanda.
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation, Absalom Kibanda,
usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiojulikana wakati akivuka
geti kuingia nyumbani kwake na gari yake aina ya Nissan.
Wavamizi hao walivunja kioo cha gari lake na kumchomoa ambapo walimpiga mapanga na kumjeruhi vibaya jicho la kushoto. Baada ya kufanyiwa unyama huo Kibanda alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.

(PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment